Je wajua? Jonas Mkude ni mchezaji pekee aliyedumu Simba tangu ilipochukua VPL kwa mara ya mwisho?

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,252
mkude.jpg

Imepita misimu mitano tangu Simba itwae taji la VPL kwa mara ya mwisho. Klabu hiyo ilitangaza ubingwa wake wa ligi kwa mara ya mwisho mwanzoni mwa mwezi May 2012 msimu wa 2011/2012 baada ya kuichapa Yanga 5-0 uwanja wa taifa.

Wachezaji wengi wameshaondoka na wengine kuingia ndani ya kikosi cha Msimbazi lakini ni wachezaji wanne tu ambao kwa sasa wapo Simba na walikuwepo wakati Simba ikitwaa kombe la ligi kuu Tanzania bara misimu mitano iliyopita.

Jonas Mkude ndiye mchezaji wa Simba aliyekuwepo kwenye kikosi kilichochukua ubingwa wa VPL mwaka 2012 na ameendelea kudumu kwenye klabu hiyo hadi sasa. Alipandishwa kutoka kikosi cha Simba cha vijana na ndiye na kufanikiwa kubeba ndoo wakati huo akiingia kucheza kutokea benchi kama mchezaji chipukizi.

Said Ndemla, Ibrahim Ajib, Ramadhani Singano, Hassani Isihaka ni baadhi ya vijana waliopata kucheza Simba lakini hawakubahatika kubeba kombe la VPL hadi wengine wameondoka kwenye klabu hiyo wakiwaacha Mkude na Ndemla.

Msimu uliopita, Simba ilikaribia kuchukua ubingwa wa ligi kuu lakini malengo hayo yakazimwa na Yanga kwa kulichukua kombe hilo kwa mara ya tatu mfululizo kwa tofauti ya magoli baada ya timu zote kulingana pointi.

Msimu huu Simba inatajwa kuwa miongoni mwa timu zitakazotoa upinzani wa nguvu katika kuwania ubingwa wa VPL kutokana na usajili walioufanya, tayari kikosi cha kocha Joseph Omog kinaongoza ligi kikiwa na pointi 11 sawa na Mtibwa Sugar na Azam lakini wastani wa magoli ndio unazitofautisha timu hizo katika nafasi tatu za juu.

Ni nafasi nyingine kwa mkude kuweka rekodi ya kuwa mchezaji wa Simba aliyechukua ndoo mbili za VPL bila kuhama tangu alivyopandishwa kucheza kikosi cha wakubwa.

Emanuel Okwi

Alifunga magoli mawili wakati Simba ikiifunga Yanga 5-0, ni miongoni mwa wachezaji waliochangia kwa kiasi kikubwa Simba kutwaa ubingwa huo. Badae Okwi aliondoka na kuelekea vilabu vingine kama Etoile du Sahel, SC Villa, Yanga, SonderjyskE kwa nyakati tofauti lakini baada ya kuzunguka huko amekuwa akirejea Simba kama alivyofanya pia kabla ya msimu huu.

Shomari Kapombe

Ni miongoni mwa wachezaji waliokuwepo wakati Simba ikisherekea ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara mwaka 2012 lakini badae akafanikiwa kutoka nje ya nchi na kujiunga na Cannes ya Ufaransa ambako hakudumu kwa muda mrefu akarejea nchini kisha kwenda Azamkabla ya kurudi tena Simba.

Mwinyi Kazimoto

Alianza kuwika akiwa na JKT Ruvu Stars ya Pwani, ubora wake ukafanya asajiliwe na Simba, kutokana na ‘zari’ ile anaingia tu Simba msimu huohuo akanyakua ndoo ya VPL. Badae alijiunga na klabu ya Al-Markhiya ya Qatar na baadae mwaka 2015 akarejea nchini na kujiunga na Simba kwa mara nyingine tena.

Habari kwa hisani ya Shaffih Dauda
 
Usitukumbushe janga la 5-0, hebu tuzungumzie Ngoma, hivi kwa nini anakuwa majeruhi kila mara? Au hujuma?
 
Back
Top Bottom