Je unaijua nguvu ya maji ya bendera?

Je unaijua nguvu ya maji ya bendera?

mkuchun

Member
Joined
Apr 21, 2013
Posts
9
Reaction score
6
Je ungependa kuwa na ujasiri wa kuongea mbele za watu? Je ungependa nyota yako ing'are katika ulingo wa siasa? Je unapenda kupata kibali na kukubalika mbele za watu kama alivyokuwa baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere? Jibu ni rahisi tu " kunywa maji ya bendera" !!!


kwa wale msiojua, ni vyema mkifahamu kwamba nguvu ya maji ya bendera ni kubwa mno. Ina uwezo wa kumbadilisha mtu na kumfanya kiumbe mwingine kabisa tofauti na alivyokuwa mwanzo. Nguvu ya maji hayo huathiri uwezo wa mtu kiakili, kihisia, kiutu na ki-mwonekano kwa ujumla.


Baada ya kujua hayo je ungetamani kunywa maji ya bendera? Je uliwahi kumfahamu mtu aliyekunywa maji hayo na je waweza tofautisha mwonekano wake kabla na baada ya kunywa maji ya bendera? Kama moja wapo ya jibu kwa maswali hayo hapo juu ni hapana basi endelea kusoma hapa chini:


Faida za kunywa maji ya bendera: 1). Ujasiri wa kusimama na uwezo wa kuongea mbele za watu(KUROPOKA). 2). kupata kibali na kukubalika kwa watu-hasa WAJINGA. 3). Uwezo wa kuropoka maneno mengi bila woga. 4). Dharau kwa watu wanaokuzunguuka na kuwaona si kitu. 5). Kujiotoa ufahamu wako wa hapo awali. 6). Kuwa na utiifu mkubwa(msukule) kwa wanaokupa maji hayo. 7). Kutokukubali ukweli pale ukweli huo unapokinzana na matakwa ya wenye maji.


Kuna vielelezo vingi vya kudhihirisha hayo niliyoyataja hapo juu: Mfano no.3). Uwezo wa kuropoka maneno mazito yenye dhihaka kwa watu. n a no.4). Dharau kwa watu wanaokuzunguuka na kuwaona si kitu.(rejea kauli hizi)


-.......10 mil. ni hela ya kununulia mboga!!!by prof.Tiba -.......Watanzania hata wakila nyasi-ndege lazima inunuliwe..by Mh.Mramba -.......hivyo ni Vijisenti tu,.,.,.by joka lenye makengeza -.......tutashinda tu hata kwa bao la mkono...,.by Nape -.......waliotoka ,.,.hao ni makapi,.,by Kinana -.......huyu kwangu ni sawa na tumbili tu...by katibu mkuu wa wizara -.......hao ni ‘oil chafu'..,..by kada muhimu katika chama


5). Kujiotoa ufahamu wako na kukabidhiwa ufahamu wa wanaokupa maji ya bendera. Mfano: -... ....kuwanunulia laptop walimu wa shule za msingi.,.,.by presidential candidate material, mh. Dr. JPM -.......hizi pesa za escrow sio pesa za umma...by prof. makapi


Mifano mingine no. 7). Kutokukubali ukweli pale ukweli huo unapokinzana na matakwa ya wenye maji ya bendera.
-......kitendo (prof. Humphrey Polepole) cha kukaa kimya na kutokutolea ufafanuzi pale wananchi wanapohoji ni kwa nini wasiwanyime kura mgombea uraisi na m/kiti wa lililokuwa bunge maalum la katiba...kwa vile walichakachua katiba ya wananchi...

Haya ni machache tu! Ila kama wewe ni kijana bado na ungependa kujua zaidi juu ya nguvu za maji ya bendera na huenda ungependa na wewe uinuke kwenye ulingo wa kisiasa za Tanza-nia basi huna budi kufwatilia kwa ukaribu mienendo na kauli za vijana wafwatao: Nape Mnauye(Mbunge mtarajiwa) ,Mh. Ritz K.(Mbunge), Mh. Makonda na Mh. L. Lusinde(Mb), Mh. J. Makamba(Mb), Mh.Mwigulu Nchemba(Mb) Mh. Nyarandu(Mb) na wengine.


 
Ongeeni yote yawaishe ila tutakapoanza msiseme goli la mkono make tutawapeleka mkakae seat za nyuma ..utumieni vizuri mda huu
 
Back
Top Bottom