Je, unazijua Sifa za mgombea wa Ubunge?

Mwakaboko King

JF-Expert Member
Apr 22, 2015
1,099
207
Kama kawaida nikiwa mdau wa masuala ya Siasa za Tanzania nimeona ni jambo la Afya kwa pamoja tukijikumbusha na kuziangalia sifa zinazozingatiwa wakati wa Uteuzi wa mgombea wa Kiti cha Ubunge katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wewe ambaye umejipanga kuingia katika kinyang'anyiro cha nafasi hii muhimu katika Uchaguzi ujao ni vyema ukaungana nami kupitia sifa zinazotakiwa. Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ibara ya 67 (1) mtu atastahili kuchaguliwa kuwa Mbunge iwapo anasifa zifuatazo;-
  1. Ni raia wa Tanzania
  2. Ana umri wa miaka 21 au zaidi
  3. Anajua kusoma na kuandika kwa Kiswahili na Kiingereza
  4. Ni mwanachama na ni mgombea aliyependekezwa na chama cha Siasa chenye usajili kamili
5. Hajatiwa hatiani na Mahakama yoyote kwa kosa la kukwepa kulipa kodi katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya uchaguzi.

**************************************************************************
Angalizo: Hata kama mtu ana sifa zote za kugombea hataruhusiwa kugombea Ubunge kama
  1. Ni raia wa nchi nyingine
  2. Kwa mujibu wa Sheria inayotumika katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imethibitishwa kwamba mtu huyo ana ugonjwa wa akili
  3. Amehukumiwa Kifo na Mahakama
  4. Anatumikia kifungo cha zaidi ya miezi sita
  5. Katika kipindi cha miaka 5 kabla ya tarehe ya Uchaguzi Mkuu amepata kuhukumiwa na kupewa adhabu ya kifungo kwa kosa linaloambatana na utovu wa uaminifu au kwa kuvunja Sheria ya maadili ya viongozi wa Umma.
Hayo ni mambo muhimu ya kuzingatia unapotaka kugombea nafasi ya Ubunge! Hoja iko mezani sasa naomba KUWASILISHA.
 
Sifa za kielimu Za wanaogombea East Africa wafuatlie kwelikweli siyo tu watu kuleta vyeti wawe wapya au wa bunge lillopita kuna Kolomijes wengi sana.Haya TISS kazi kwenu
 
Awe Mtanzania, elimu angalau darasa la saba, ajue walau kuandika, kusoma na kuhesabu. Unaweza kuangalia wasifu wa Kibajaji ama Msukuma ktk website ya Bunge.
 
Kuna kasumba ya wasanii wa bongo movie, bongo fleva, commedian na kadhalika kujihusisha na masuala mazima ya siasa. Kabla sijaendelea sana na mada hii naomba nitengeneze hoja ya msingi Kama ifuatavyo.

Kwa mujibu wa Katiba na sheria ya nchi yetu Kuna haki ya kila Raia wa Tanzania wa kuzaliwa kugombea nafasi yoyote ya kuwa kiongozi anayohitaji kama akiona na vigezo vyote kubwa kabisa Katiba yetu ni kama kujua kusoma na kuandika moja ya vigezo kuu mbili na nguzo ya sheria hii.

Sasa hoja kuna baadhi ya wasanii kama vile Harmonize, Shilole, Steve Nyerere nk wanaoneka kuonyesha nia ya kugombea katika majimbo yao sasa. Hivi kigezo cha kujua kusoma na kuandika pekee ndiyo kinacho dhingatiwa mtu kupewa ridhaa ya kuwa mwakilishi wa wananchi BUNGENI.

Hivi kama so kutuletea Bunge la wana-comedy, wakata mauno na watu wanaopenda kiki, badala ya kutetea wananchi wao walio wapa ridhaa ya kuongoza. Sasa hilo haliwezakani Watanzania lazime tubadilikae katika Karne hii ya 21 ambayo imetawaliwa na globalization, na technology lukuki. kuteua watu wenye angalau kama ni kigezo cha

1. Elimu, awe angalau ameishia kidato cha sita
2. Mchapakazi
3. Kujua na kutambua mamlaka aliopewa na uzalendo kwa nchi yake, sio kuja kuteua watu kwa kuangalia kigezo cha umaarufu na vituko wanavyo vifanya kwenda kutuwakilisha Watanzania.

Sasa tunahitaji maendeleo chanya(+), kwahiyo tunataka watu wenye Elimu. Shahada za uzamivu na uzamili na wanao jitetea kwamba kigezo ni kujua kusoma na kuandika tu lazima tuangalie sheria hii imetungwa lini na leo ni lini, au imetungwa karne ya ngapi na Sasa tuko karne ya ngapi, tuko wapi na tunataka kufikia azma gani.

Iyo msanii akae na atumie upendeleo wake ya kuwa msanii kutangaza na kufanya kuhamasisha watu wajitokeze kumuunga mkono. There is no haja kubwa ya kuwa na viongozi wasio na kuwajibika kwa wananchi wao. This tendency should be stopped this year 2020.

Asante sana.

by .........(ma-chemist)📝
 
Back
Top Bottom