Je, Wajua? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, Wajua?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Jan 18, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jan 18, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,490
  Likes Received: 81,808
  Trophy Points: 280
  Katika uchunguzi wa Ernst and Young kuhusiana na ufisadi wa EPA
  katika mwaka 2005/2006 iligunduliwa kiasi cha shilingi bilioni 133
  ziliibwa na kuwanufaisha mafisadi. Inawezekana kabisa kama uchunguzi huo
  ungeanza tangu 1995 wakati Mkapa alipoingia madarakani si ajabu kiasi hicho
  kingeongezeka maradufu au hata zaidi. Pamoja na kuambiwa baadhi ya pesa hizo zimerudishwa lakini hadi hii leo hakuna uthibitisho wowote unaonyesha pesa hizo zimerudishwa.

  Meremeta nayo zilichotwa shilingi 155 billioni. Ufisadi wa Meremeta hadi
  hii leo haujachunguzwa maana tumeambiwa unahusiana na usalama wa nchi. Kama wataalamu wa Ernst and Young wangepewa nafasi ya kuchunguza ufisadi uliofanywa ndani ya Meremeta kuna uwezekano kiasi hicho kilichoibwa labda kingeongezeka zaidi.

  Richmonduli ala Dowans kampuni ya kitapeli nayo zilichotwa 172 billioni na kulipwa kampuni ya kitapeli ambayo ilikuwa haijui chochote kuhusu umeme na wala haikuwa na makao yake majuu Houston, US achilia mbali kuwa na branch.

  Jumla ya wizi wote huu ni shilingi 460 billioni na hii ni kwa kipindi kifupi sana. Pesa ambayo ingeweza kabisa kuwapatia mikopo ya 100% wanafunzi wote wa vyuo vikuu, kununua madawa katika mahospitali yetu na vitanda na kujenga madarasa ili wanafunzi wa shule za msingi ambao hawakupata nafasi ya kuendelea na masomo ya sekondari kutokana na 'ukosefu wa madarasa' kupata nafasi hiyo na kuwapatia mafunzo ya kina walimu wa shule za msingi na sekondari ili kupumguza upungufu mkubwa wa walimu uliokuwepo.

  Tanzania si maskini kiasi hicho, bali ni ufisadi wa hali ya juu na gharama kubwa za uendeshaji wa serikali yetu inayotaka kujiendesha kwa fahari kubwa, kusaini mikataba mibovu ya rasilimali zetu ndiyo inayoifanya nchi yetu kutopata maendeleo yoyote yale miaka nenda miaka rudi.
   
Loading...