Je, unakopesha kwa riba? Erevuka, soma hapa

Bujibuji Simba Nyamaume

Platinum Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
79,007
Reaction score
168,594
NAONGEA NA WEWE, WEWE UNAYEKOPESHA PESA KWA RIBA.
Ni muhimu sana kwenu kulijua hili. Siku hizi kuna watu wengi wajanjajanja wamejianzishia tubiashara twa kukopesha hela kwa "riba". Au wengine hata siyo wafanyabiara ila tu anakuja mtu anaomba umkopeshe hela. Unamkubalia lakini kwa sharti la riba ya kiasi fulani. Au mkopaji mwenyewe anakushawisi kuwa ukimpa atarejesha kwa riba. Vyovyote itakavyokuwa suala la msingi ni kuwa katika makubaliano yenu mmeweka riba. Basi jambo hili ni kinyume cha sheria na halikubaliki.

Ikiwa uliyemkopa atakataa kukulipa hela yako basi utakuwa huna la kufanya. Hata ukienda mahakamani bado mahakama haiwezi kukusaidia. Haiwezi kuamuru ulipwe hiyo hela. Utakuwa umepoteza. Na si tu utapoteza hizo za riba bali pia hata hizo ulizomkopa (principal sum). Usimkopeshe mtu kwa riba kwani akiamua asikulipe huna la kumfanya kwa mujibu wa sheria.
Wengine hukimbilia Polisi kulalamika. Yumkini ni makosa. Na huyo askari anayeshughulikia kesi kama hii yupo katika makosa. Si kazi ya polisi kushughulikia masuala kama haya. Yafaa tuyajue haya ili tuwe makini.
Mahakama Kuu na hata Mahakama ya Rufaa zimeamua hivyo katika kesi nyingi . Mojawapo ni Shauri Namba 66/2007 kati ya ULF NILSON dhidi ya DR. TITO MZIRAY ANDREW . Katika shauri hili Jaji A.F.NGWALA alisema kwamba hata kama kuna makubaliano ya maandishi kuhusu malipo ya riba bado mtu binafsi ambaye hakusajiliwa wala hana leseni ya kufanya biashara ya fedha hawezi kutoza riba. Mwishoni alibatilisha makubaliano yote ya huo mkopo.

Kubatilishwa kwa makubaliano yote ya huo mkopo maana yake hata zile fedha ulizomkopa ambazo sio riba nazo zinakufa kwasababu mkataba mzima umebatilishwa, na mahakama imeuazimia (declare) kuwa haramu. Unaweza kuona utakuwa umepoteza kiasi gani. Na hali ni hii ni hata kwa kampuni ambazo hufanya biashara hizi bila leseni ya biashara ya fedha.
Yawezekana wakati unamkopa aliweka mali yoyote rehani. Iwe baiskeli, pikipiki,gari, nyumba, kiwanja au kinginecho madhali tu ni rehani. Hii nayo ni haramu na imekatazwa na sheria. Kifungu cha 6( 1 ) cha Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha kinasema kuwa mtu yeyote ambaye hafanyi biashara ya benki/fedha na hana leseni ya biashara hiyo haruhusiwi kupokea rehani kwa ajili ya mkopo kutoka kwa mtu yeyote. Kifungu kidogo cha ( 2 ) kimetangaza adhabu ya faini isiyozidi milioni 20, kifungo kisichozidi miaka mitano, au vyote kwa pamoja yaani kifungo pamoja faini. Kumbe basi utaona kuwa sio tu hairuhusiwi bali pia waweza kwenda jela. Kwa hiyo ni vyote kutoza riba pamoja na kuomba/ kupokea rehani ni makosa.

Kinachowachanganya watu wengi ni kwamba kuna maneno ya mtaani kuwa mkataba ni mkataba na makubaliano ni makubaliano ilimradi tu wahusika wote wameridhia na wameandikishana na kusaini kwa hiari zao. Mtu anategemea kumwambia mwenzake si ulisaini hapa. Ulisaini ukitegemea nini, na maneno mengine kama hayo. Ndugu, maneno hayo hayana msaada kwako, unapoteza tu mda. Kifungu cha 10 cha Sheria ya Mikataba kinasema kuwa makubaliano yote ni mikataba kama yamefanyika kwa hiari, na wahusika wenye sifa, kwa biashara halali, na makubaliano hayo yasiwe yamekatazwa na sheria nyingine yoyote. Utaona kifungu kinasisitiza kuwa hata kama makubaliano yatakuwa kama kifungu kilivyosema lakini bado makubaliano hayo yasiwe yamekatazwa na sheria nyingine yoyote.
Kwahiyo ni kweli kabisa kuwa makubaliano ni makubaliano isipokuwa yanakuwa makubaliano kamili na halali kama hayajatangazwa na sheria nyingine kuwa haramu. Na makubaliano ya riba na rehani kwa ambao sio taasisi ya fedha na wasio na leseni yametangazwa na sheria nyingine ambayo ni Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha kuwa haramu. Kwa msingi huu ile dhana ya makubaliano ni makubaliano tuliyoizoea mtaani inakufa na haipo tena . Hivyo usiifikirie tena katika mawazo na utetezi/kinga yako. Haitakusaidia!!

Sisi sote ni binadamu, na ubinadamu ni kusaidiana. Hivyo sheria haikatazi kusaidiana au kukopeshana hela kwa kuandikishana. Hela mnaweza kusidiana kwa kukopana. Lakini iwe tu kiubinadamu (socially) bila ya riba wala rehani (commercially). Msaada uwe msaada na isiwe katika mfumo wa faida, mapato au biashara. Na hapa mnaweza kuandikishana na Mahakama ikasaidia kupatikana haki ikiwa mkopaji amekaidi malipo, yaani aliyekopa anasumbua kurudisha hela kwa mtu alomkopesha. Kwahiyo ndugu jihadhari, jihadhari hasa wewe mtoa mkopo.

Mmalile, mimi nilikuwa nakukumbushapo tu!!
 
Wakopeshaji wanajua yote hayo, unakopeshwa laki 5, mkataba unaandikwa umekopa laki saba na nusu tu Bila riba! Hapo unakwepaje na umekiri kuchukua laki saba na nusu kiuhalisia una laki 5 tu, hutaki acha kapambane na shida zako!
 
Hiki ndicho mkopeshaji makini anapaswa kufanya, nimefanya sana hivi mtu anakuja anataka laki 4 unamwambia utarejesha laki 5 na ishirini baada ya mwezi means kwa kila laki moja ni faida ya elfu 30, anakubali, unamtolea mkataba kwamba amechukua laki 5 na ishirini na mashahidi wapo kabisa...hakuna mahala pameandikwa riba unadhani mahakamani changu sipati? Sababu hata akisema alinikopesha laki 4 tu ushahidi wa hivyo hamna
So mfanyabiashara yaaan individual money provider fanya biashara kiujanja vinginevyo swala la mkataba litakupotezea hela yako
 
Ziko mahakama za kimila. Unashushwa ngiri mdomoni. Kama nina hela ya kukukopesha nitakosa hamsini ya kumpa babu akuharibu na ukoo wako ?
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] weeeeeeee jamaa umenichekesha kweli
 
Ziko mahakama za kimila. Unashushwa ngiri mdomoni. Kama nina hela ya kukukopesha nitakosa hamsini ya kumpa babu akuharibu na ukoo wako ?
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji119][emoji119]
 
Ziko mahakama za kimila. Unashushwa ngiri mdomoni. Kama nina hela ya kukukopesha nitakosa hamsini ya kumpa babu akuharibu na ukoo wako ?

Bila shaka mkuu utakua unatokea kwamsisi au kilindi asilia
 
Siku hizi mathalan umkopa million moja wanaandika umekopa million moja na laki tatu ,hapa riba haitajwi kabisa kwenye mkataba
 
Kilichotokea Mlandizi mlikiona na kilichotokea Gongola mboto mlikiona LIVE. lete uhuni kwenye jasho la mtu uone. Sisi wakopeshaji wa vohela vidogo vidogo hatuendi mahakama kuu kwa majaji. Kwanza tuko out of place. Mtu kakopa elfu hamsini utampeleka mahakama kuu ? Hao nyuki wana kazi gani ?
 
NAONGEA NA WEWE, WEWE UNAYEKOPESHA PESA KWA RIBA.
Ni muhimu sana kwenu kulijua hili. Siku hizi kuna watu wengi wajanjajanja wamejianzishia tubiashara twa kukopesha hela kwa "riba". Au wengine hata siyo wafanyabiara ila tu anakuja mtu anaomba umkopeshe hela. Unamkubalia lakini kwa sharti la riba ya kiasi fulani. Au mkopaji mwenyewe anakushawisi kuwa ukimpa atarejesha kwa riba. Vyovyote itakavyokuwa suala la msingi ni kuwa katika makubaliano yenu mmeweka riba. Basi jambo hili ni kinyume cha sheria na halikubaliki.

Ikiwa uliyemkopa atakataa kukulipa hela yako basi utakuwa huna la kufanya. Hata ukienda mahakamani bado mahakama haiwezi kukusaidia. Haiwezi kuamuru ulipwe hiyo hela. Utakuwa umepoteza. Na si tu utapoteza hizo za riba bali pia hata hizo ulizomkopa (principal sum). Usimkopeshe mtu kwa riba kwani akiamua asikulipe huna la kumfanya kwa mujibu wa sheria.
Wengine hukimbilia Polisi kulalamika. Yumkini ni makosa. Na huyo askari anayeshughulikia kesi kama hii yupo katika makosa. Si kazi ya polisi kushughulikia masuala kama haya. Yafaa tuyajue haya ili tuwe makini.
Mahakama Kuu na hata Mahakama ya Rufaa zimeamua hivyo katika kesi nyingi . Mojawapo ni Shauri Namba 66/2007 kati ya ULF NILSON dhidi ya DR. TITO MZIRAY ANDREW . Katika shauri hili Jaji A.F.NGWALA alisema kwamba hata kama kuna makubaliano ya maandishi kuhusu malipo ya riba bado mtu binafsi ambaye hakusajiliwa wala hana leseni ya kufanya biashara ya fedha hawezi kutoza riba. Mwishoni alibatilisha makubaliano yote ya huo mkopo.

Kubatilishwa kwa makubaliano yote ya huo mkopo maana yake hata zile fedha ulizomkopa ambazo sio riba nazo zinakufa kwasababu mkataba mzima umebatilishwa, na mahakama imeuazimia (declare) kuwa haramu. Unaweza kuona utakuwa umepoteza kiasi gani. Na hali ni hii ni hata kwa kampuni ambazo hufanya biashara hizi bila leseni ya biashara ya fedha.
Yawezekana wakati unamkopa aliweka mali yoyote rehani. Iwe baiskeli, pikipiki,gari, nyumba, kiwanja au kinginecho madhali tu ni rehani. Hii nayo ni haramu na imekatazwa na sheria. Kifungu cha 6( 1 ) cha Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha kinasema kuwa mtu yeyote ambaye hafanyi biashara ya benki/fedha na hana leseni ya biashara hiyo haruhusiwi kupokea rehani kwa ajili ya mkopo kutoka kwa mtu yeyote. Kifungu kidogo cha ( 2 ) kimetangaza adhabu ya faini isiyozidi milioni 20, kifungo kisichozidi miaka mitano, au vyote kwa pamoja yaani kifungo pamoja faini. Kumbe basi utaona kuwa sio tu hairuhusiwi bali pia waweza kwenda jela. Kwa hiyo ni vyote kutoza riba pamoja na kuomba/ kupokea rehani ni makosa.

Kinachowachanganya watu wengi ni kwamba kuna maneno ya mtaani kuwa mkataba ni mkataba na makubaliano ni makubaliano ilimradi tu wahusika wote wameridhia na wameandikishana na kusaini kwa hiari zao. Mtu anategemea kumwambia mwenzake si ulisaini hapa. Ulisaini ukitegemea nini, na maneno mengine kama hayo. Ndugu, maneno hayo hayana msaada kwako, unapoteza tu mda. Kifungu cha 10 cha Sheria ya Mikataba kinasema kuwa makubaliano yote ni mikataba kama yamefanyika kwa hiari, na wahusika wenye sifa, kwa biashara halali, na makubaliano hayo yasiwe yamekatazwa na sheria nyingine yoyote. Utaona kifungu kinasisitiza kuwa hata kama makubaliano yatakuwa kama kifungu kilivyosema lakini bado makubaliano hayo yasiwe yamekatazwa na sheria nyingine yoyote.
Kwahiyo ni kweli kabisa kuwa makubaliano ni makubaliano isipokuwa yanakuwa makubaliano kamili na halali kama hayajatangazwa na sheria nyingine kuwa haramu. Na makubaliano ya riba na rehani kwa ambao sio taasisi ya fedha na wasio na leseni yametangazwa na sheria nyingine ambayo ni Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha kuwa haramu. Kwa msingi huu ile dhana ya makubaliano ni makubaliano tuliyoizoea mtaani inakufa na haipo tena . Hivyo usiifikirie tena katika mawazo na utetezi/kinga yako. Haitakusaidia!!

Sisi sote ni binadamu, na ubinadamu ni kusaidiana. Hivyo sheria haikatazi kusaidiana au kukopeshana hela kwa kuandikishana. Hela mnaweza kusidiana kwa kukopana. Lakini iwe tu kiubinadamu (socially) bila ya riba wala rehani (commercially). Msaada uwe msaada na isiwe katika mfumo wa faida, mapato au biashara. Na hapa mnaweza kuandikishana na Mahakama ikasaidia kupatikana haki ikiwa mkopaji amekaidi malipo, yaani aliyekopa anasumbua kurudisha hela kwa mtu alomkopesha. Kwahiyo ndugu jihadhari, jihadhari hasa wewe mtoa mkopo.

Mmalile, mimi nilikuwa nakukumbushapo tu!!
Asante sana kwa shule brother, sikuwa nikijua hivi vitu.
 
1. Niliwahi kushangaa kuona hukumu ya rufaa ya mahakama ya wilaya ya Magu - Mwanza kwa kesi ya namna hiyo kuandika kuwa " te evidence reveals that there was a contractual relationship"

2. Mimi nilishuzunika sana sikuwa na lakufanya huku nikiwaza kuwa hakimu kweli hajawahi wala hajui uwepo wa sheria ya benki na taasisi za kifedha hasa kifungu cha 6?

3. Ni kweli hajui na wala hajawahi kusomaa nini maana ya illegal contract? na doctrine of "Ex turpi causa non oritur actio"?
 
Ukikopesha kwa riba mf. 100000 izae 20000 . Maandishi : nimechukua 120000 nitarudisha mwisho wa mwezi, hapo riba imemezwa
 
NAONGEA NA WEWE, WEWE UNAYEKOPESHA PESA KWA RIBA.
Ni muhimu sana kwenu kulijua hili. Siku hizi kuna watu wengi wajanjajanja wamejianzishia tubiashara twa kukopesha hela kwa "riba". Au wengine hata siyo wafanyabiara ila tu anakuja mtu anaomba umkopeshe hela. Unamkubalia lakini kwa sharti la riba ya kiasi fulani. Au mkopaji mwenyewe anakushawisi kuwa ukimpa atarejesha kwa riba. Vyovyote itakavyokuwa suala la msingi ni kuwa katika makubaliano yenu mmeweka riba. Basi jambo hili ni kinyume cha sheria na halikubaliki.

Ikiwa uliyemkopa atakataa kukulipa hela yako basi utakuwa huna la kufanya. Hata ukienda mahakamani bado mahakama haiwezi kukusaidia. Haiwezi kuamuru ulipwe hiyo hela. Utakuwa umepoteza. Na si tu utapoteza hizo za riba bali pia hata hizo ulizomkopa (principal sum). Usimkopeshe mtu kwa riba kwani akiamua asikulipe huna la kumfanya kwa mujibu wa sheria.
Wengine hukimbilia Polisi kulalamika. Yumkini ni makosa. Na huyo askari anayeshughulikia kesi kama hii yupo katika makosa. Si kazi ya polisi kushughulikia masuala kama haya. Yafaa tuyajue haya ili tuwe makini.
Mahakama Kuu na hata Mahakama ya Rufaa zimeamua hivyo katika kesi nyingi . Mojawapo ni Shauri Namba 66/2007 kati ya ULF NILSON dhidi ya DR. TITO MZIRAY ANDREW . Katika shauri hili Jaji A.F.NGWALA alisema kwamba hata kama kuna makubaliano ya maandishi kuhusu malipo ya riba bado mtu binafsi ambaye hakusajiliwa wala hana leseni ya kufanya biashara ya fedha hawezi kutoza riba. Mwishoni alibatilisha makubaliano yote ya huo mkopo.

Kubatilishwa kwa makubaliano yote ya huo mkopo maana yake hata zile fedha ulizomkopa ambazo sio riba nazo zinakufa kwasababu mkataba mzima umebatilishwa, na mahakama imeuazimia (declare) kuwa haramu. Unaweza kuona utakuwa umepoteza kiasi gani. Na hali ni hii ni hata kwa kampuni ambazo hufanya biashara hizi bila leseni ya biashara ya fedha.
Yawezekana wakati unamkopa aliweka mali yoyote rehani. Iwe baiskeli, pikipiki,gari, nyumba, kiwanja au kinginecho madhali tu ni rehani. Hii nayo ni haramu na imekatazwa na sheria. Kifungu cha 6( 1 ) cha Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha kinasema kuwa mtu yeyote ambaye hafanyi biashara ya benki/fedha na hana leseni ya biashara hiyo haruhusiwi kupokea rehani kwa ajili ya mkopo kutoka kwa mtu yeyote. Kifungu kidogo cha ( 2 ) kimetangaza adhabu ya faini isiyozidi milioni 20, kifungo kisichozidi miaka mitano, au vyote kwa pamoja yaani kifungo pamoja faini. Kumbe basi utaona kuwa sio tu hairuhusiwi bali pia waweza kwenda jela. Kwa hiyo ni vyote kutoza riba pamoja na kuomba/ kupokea rehani ni makosa.

Kinachowachanganya watu wengi ni kwamba kuna maneno ya mtaani kuwa mkataba ni mkataba na makubaliano ni makubaliano ilimradi tu wahusika wote wameridhia na wameandikishana na kusaini kwa hiari zao. Mtu anategemea kumwambia mwenzake si ulisaini hapa. Ulisaini ukitegemea nini, na maneno mengine kama hayo. Ndugu, maneno hayo hayana msaada kwako, unapoteza tu mda. Kifungu cha 10 cha Sheria ya Mikataba kinasema kuwa makubaliano yote ni mikataba kama yamefanyika kwa hiari, na wahusika wenye sifa, kwa biashara halali, na makubaliano hayo yasiwe yamekatazwa na sheria nyingine yoyote. Utaona kifungu kinasisitiza kuwa hata kama makubaliano yatakuwa kama kifungu kilivyosema lakini bado makubaliano hayo yasiwe yamekatazwa na sheria nyingine yoyote.
Kwahiyo ni kweli kabisa kuwa makubaliano ni makubaliano isipokuwa yanakuwa makubaliano kamili na halali kama hayajatangazwa na sheria nyingine kuwa haramu. Na makubaliano ya riba na rehani kwa ambao sio taasisi ya fedha na wasio na leseni yametangazwa na sheria nyingine ambayo ni Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha kuwa haramu. Kwa msingi huu ile dhana ya makubaliano ni makubaliano tuliyoizoea mtaani inakufa na haipo tena . Hivyo usiifikirie tena katika mawazo na utetezi/kinga yako. Haitakusaidia!!

Sisi sote ni binadamu, na ubinadamu ni kusaidiana. Hivyo sheria haikatazi kusaidiana au kukopeshana hela kwa kuandikishana. Hela mnaweza kusidiana kwa kukopana. Lakini iwe tu kiubinadamu (socially) bila ya riba wala rehani (commercially). Msaada uwe msaada na isiwe katika mfumo wa faida, mapato au biashara. Na hapa mnaweza kuandikishana na Mahakama ikasaidia kupatikana haki ikiwa mkopaji amekaidi malipo, yaani aliyekopa anasumbua kurudisha hela kwa mtu alomkopesha. Kwahiyo ndugu jihadhari, jihadhari hasa wewe mtoa mkopo.

Mmalile, mimi nilikuwa nakukumbushapo tu!!
Ngimba kalumbu ulimnkafu
 
Back
Top Bottom