Je, unataka kufanikiwa katika maisha yako?

Je, unataka kufanikiwa katika maisha yako?

Joined
Oct 10, 2014
Posts
6
Reaction score
4
Unataka kufanikiwa katika maisha yako? Unataka kuona unapiga hatua kuelekea kwenye mafanikio yako? Unataka kuona maisha yako yakibadilika na kushuhudia ongezeko katika maisha yako? Wewe ni mfanyakazi na unataka kujikwamua kimaisha kwa kujiongezea kipato kutoka ndani na nje ya kazi yako?

Au wewe ni mfanyabiashara kwa namna moja au nyingine mambo hayaendi vizuri katika bishara yako na unahamu na kiu ya kuona mabadiriko kwenye bishara yako, au wewe ni muhitimu wa chuo au ndiyo unakaribia kuhitimu chuo na unataka kuanza kujifunza ili uweze kujiandaa na changamoto za maisha kwenye eneo la fedha na maeneo mengine? Au wewe unataka mafanikio kwa ujumla tu katika maisha yako na hujui nini cha kufanya na mahari gani pa kuanzia?

Kama maswali hayo hapo juu ni moja kati ya maswali unayo jiuliza basi hapa umefika mahali sahihi pa kupata majibu ya maswali yako, mimi
paul masatu ni mjasiriamali(enterprenure), mkufunzi(mentor), mzungumzaji muhamasishaji(motivational speaker) na mwalimu wa elimu ya kujikwamua kimaisha(life coach), mwenye uzoefu wa takriban miaka kumi sasa.

Ninao ujuzi na mbinu za kisayansi zilizothibitishwa na mimi mwenyewe na watu wengi waliyofanikiwa, ambazo utakapozitumia zitakusaidia kuyabadilisha maisha yako na kuanza kushuhudia mafanikiao kwenye maeneo yote ya maisha yako ikiwemo na eneo la fedha(pato lako).

Ujuzi huu nimeupata kwa njia ya elimu niliyojifunza na kuitendea kazi katika maisha yangu kwa takribani miaka kumi sasa, elimu hii nimeipata kutoka katika vyanzo mbali mbali kama kusoma vitabu mbali mbali(karibu kila mwezi ndani ya miaka kumi sasa nimekuwa nikisoma vitabu viwili mpaka vitatu kila mwezi kuhusu siri za mafanikio) na pia nimekuwa nikinunua maarifa kwa njia ya mtandao(online materials) kutoka kwa wafanya biashara, waandishi na wazungumzaji wahamasishaji(motivational speaker) maarufu duniani wenye ujuzi wa kutosha uliyo thibitishwa utakao kufanikisha kwenye eneo la fedha na maeneo mengine katika maisha yako.

Nimehudhuria semina mbali mbali zilizonipa maarifa ya njia za asili kabisa za kumfanya mtu afanikiwe kifedha na maeneo mengine katika maisha yake, lakini pia nimekuwa na naendelea kuwa mkufunzi wa baadhi ya watu ambao kwa kunifuatilia mimi maisha yao yamebadirika na wanashuhudia uwezo wao wa kukabiliana na changamoto za maisha ukiongezeka, lakini pia ni muanzilishi na mmiliki wa makampuni na biashara mbali mbali ambazo zimepitia vipindi vyote vya kushindwa na kufanikiwa huku upande wa kufanikiwa ukiwa mkubwa zaidi, hivyo nina ujuzi wa kukusaidia kufanikiwa katika bishara yako.

Lakini mimi pia ni mmoja wapo wa team ya ''amka na badilika'' kipindi cha television kinachofundisha na kuhamasisha watu kutimiza ndoto zao.

Kwa maelezo hayo hapo juu utathibitisha kabisa ya kwamba nina ujuzi na uzoefu wa kutosha wa kukusaidia kuyabadilisha maisha yako kwenye eneo la fedha na maeneo mengine pia, nimekuwa nikifanya hivyo kupitia elimu ninayotoa kupitia mitandao ya kijamia kwenye face book page yangu ya
paul masatu, website yangu yawww.paulmasatu.com na nitafanya hivyo kwenye shule yangu (online course) itakayo anza soon kwa waliyo jiandikisha, nimefanya hivyo pia kupitia vipindi vya television, semina mbali mbali ninazo ziandaa mwenyewe na ninazo alikwa na watu wengine.


Sasa wapi tunaanzia? Mara nyingi ninapokuwa nazungumza na watu kuhusu mafanikio na watu wanapohamasika au watu wanaposoma makala zangu mbali mbali na wanapo hamasika na kutaka kuanza kuchukua hatua, moja kati ya maswali ninayo kutana nayo mara kwa mara ni
ninaanzaje?Ninaazia wapi?

Hili ni swali ambalo nimekuwa nikikumbana nalo mara kwa mara, na mimi leo naanza kwa kukuliza swali hilo, kama wewe unaswali au maswali kati ya yale niliyouliza pale juu sasa unaazaje au unaazia wapi kuelekea kwenye safari hii ya mafanikio? Swali hili nilikuwa nalo miaka kumi iliyopita na miaka mingine michache iliyo endelea, baada ya kuacha iliyokuwa ajira yangu na kuamua kushughurika na mambo yangu, ili kuelekea safari hii ya mafanikio, nilikuwa na swali hili kichwani mwangu, kwakweli wakati huo sikujua nianzie wapi, ilikuwa kama nimepelekwa kwenye jamii nyingine ambayo inazungumza lugha tofauti na lugha ninayo zungumza, sikujua nianzie wapi kwakweli, wakati huo majukumu hayakuwa yananisubiri, wajibu wangu wa kuhudumia maisha yangu na yafamilia yangu ulikuwa pale pale, presha ikawa kubwa, ugumu wa maisha, fedha haitoshi, ongezeko la gharama za maisha na changamoto nyingi za maisha zilikuwa wimbo wangu wa kila siku.

Kama walivyo watu wengine, kwa sababu ya kutokuwa na maarifa sahihi na kuto kujua wapi kwa kuanzia nilianza kutumia njia ya kupapasa, yaani najaribu hiki naakiacha, nashika hiki kinashindwa nakiacha, nasikia watu wakisema hiki namimi naamua kufuata mkumbo, natumia hela zangu nawekeza baada ya muda hamna kitu, jambo hilo linakufa, unasikia biashara hii inalipa unaamua kuingia, baada ya muda bishara haiendi mwisho mtaji unakufa, na staili nyingine za kuchukua hatua kama vile watu wanavyochukua hatua kutokana na kipi unasikia, kipi unaona, vyombo vya habari vinasemaje, umekuwa ndiyo utaratibu wa watu wengi, mwisho kabisa baada ya kuona nabahatisha na na hakuna mafanikio yoyote, kama walivyo watu wengine nikaamua kurudi shule, nikapata nafasi ya kusoma kwenye chuo cha usimamiz wa fedha(ifm) nikasoma stashahada ya juu ya usimamizi wa fedha(post graduate diploma in financial management) kwa kiwango fulani ilinisaidia,

Lakini ukweli ni kwamba elimu hizi za vyuoni(formal education) msaada wake huku mtaani ni mdogo sana, hasa unapoamua kuanzisha jambo lako mwenyewe, kwahiyo ile staili ya kujifunza kwa kupapasa ikaendelea, matokeo yake ikawa mambo yakawa yanaenda pole pole sana na nikatumia muda mrefu na gharama kubwa kuanza kufikia ndoto zang.

Katika muda huo mrefu na kwa gharama kubwa niliyoingia nikaanza kugundua baadhi ya siri za mafanikio, nikapata hasa chanel ya mambo gani ya kufanya na hatua gani za kupitia, nikapiga picha maisha yangu nyuma nikaona kila hatua nliyopiga ilitokana na kuzitumia hizi kanuni, lakini nilifanya kwa kupapasa sana baada ya kufanya mambo matano ambayo siyo nikajikuta nafanya moja ambalo ni sahihi, lile sahihi ndilo lililoniwezesha kupiga hatua moja au mbili mbele, ndiyo maana mambo yangu yakawa yanaenda polepole sana.

Mbeleni huko sasa, baada ya kupiga picha maisha yangu ya nyuma na kugundua/kuzifahamu zile hatua ambazo nilizichukua kwa kubahatisha bila mimi kufahamu, nikagundua kuwa kumbe ili niweze kupiga hatua mbele kunamambo ninayo takiwa kuyafanya, kunahatua ninatakiwa nizipige, nikiweka kwenye matendo hizo hatua naona mambo yanaongezeka, pato langu linakuwa, bishara yangu inakuwa, nikamua kuanza kujifunza zaidi, ni mambo gani hayo? Ni hatua zipi hizo? Ni kanuni zipi hizo?

Nikanza kujifunza huku nikizifanyia mazoezi, lakini pia nikaanza kuwafuatilia watu wengine waliyo fanikiwa, nikiwasikiliza, nikiwasoma, kwa sababu nilisha anza kuzifahamu hizi mbinu, nikagundua sababu kubwa zilizofanya wafanikiwe ndizo hizi hizi, yaani mambo hayo ndiyo msingi wa mafanikio yao, ndiyo msingi wa biashara zao kufanikiwa, ndiyo msingi wa maisha yao kifedha kufanikiwa.

Nikanza kupata hamu ya kuendelea kujifunza mbinu hizi, nikanza kununua vitabu mbali mbali, nikajiunga kwenye mitandao kuwafuatilia hawa watu, nikawa nayasoma mawazo yao kwa kusoma makala zao, vitabu vyao, lakini nikalipia baadhi ya masomo yandani kabisa kuhusu hizi mbinu masomo ambayo mara nyingi hawayatoi bure.

Lakini kwasababu ya hamu yangu(desire) yakutaka kufanikiwa ilikuwa kubwa, sikuona ugumu, kwa kadiri nilipopata uwezo wa kununua maarifa haya nilinunua, na kwa kweli naweza kukiri huo ulikuwa uwekezaji wangu mkubwa niliyo ufanya katika maisha yangu, na kila nilipo yafanyia kazi hayo maarifa, ndipo nilipoona ongezeko katika maisha yangu, fedha yangu ikawa inaongezeka kwa kasi ya ajabu, biashara zangu zikawa zinakuwa, mchango wangu kwa jamii ukawa unaongezeka, nikaanza kufahamika, uwezo wangu wa kupambana na changamoto ukaongezeka, nikawa mtu mpya kabisa.

Ni kama vile maisha nimeyashika mkononi, kwa sababu ninayaelekeza kwenye mwelekeo ninaoutaka mimi, uwezo wangu wa kutimiza malengo yangu ukaongezeka, nimefika wakati wa kuzishirikisha hizi siri kwa wenzangu, mimi naamini nimepita njia niliyopita si kwa bahati mbaya, ilikuwa inakusudi mimi kupita njia hiyo.

Labda wapo watu wanaohitaji kujikwamua kimaisha, yumkini wapo watu wengi wenye maswali kama yale niliyo uliza pale juu, lakini jambo zuri na la kutia moyo watu hawa hawahtaji kupita njia hii yakubahatisha niliyopita mimi, hawahitaji kupoteza muda wote niliyopoteza mimi ili kutimiza ndoto zao, hawahitaji kutumia gharama kubwa ya miaka yote kumi kuanza kushuhudia ndoto zao zikitimia, labda wanacho hitaji ni kuanza kunifuatilia mimi na watu wengine kama mimi wenye ujuzi na ufahamu wa mbinu za kufanikiwa, na kuanza kujifunza mbinu hizi, na kwa sababu mbinu hizi ni za asili, watakapo zitumia na kuziweka kwenye matendo wataanza kushuhudia mabadiliko kwenye maisha yao.

Na mimi niko tayari kuzifunua siri hizi kwao, ninacho hitaji kutoka kwao ni utayari wao wa kujifunza na kuyafanyia kazi yale yote watakayo jifunza.
 
Ukiwa kama motiveter speaker,
utanishauri nini kijana ambaye hata shule sikuenda lakn nataka mafanikio,,,!
nitafanye ili niweze kujikwamua.

kama wewe una mtoto ,
ni siri ngani utamwabia ili aje awe na mafanikio katika maisha yake
 
Ukiwa kama motiveter speaker,
utanishauri nini kijana ambaye hata shule sikuenda lakn nataka mafanikio,,,!
nitafanye ili niweze kujikwamua.

kama wewe una mtoto ,
ni siri ngani utamwabia ili aje awe na mafanikio katika maisha yake

Shy land, mimi kwa mtazamo wangu, sidhani kama mafanikio ya mtu yanahusisha shule, na nakubali kuwa na elimu ni mwanzo mzuri wa kuwa na mafanikio. Tuna mifano mingi ya watu hawakupata fursa ya shule kama ilivyo sasa na wamekuwa wanauwezo kifedha kuzidi yule profesa, au mtu mwenye phd za kutosha. Nadhani bwana paul anachosema hapo, ni mtu kujitambua ndani ya nafsi na kutumia fursa ulikuwa nayo ikuletee mabadiliko na kuzikabili changamoto zote.(Usiombe changamoto zisikupate, omba kuwa na hekima kukabili changamoto) Ukiwa muoga, na ukakubali kila mwaka uwe na changamoto hiyo hiyo hakika, utakuwa na hela ya kununua luku, maji, kodi, na ada ya shule. Ukisubiri pension. Ni mtazamo wangu tu.
 
Shy land, mimi kwa mtazamo wangu, sidhani kama mafanikio ya mtu yanahusisha shule, na nakubali kuwa na elimu ni mwanzo mzuri wa kuwa na mafanikio. Tuna mifano mingi ya watu hawakupata fursa ya shule kama ilivyo sasa na wamekuwa wanauwezo kifedha kuzidi yule profesa, au mtu mwenye phd za kutosha. Nadhani bwana paul anachosema hapo, ni mtu kujitambua ndani ya nafsi na kutumia fursa ulikuwa nayo ikuletee mabadiliko na kuzikabili changamoto zote.(Usiombe changamoto zisikupate, omba kuwa na hekima kukabili changamoto) Ukiwa muoga, na ukakubali kila mwaka uwe na changamoto hiyo hiyo hakika, utakuwa na hela ya kununua luku, maji, kodi, na ada ya shule. Ukisubiri pension. Ni mtazamo wangu tu.

Asante kwa jibu lako,

nini hasa binu na siri inayompelekea mtu kuwa na mafanikio.

ni kwa nini watu wengine wanafanikio ili hali wengine mafanikio hawayapati.
 
Asante kwa jibu lako,

nini hasa binu na siri inayompelekea mtu kuwa na mafanikio.

ni kwa nini watu wengine wanafanikio ili hali wengine mafanikio hawayapati.

Ninaamini, nikutambua kuwa wewe ndio mwenye jukumu la maisha yako na kubadilisha fikra zako, na kutoa maswali ya labda na au? Na kuanza kujiuliza kwa nn ? Swali la kwa nn? Ndo unapata jibu. Ukitaka fanya jambo, fanya likifeli fanya tena, kwa umakini zaidi. Mie sio mhamasishaji. Najibu kwa sababu nina amini kabisa. Kwenye mafanikio ya kutafuta na sio yale ya bahati. Mimi na biashara zangu, bado sijafika mafanikio ninayoyataka kibiashara na maisha pia., ila kwenye kupeleka proposal/bid watu nilikua nafanya nao kazi, kuna company walikuwa wanaziogopa. Mm moyoni kabisa huwa najiuliza, nisipo bid mimi? Nani atabid? Na kwa nn mtu mwengine afanye wakati uwezo tunao? hilo swali huwa linanisaidia sana.. Na jikuta napata clients zaidi. Tumsubiri bwana paul aje mwenywe.
 
inavutia...?


Inavutia sana mkuu, nimesoma leo subuhi nimeona naguswa kabisa. Nimeangalia tovuti yake. Ana makala nyingine pia. So powerful. Elimu ka hizi ndo za msingi. Kila mtu anawaza maisha bora. Wengine tunaona wanapata kila siku. Kwa nn isiwe sisi?
 
Inavutia sana mkuu, nimesoma leo subuhi nimeona naguswa kabisa. Nimeangalia tovuti yake. Ana makala nyingine pia. So powerful. Elimu ka hizi ndo za msingi. Kila mtu anawaza maisha bora. Wengine tunaona wanapata kila siku. Kwa nn isiwe sisi?

Jamas, kusema ukweli jamaa anajua siyo siri,
labba tumusubiri aje, maana ni maswali mengi yanamusubili hapa..
 
Uzi mzuri mkuu PAUL ila siku nnyingine uwe unawekan na paragraph /haya katika mada zako ili tupate mtririko mzuri wa mawazo yako. Ila umeeleza vema .
 
Back
Top Bottom