Je unaziamini bahati nasibu za simu? mi siamini

Mabagala

JF-Expert Member
Nov 27, 2009
1,477
325
Unaamini ukituma sana sms zile wanazokata wastani wa shilingi mia tano au ile inayokaribia karibia utashinda? Hujaskia kesi kama vile mtu anachonga na wafanyakazi wa huko ili utangazwe mshindi? chukulia kwenye milioni moja ya ushindi wanamwambia mshindi wa kutengenezwa kuwa utachukua laki mbili au moja nyengine itabaki huku ili waliofanikisha ushinde nao wapate chochote? Mimi nimeshaona ivi, ndo maana nakata tamaa hata kushiriki izi nanihii zao, waweza cheza hadi umalize kila kitu na mwenzako akagusa sms moja tu na akaambiwa ndo mshindi!

Tanzania ntakupenda daima.
 
Sidhani.ile ni biashara tu,unajua kampuni za simu zinatengeneza pesa nyingi through bahati nasibu kuliko kuuza vocha,ndio maana unaona kampuni kama tigo iko cheap kimatumizi,hawategemei sana kuuza vocha wamejikita zaidi kwenye bahati nasibu kwani zinawalipa zaidi..
 
yeah zinawalipa wachezesha bahati nasibu kuliko hata wachezao
 
Kuna kitu hakipo sawa kwenye hzi bahati nasibu ndio maana kila "mshindi" anapopatikana anakalilishwa kusema kuwa hyo ni bahati nasibu ya ukweli
 
Milioni moja inauzwa laki 4 hadi 6, hakuna bahati nasibu hapo.
Changanya zako.
Milioni moja watakwambia zoezi limefanikishwa na watu wa nne wewe ni watano, so tutagawana laki mbili mbili, ukizingatia umetuma text moja tu ukatangazwa mshindi, basi unakuwa hujapoteza kitu.
 
ndo maana mtu akipigiwa simu ni mshindi anakuwa hana ile furaha ya ukweli maana anaelewa kiwango anachoenda kupokea pale ni kidogo
 
Mashndano yoyote yanayohusisha ushndi wa hela au zawadi yoyote yenye thamani, mara nyingi matokeo yanapangwa. Me nakumbuka shindano la kumtafuta balozi wa grand malt vyuoni. Chuo che2 walikuja 2kaanza kusaka kura hadi 2kaingia 2nd round ahaa kuna demu alikua hayupo serious kusaka kura akawa ana2ambia wingi wa kura sio ushndi. Siku ya siku anatangaza ye ndo wa kwanza akapewa laki 4, me nkaambulia kuwa wa 2 na ki laki changu ki 1. Ila hadi leo najua yule demu alipewa
 
ndo ivyo mkuu, lakini si kuna mamlaka isimamiayo michezo kama hii?
 
ndo ivyo mkuu, lakini si kuna mamlaka isimamiayo michezo kama hii?

mkuu upo Tz gani? Hyo mamlaka hata ofc zake utachoka, ma-officer wake wakiitwa kwenye hzo bahati nasibu wanapewa posho na wao wenyewe wanatangaza "mshindi"
 
Mimi kidogo nipo tofauti na wachangiaji waliopita.sikatai kama kuna ubabaishaji ila nimeshuhudia rafiki yangu wa karibu akishinda gari aina Hyndai i10 na alikabidhiwa bila mizengwe yoyote.Mpaka leo tunatesea kitaa na gari letu la bure.Na ile kampuni ya simu ambayo ni vodacom walitoa magari mia moja kwa washindi. Ubabaishaji unatokea kwa sababu kampuni nyingine za simu zinakuwa hazina usimamizi mzuri kwa mameneja masoko na maofisa uhusiano wao,hali inayopelekea wacheze dili na maofisa kutoka shirika la bahati nasibu.
 
Unategemea nini Tarimba ndo Mkurugenzi wa mambo ya bahati nasibu taifa je kunanini??
 
mkuu upo Tz gani? Hyo mamlaka hata ofc zake utachoka, ma-officer wake wakiitwa kwenye hzo bahati nasibu wanapewa posho na wao wenyewe wanatangaza "mshindi"
Kaka katika magari 100 yaliyotolewa unaweza ukakuta 10 tu ndo yametoka kihalali, na ndio rafiki yako akabahatika kwenye hayo kumi
 
Back
Top Bottom