Je, virusi vinaweza kufundishwa?

Je, virusi vinaweza kufundishwa?

Sun is Sun

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2024
Posts
1,152
Reaction score
1,696
Nimekuwa nikitafakari swali ambalo huenda wengi tunaliona la kawaida au la kisanii lakini lina uzito wa kisayansi na kijamii: nawezekana kweli virusi kufundishwa? Swali hili limenitokea baada ya kuangalia ile filamu ya The Brothers Grimsby ambapo kuna njama ya kutumia virusi maalum kuua watu wa tabaka la chini pekee eti virusi hivyo vinatambua DNA za maskini.

Kwa mtu wa kawaida unaweza kusema ni kejeli au kichekesho tu cha filamu. Lakini je, kuna ukweli wowote wa kisayansi kuhusu hili?

1.Virusi haviwezi kuufundishwa kama binadamu.

Kwanza ni vizuri kuelewa kuwa virusi sio viumbe hai kamili havina seli, ubongo, wala mfumo wowote wa kujifunza. Havitendi kwa akili bali vinaingilia seli za viumbe hai na kuzipa maagizo ya kuzalisha virusi zaidi.

2.Lakini vinaweza kubadilishwa au kutengenezwa

Hapa ndipo mambo yanapoanza kuwa ya kutisha na ya kuvutia pia. Sayansi ya kisasa ya bioengineering na synthetic biology inaruhusu wanasayansi kufanya yafuatayo;

Kutengeneza virusi vipya maabara (synthetic viruses)

Kubadilisha virusi vya kawaida kuwa na madhara zaidi (gain of
function)

Kutengeneza virusi vinavyolenga seli fulani (kwa mfano za kansa)

Kutumia virusi kusafirisha dawa au chanjo ndani ya mwili (viral vectors)

Mifano halisi:

1. Tiba ya Kansa kwa kutumia virusi.
Wanasayansi wamebadilisha virusi vya herpes ili viue seli za saratani tu. Mfano halisi ni tiba iitwayo T-VEC inayotumika kupambana na melanoma (saratani ya ngozi).

2. Chanjo kama AstraZeneca COVID-19.
Inatumia virusi vya sokwe vilivyodhoofishwa kusafirisha maagizo ya kinga ya mwili dhidi ya corona.

3. Utafiti wa Gain of Function
Wanasayansi walibadilisha virusi vya mafua (H5N1) viweze kuambukizwa kwa hewa ili kuelewa hatari yake. Utafiti huu ulipingwa vikali kwa kuwa unaweza kutumika kama msingi wa kutengeneza silaha.

Je, Silaha za virusi zipo?

Jibu ni ndiyo, ingawa ni haramu kwa mujibu wa mkataba wa kimataifa wa Biological Weapons Convention (BWC), baadhi ya mataifa kama Marekani, Urusi na wengine wamewahi kufanya utafiti juu ya kutumia virusi kama silaha. Kuna ripoti kuwa virusi vya smallpox, anthrax na hata Ebola viliwahi kufanyiwa utafiti kwa madhumuni ya kijeshi.

Je, ni hatari au msaada?

Hapa ndipo mjadala unapoanza.

Bioengineering ya virusi inaweza kuokoa maisha kwa chanjo na tiba.

Lakini ikitumika vibaya inaweza kugeuka kuwa janga la kimataifa.

Mwisho,

Virusi haviwezi kufundishwa kama wanafunzi lakini vinaweza kufundishwa kisayansi yaani kubadilishwa tabia kupitia bioengineering.
Na jambo hili lina uwezo mkubwa aidha wa kuokoa maisha au kuharibu dunia nzima.

Asanteni kunipa mda wenu.
 
Ahsante kwa elimu...
 
Back
Top Bottom