Je, wajua majukumu ya Mwenyekiti wa mtaa?

Adolph Sendeu

JF-Expert Member
Apr 21, 2009
269
250
Majukumu ya Mwenyekiti wa Mtaa
  1. Atakuwa ndiye Mkuu wa Serikali ya Mtaa;

  2. Atakuwa na wajibu wa kuitisha na kuongoza mikutano yote ya Halmashauri ya Mtaa, pamoja na Mikutano Mikuu ya Mtaa. Lakini endapo Mwenyekiti hayupo katika mkutano wowote, wajumbe wa mkutano unaohusika wanaweza kuchagua Mwenyekiti wa muda wa mkutano huo;

  3. Atakuwa mwakilishi wa Mtaa kwenye Kamati ya Maendeleo ya Kata; WARD DEVELOPMENT COMMETEE

  4. Atawahudumia kwa usawa wanaMtaa wote, bila kujali tofauti za Kisiasa, Kijinsia au za Kidini;

  5. Atakuwa mfano wa uongozi bora na utendaji bora wa kazi, kwa kuwa na shughuli zake mwenyewe za kujitegemea, ambazo zaweza kuigwa na wanaMtaa wenzake.
 
Wanajamvi, nimeweka majukumu ya mwenyekiti wa mtaa nikiwa nataka kuwauliza, na kuwaomba wengi wenu humu ambao ni wasomi, je kuna ambaye ni mwenyekit wa serikali ya mtaa humu? Je kuna hata mwenye wazo la kugombea uenyekiti wa mtaa anapoishi? jamani amkeni, nyinyi ambao ni wasomi mnaacha kushika hizi nafasi nyeti mnaziacha kiholela kwa watu ambao wengi wao hawana vision wala hawajui kuwa wanagombea nafasi kana hizo. sanasana mtu akikuambia ni kwamba anataka elfu tano tano za kugonga mihuri na kuamua kesi za watu
 
Adolph Sendeu

JF-Expert Member
Apr 21, 2009
269
250
naomba na hatua za kumfukuza mwenye kiti wa mtaa au kijiji

Madaraka na Majukumu ya Mkutano Mkuu wa Kijiji[hariri | hariri chanzo]

 • Kusimamia na kuwajibisha watendaji.
 • Kuweka taratibu za namna ya kuitisha vikao vya dharura.
 • Kupitia Mkutano Mkuu Maalum wa uchaguzi kuwachagua Mwenyekiti wa kijiji na wajumbe wa halmashauri ya Kijiji.
 • Kujaza nafasi za viongozi wa halmashauri ya Kijiji zilizo wazi.
 • Kujadili na kupokea au kukataa taarifa za utekelezaji wa shughuli za kijiji kutoka halmashauri ya kijiji.
 • Kupokea, kujadili na kupitisha au kukataa taarifa ya mapato na matumizi ya fedha za kijiji.
 • Kupokea, kujadili na kupitisha au kukataa mapendekezo ya kodi, ushuru na vyanzo vingine vya mapato ya kijiji.
 • Kupokea na kujadili taarifa ya makusanyo ya fedha za kodi, ushuru na mapato mengine ya kijiji.
 • Kupokea, kujadili na kufanyia maamuzi mapendekezo ya serikali ya kijiji ya kutunga sheria ndogondogo.
 • Kupokeam kujadili na kuyafanyia maamuzi masuala kuhusu ugawaji wa ardhi na matumizi ya rasilimali zingine za kijiji.
 • Kuhoji, kudadisi, kukosoa, kukubali au kukataa taarifa na mapendekezo ya serikali ya kijiji.
 • Kuondoa madaraka serikali ya kijiji au mjumbe yeyote kabla ya muda wao.
 • Kupitisha azimio la kukaripia rasmi mjumbe yoyote wa halmashauri au halmashauri kwa ujumla kwa utendaji mbovu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom