Je Wajua Watanzania Hawajawahi Kuwa na Katiba Yao?Katiba Mpya ya Samia Ni Bonge la Fursa Kupata Katiba ya Kwanza ya Wananchi!, Tuchangamkie Fursa Hii!

Je Wajua Watanzania Hawajawahi Kuwa na Katiba Yao?Katiba Mpya ya Samia Ni Bonge la Fursa Kupata Katiba ya Kwanza ya Wananchi!, Tuchangamkie Fursa Hii!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
57,101
Reaction score
128,716
Wanabodi
Habari za Jumapili?.
Hii ni makala yangu kwenye gazeti la Nipashe la leo.
Safari ya Katiba .jpg


Ukifungua katika ya JMT ya mwaka 1977, neno la kwanza kwenye katiba ni neon "KWA KUWA SISI Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tumeamua rasmi na kwa dhati kujenga katika nchi yetu jamii inayozingatia misingi ya uhuru, haki, udugu na amani: KWA HIYO, BASI, KATIBA HII IMETUNGWA NA BUNGE MAALUM LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, kwa niaba ya Wananchi, kwa madhumuni ya kujenga jamii kama hiyo"
Kumaanisha kwamba katiba inapaswa kuwa ni katika ya wananchi, lakini ukweli halisi uliopo, Watanzania hawajawahi kuwa na Katiba yao ya wananchi!, wananchi au Watanzania, hawajawahi kushirikishwa kutengeneza katiba yao, hivyo hii hoja ya Katiba Mpya ya Samia, ni bonge la fursa kwa Watanzania, kupata Katiba yaa ya kwanza ya Wananchi!, hivyo natoa wito kwa Watanzania wenzangu, tuchangamkie kwa dhati fursa hii, ambayo ipo kwenye Dira ya Taifa na kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM, ambapo Rais Samia akilizindua Bunge jipya, aliahidi huu mchakato kuanza ndani ya siku 100 za kwanza!.

Lengo la Makala hizi za Katiba: Ni Kutoa Elimu kwa Umma kuhusu Katiba, Sheria, Haki na Wajibu.
Kufuatia mwaka huh ni mwaka wa kuanza kwa mchakato mwingine wa katiba mpya, ambayo hii sasa ni Katiba ya Samia, kufuatia ule mchakato wa Katiba ya Warioba kuishia njiani bila kutupatia katiba mpya, ili tupate katiba mpya ambayo ni katika bora, ni muhimu kuyaangazia mapungufu ya katika cii iliyopo ili yasijirudie kwenye katiba mpya. Wananchi wakielimishwa kuhusu katiba, watakuwa na uwezo zaidi kutoa maoni yao wanataka katika maya ya aina gani yenye mambo gani.
View: https://youtu.be/ZJIKhnZCf04?si=DFGXM5uuL_YJghBB

Katiba Ndilo Jambo Kuba Kuliko Mambo Menige Yote na Ndilo Jambo Muhimu Kiliko Jambo Jengine Lolote!.
Moja ya mambo makubwa yenye maslahi makubwa kwa taifa, kwenye Dira ya Taifa 2025-2550 na kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM, 2025-2030 ni hoja ya kuanza kwa mchakato wa katiba mpya. Na Rais Samia wakati akilizindua Bunge jipya, aliahidi, mchakato kuanza ndani ya siku 100 za kwanza za awamu hii. Kwa vile katiba ndio kitu muhimu kuliko kitu kingine chochote, pamoja na mambo mengine, lakini mwaka huu makala hizi zitajikita zaidi kwenye utoaji wa elimu ya katiba, sheria, haki na wajibu, ili kuwaelimisha Watanzania kuijua katiba yao hii iliyopo, mapungufu yake, ili muda wa kutoa maoni kuhusu katiba mpya, wengi watoe maoni ya kitu wanachokijua.

Kwa mujibu wa wataalamu wa sheria kote ulimwenguni wanasisitiza katiba inahitaji kupitiwa mara kwa mara kuhakikisha inakwenda na wakati uliopo. Kiukweli kabisa, Katiba yetu hii iliyopo, ilipitwa na wakati kitambo, kiasi kwamba mpaka yametokea ya kutokea, tungefanya mabadiliko ya msingi kwa wakati, kilichotokea October 29, kisingetokea.

Naomba tuanze na historia ya katiba ya Tanzania.

Katiba ya Kwanza: Katiba ya Uhuru ya mwaka 1961- Haikuwa ya Watanzania, ni Katiba ya Waingereza Ilitungwa Ungereza!
Tanzania tulianza tukiwa Tanganyika, hivyo Katiba ya kwanza ni katiba ya Tanganyika ya mwaka 1961 ambayo ni katiba ya uhuru, ilitokana na azimio la sheria ya uhuru (Order in Council) lililopitishwa katika Bunge la Uingereza na kuletwa Tanganyika kama Katiba ya awali. Katiba hii ilitengenezwa Westminster na Waingereza nchini Uingereza na kuletwa kwetu bila kumshirikisha Mtanzania yeyote, hyaani katiba ya kuletewa. Hata hivyo Katiba hii ilikuwa na mapungufu kadhaa kubwa ikiwa mambo mengi ya kutegemea kufanyiwa maamuzi toka Uingereza chini ya Malkia ambaye ndiye alikuwa mkuu wa nchi yetu.

Katiba ya Pili: Katiba ya Jamhuri ya Mwaka 1962: Haikuwa Katiba ya Wananchi, ni katika ya Wabunge wa TANU!
Tarehe 9 Desemba 1962, Tanganyika ilijigeuza kuwa Jamhuri, hivyo tukaachana na katiba ya kupewa na Waingereza, tukatengeneza katiba yetu ya pili, yaani katiba ya Jamhuri, ila bado hatukuhusisha wananchi, bali ni wabunge 71 wa TANU ambao walijigeuza na kuwa Bunge Maalum la Katiba lililopitisha Katiba hii. Katiba ya 1962 ndiyo ilianzisha mfumo wa Urais wa kifalme ambaye pia alikuwa Mkuu wa nchi, Amiri Jeshi Mkuu na kiongozi wa serikali. Baraza la Mawaziri wote waliwajibika kwa Rais badala ya Bunge.

Katiba ya Tatu: Katiba ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ya mwaka 1964- Wananchi Hawakushirikishwa ni Bunge la Tanganyika Tuu Lilitunga!
Mwaka 1964 tulipoungana na Zanzibar na kuwa Tanzania, tukapitisha katiba ya tatu ya Muungano. Katiba hii ilitokana na hati za makubaliano ya muungano ambazo zilifikiwa kuelekea siku ya muungano ulifanyika tarehe 26 Aprili 1964. Katiba hii ilianzisha mambo 11 ya Muungano ambayo kwa sasa yamefikia 22. Katiba ya Tanganyika pamoja na Tanganyika yenyewe vilikufa kifo cha kawaida wakati wa kuanzisha muundo wa serikali mbili. Rais wa Zanzibar alikuwa pia Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano na mjumbe wa Baraza la mawaziri. Katiba hii ilianzishwa kwa tamko la Rais na kuridhiwa na Bunge la Tanganyika tuu, japo inasemwa pia iliridhiwa na na Baraza la Wawakilishi la Zanzibar lakini hakuna kumbukumbu zozote za maandishi kuthibitisha Zanzibar waliridhia. Hii ilikuwa iwe ni Katiba ya muda tuu wa mpito ya Muungano ambayo ingetumika kwa muda wa mwaka mmoja tu na iliweka utaratibu wa kuandaa Katiba ya kudumu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuunda Tume ya Katiba na Bunge la Katiba ili kuhakikisha ushiriki wa wananchi wa Jamhuri ya Muungano unakuwepo. Tume hii ndiyo ya kwanza ya Katiba ya Tanzania na ilikuwa chini ya uongozi wa Mheshimiwa Rashid Mfaume Kawawa.

Katiba ya Nne ni Katika ya Muda ya Mpito ya Mwaka 1965: Haikushirikisha Wananchi, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Katiba hii ya mwaka 1965 ilijulikana kama Katiba ya mpito na ndiyo iliyorasimisha nchi kuwa ya chama kimoja cha siasa. Hata hivyo kulikuwa na vyama viwili. Tanganyika iliongozwa na Tanganyika African National Union (TANU) wakati Zanzibar ikiwa chini ya Afro Shirazi Party (ASP). Katiba ya chama cha TANU ilikuwa sehemu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Jambo hili nalo limezua mjadala miongoni mwa wananchi. Katiba hii ilitokana na mchakato wa Tume ya Rais ya Katiba iliyokusanya maoni ya baadhi ya wananchi. Ghafla, mambo ya Muungano yalianza kuongezeka na utata wa uhuru (autonomy) wa Zanzibar nao ukazidi jambo ambalo limeendelea kutatiza muungano kwa muda mrefu.

Katiba ya Tano: Katiba ya Kudumu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977- Haikushirikisha Wananchi, Hii ni Katiba ya CCM ya Mwaka 77, ikageuzwa kuwa Katiba ya Nchi!.
Hii iliyopo sasa kwa jina maarufu la Katiba ya JMT ya Mwaka 1977 ilitokana na Tume ya Rais iliyokuwa na wajumbe 20 (10 toka kila upande wa Muungano) ikiongozwa na Sheikh Thabit Kombo na Katibu wake akiwa Ndugu Pius Msekwa kuunganisha vyama, hivyo ilikuwa Katiba ya CCM ambayo ilizaliwa baada ya kuunganisha vyama vya TANU na ASP tarehe 5 Februari 1977. Katiba yenyewe ilijikita katika misingi mikuu mitatu ambayo ni Urais wa kifalme, mfumo wa chama kimoja cha siasa na muundo wa serikali mbili kuelekea serikali moja. Katiba hii ilipitishwa na Bunge maalum lililoteuliwa na Rais kutokana na Bunge la kawaida.

Wiki Ijayo Nitazama ndani ya Katiba ya JMT ya Mwaka 1977.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali
 
Huyu Rais kivuli ambaye hana ustahimilivu kwa wapinzani na wakosoaji utegemee akupe katiba bora?.

Huyu Rais kivuli ambaye akikosolewa anakupoteza utegemee akupe katiba bora?.

Huyu SAMIA ambaye hataki ushauri wala maoni zaidi ya sifa na kumuabudu utake akupe katiba bora?.

Huyu jambazi ambaye haeshimu katiba iliyopo kwa kuiita ''kijitabu'' zaidi ya kuona misaafu ya dini ndio ya maana kuliko sheria za nchi akupe katiba bora?.

Huyu Jambazi ambaye yuko tayari kuharibu maisha ya maelfu ili abaki ikulu utegemee akupe katiba bora?.

Huyu ambaye alishirikiana na majambazi wenzie kumnyang'anya mtangulizi wake ofisi ya rais bila utaratibu utegemee akupe katiba bora?.

Amken acheni kuota, nyuma ya samia kuna mamia ya makundi ya kijambazi ambayo yananufaika na umasikini+ujinga wa mtanzania, na hawako tayari kwa mabadiriko, ndiomaana makundi hayo kila wanachokitaka wanapata ndani ya muda mfupi, lkn mtanzania wa kawaida akidai haki zake hapati na huenda hata kile kidogo akaporwa.

Samia hamalizi miaka 5, lazima watifuane, wasalitiane na watahujumiania wao kwa wao mwishoe wataanza kuwindana na kutoana roho ili kulinda maslahi yao.

Mark hii post tutakutana au kwa ambao watakuwa HAI watayashuhudia haya, siasa za Tanzania zinakwenda kubadirika, usiwehuke na hizi harakati wanazifanya sasa.
 
Huyo mama asijichetue, katiba pendekezwa ipo, mchakato uendelee ulipoishia. Hakuna haja ya kutumia mabilioni ya shilingi ya walipa kodi kisa kumsafisha huyu mama.

Asitake kujisafisha kwa gharama za walipa kodi afu badae mchakato aukwamishe kwa makusudi. Tume ya Warioba ilitumia mabilioni ya shilingi na mchakato maccm wakaukwamisha.

Tuendelee tulipoishia, aache udwanzi.
 
Back
Top Bottom