Je ungali unazikumbuka Kashfa hizi!

Juaangavu

JF-Expert Member
Nov 3, 2009
935
132
Je ungali unazikumbuka scandal hizi ambazo zimetokea ndani ya taifa letu, tafadhali ongezea kadri unavyokumbuka:

RichMonduli - ilikuwa inakomba Shs 152ml kwa siku
Deepgreen
Meremeta
Kagoda
Majengo pacha ya BoT yaliingiza hasara ya Shs 221 billion;
Import Support
EPA
IPTL

Lakini hakuna anaye nyea ndoo pale Ukonga.

Lakini hivi sasa macho yetu, masikio na microphone za vyombo vya habari zimeelekezwa kwa Babu Loliondo.
Tanzania bwana ni nchi ya matukio kweli kweli. Any way tunasonga mbele kimkandamkanda
 
Yupo aliyepatikana na kosa ndiye ananyea ndoo Liyumba!Wengine wameshindwa kuwatia hatiani kwa kukosekana ushahidi wa moja kwa moja!DPP wetu hawajui jinsi yakuandaa mashita kwa kesi za uhujumu uchumi hivyo wanajinasua kirahisi kwa ushahidi huwa nimgumu kupatikana!
 
kweli linyumba liko segerea? Tanzania bwana kaz kwerkwer aliyeiba kuku ukonga miaka 15, alikwapua mabilioni segerea miaka 3. Viva Kiwete na ccm yako.?
 
Yupo aliyepatikana na kosa ndiye ananyea ndoo Liyumba!Wengine wameshindwa kuwatia hatiani kwa kukosekana ushahidi wa moja kwa moja!DPP wetu hawajui jinsi yakuandaa mashita kwa kesi za uhujumu uchumi hivyo wanajinasua kirahisi kwa ushahidi huwa nimgumu kupatikana!

Kweli kabisa KakaKiiza, hata huyu Lyumba kama si msaada wa kiuchunguzi kutoka nje asingepatikana na hatia. Na haya mapungufu ndiyo yanawapa kichwa MAFISADI. Jamani watanzania wazalendo mliopo kwenye fani za sheria na mambo ya uchunguzi, hebu zamieni kwenye hili tuiokoe nchi yetu.
 
Hivi sasa zimesahaulika kabisa, kumbukumbu ni ya babu Loliondo na nasikia hivi sasa yupo mwingine Tarakea!
 
Back
Top Bottom