Je, wajua kuwa kwa Sasa Tanzania tumeanza kuchukiana kwa sababu za kiitikadi?

KakaKiiza

KakaKiiza

JF-Expert Member
11,082
2,000
Hali huko uswahilini kunaanza kuota mbegu ya chuki kutokana na sababu za kisiasa!Inabidi hatua za makusudi zichukuliwe vinginevyo kama taifa tunakoelekea siko Tuombe Mungu.

Baba wa Taifa alituacha tukiwa na upendo kwamaana ya kupendana wote tukiwa taifa moja leo ukiongelea mambo ya siasa za CCM Unaambiwa nyie mnakandamiza haki uhuru wakujieleza na kuwa CCM ni madkiteita.

Ukikuta kunaongelewa siasa za upinzani utasikia makuadi wa mabeberu mnakumbatia ushoga, nawanaenda mbali kwa kuwataja nakuwatukana viongozi wa upinzani hapa naongelea uswahilini ndiyo usiseme matusi hadharani na hakuna mamlaka inayozungumza juu ya utengamano huu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rooney

Rooney

JF-Expert Member
3,555
2,000
Hali huko uswahilini kunaanza kuota mbegu ya chuki kutokana na sababu za kisiasa!Inabidi hatua za makusudi zichukuliwe vinginevyo kama taifa tunakoelekea siko Tuombe Mungo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Itakua uswahili ya huku mitandaoni ,
Tz hiihii itokee lets say msiba watu wakutenge kisa siasa,No way,ktakua na sbab zngne ulipoona.
Unless una vivid example itoe,bila hvyo unafanya uchochezi bila kujua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
silent kills

silent kills

JF-Expert Member
568
1,000
dalili za hayo unayosema ndo naziona na ndo maana ilifikia mahali ccm hawavai madera yao uraiani wanaenda kuvalia kwenye zile fuso zinazowasomba kwenye mikutano yao
 
Kingsharon92

Kingsharon92

JF-Expert Member
6,711
2,000
Toa mifano - wapi umekuta watu wakitengana (misiba, harusi, michezo) nk sababu za kisiasa na itikadi??
Ni huko ufipa sisi huku kwetu wanasema vyuma vimekaza ila kama kawaida wanapiga kazi na maisha yanasonga hayo ya chuki anayajua mleta thread
 
V

Vumilika

JF-Expert Member
778
1,000
Hali huko uswahilini kunaanza kuota mbegu ya chuki kutokana na sababu za kisiasa!Inabidi hatua za makusudi zichukuliwe vinginevyo kama taifa tunakoelekea siko Tuombe Mungu. Baba wa Taifa alituacha tukiwa na upendo kwamaana ya kupendana wote tukiwa taifa moja leo ukiongelea mambo ya siasa za CCM Unaambiwa nyie mnakandamiza haki uhuru wakujieleza na kuwa CCM ni madkiteita...ukikuta kunaongelewa siasa za upinzani utasikia makuadi wa mabeberu mnakumbatia ushoga, nawanaenda mbali kwa kuwataja nakuwatukana viongozi wa upinzani hapa naongelea uswahilini ndiyo usiseme matusi hadharani na hakuna mamlaka inayozungumza juu ya utengamano huu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hayo mambo ya kutengana katika shughuli za kijamii kwa sababu za kisiasa yapo Unguja na Pemba lakin kwa bara kama yameanza basi ni mtihani
 
Smart911

Smart911

JF-Expert Member
41,230
2,000
Siasa ya sasa ni ya chuki na uoga mwingi...

Watu wanapuliza na kungata...


Cc: mahondaw
 

Forum statistics


Threads
1,424,632

Messages
35,068,863

Members
538,026
Top Bottom