Ambiele Kiviele
JF-Expert Member
- Dec 29, 2014
- 15,267
- 29,906
Haya madudu wanayofanyiwa baadhi ya wanaume na akina mama yapo kwa kila kabila, utafiti umebaini kuwa ni moja ya taaluma ya Kibantu katika kuongeza au kuthibiti chachu ya mapenzi na ambayo ikitumiwa vibaya inaweza kumfanya mwanaume kuwa chizi wa akili na pengine kupoteza maisha au kazi yake kabisa.
Ukiacha makabila yaliyozoeleka kwa mambo haya ya wanawake kutumia mbinu hizo za asili kuwavuta wanamume katika mapenzi(!) kama vile waTanga, Wahaya, Wanyakyusa, Wapemba, na makabila ya Pwani, inasemekana yapo makabila mengine, ambayo wanawake wanatumia teknolojia kali zaidi na yenye kutia kichefuchefu kama ukijua kuwavuruga wanaume.
Inadaiwa taaluma hiyo ya asili ambayo kwa sasa imeanza kupotea kutokana na wadada na akina mama wengi kuanza kumjua Mungu inaambatana na matumizi mabaya ya baadhi ya viumbe hai ambavyo huwezi kuvidhania vinaweza kulegeza ujanja na nguvu za mwanaume.
Inasadikika kuwa wataalamu wa kutengeneza madudu haya ni wanaume wenyewe (waganga wengi wa kienyeji ni wanaume).
Viumbe hivyo ni pamoja na yule mjusi mweupe na laini anaypenda kuishi katika nyumba zetu (mjusi kafiri) wa jamii hii:
Ukichaganyiwa kwenye menyu (chakula maalumu), hapo utakuwa huchungulii hata barazani, wewe unakuwa ni mtu wa chumbani taulo tu, kila kitu huko huko.
Hata kazini hutaki tena.
Pia kuna mijusi wale wanaokaa kwenye mawe au miamba ya mtoni au ziwani:
Ukifanyiwa hizo mambo na mjusi wa aina hizi, inadaiwa kuwa maisha yako ni mdura, ukitoka ndani waenda kazini au kanisani au msikitini, ukirejea tu ni ndani kwenye TV au chumbani na pengine kama ni mtu wa kinywaji wewe kinywaji chako ni cha kuagizia na kuwekewa kwenye jokofu (friji), mtaani na viwanja unaona nuksi na vitu sambamba na hivyo.
Kama una mengi kuhusu hii, toa maoni yako hapa chini.....