Je, unamfahamu ndege wala samaki wakubwa zaidi?

Je, unamfahamu ndege wala samaki wakubwa zaidi?

Thewildlife_tz

Senior Member
Joined
Apr 23, 2019
Posts
127
Reaction score
85
wanaitwa GREAT CORMORANT

Hawa ni ndege wanaopatikana sana bara la Amerca pamoja na Asia ila naamni bongo watakuwepo kitaalam wanaitwa "phalacrocorax carbo"
kwa hapa Tanzania wanaitwa NSOJU wako kanda ya ziwa

Kawaida ni wakubwa kiasi wenye mabawa madogo ya kuwawezesha kuruka wana mwili mweusi na rangi nyeupe shingoni,
wana uzito wa kg 5.5 - 5.8 na urefu wa cm 80 - 110 na mabawa yake huwa na urefu wa cm 160

Ni mojaa ya ndege wenye uwezo mkubwa sana wa speed akiwa majini anapiga mbizi kama umeme anauwezo wa kuogelea kwa speed ya 30km/h
hii ni kwasababu miguu yao iko webed inayomuwezesha kupiga maji

Pamoja na kuwa na uwezo wa kuruka na spidi ya 50km/h huwa hawaruki mara nyingi ila wataruka watakaponoa hatari au akiwa kwenye mishe za kumtafuta prey

Moja ya sifa kuu ya huyu ndege ni mfumo wake wa upokeaji chakula shingo zao hutanuka kutokana na size ya prey na wanakula wale samaki wakubwaaa na wanameza chap tu kama apepo

wanashingo fupi lakini inatanuka pia wana tumbo linaloadjust hivyo anaweza kula hata samaki watano wakubwa na asishibe ( daah kizazi cha fisi hiki)

Ni ndege wanaoishi kifamilia sana yaani ukoo mzima kuanzia wajomba, mababu , na hata ndugu wa hiari (extended family ) na hushirikiana sana ila sio kwenye chakula

Kuna baadhi ya nchi huwatumia sana kwa kuvuaa samaki wana technique sana za kuwinda lakini baadae wakaanza kuwindwa wao mpaka haki za wanyama zilipoanza kutumika

Muda wa mating huwa ni kwa msimu yaani dume na jike wanamate kwa uzao mmoja tu na baada ya hapo huachana na kutafuta partner mwingine (watoto wakiwa sita basi baba huwa tofauti)

Jike hutaga mayai matatu mpaka matano na huenguliwa baada ya siku 28-32
wakiwa porini wanaishi miaka 20 na wakifugwa hufika 24

VIDEO
hawa ndio great carmorant sasa hapo kaletewa samaki sasa ili kuwapiga wenzake faulo ndio anakula namna hiyo lakini baadae anakabwa ametoa jichoo (uroho mbaya sana)

Akiwa majini na akachagua prey basi humkimbiza na kuhakikisha anamkamata

 
Leta mavitu. Ila usisahau kunitag ukiweka uz mwingine
 
Hawa hata mwanza kule chato wapo wanakula sana sangara
 
Kuna ndege wakubwa zaidi kama Goliath Heron,Great white egert,Pelican,Black headed heron na African derter.
 
Back
Top Bottom