Je, Unaijua ibara 37 (1) Kwenye katiba kuhusu rais?

Emc2

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
16,808
16,886
Basi nakusihi soma hapa sasa ili kidogo upate mwanga.
17426284_274429579657533_4844502684777350272_n.jpg
 
Hicho kipengere kwa kiswahili tungeweza kusema kuwa, zaidi ya kulazimika kufuata matakwa ya katiba na sheria za nchi, Rais hatalazimiki kuchukua ushauri wa mtu yeyote.

Cha kwanza kwenye kipengere hicho inaonekana wazi kuwa Rais analazimika kufuata katiba na sheria za nchi.

Sasa tujiulize, katiba na sheria anazolazimika kuzifuata, zinasemaje juu ya kuwatumikia watu wote bila ya upendeleo au ubaguzi? Rais kwa kuwatumbua watu wengine kwa sababu tu wamelewa kazini na kuamua kumlinda kiongozi ambaye mevamia taasisi kwa vitisho kwa malengo yake binafsi, lakini kwa kutumia cheo chake, siyo ubaguzi katika kuwatumikia wananchi wote kwa haki na kwa usawa, kama alivyoapa?

Sheria pia inasemaje, Rais akiamua kuwalinda wahalifu? Wanasheria wanaweza kutusaidia zaidi.
 
Some pia idara ya 47 na 107 utashangaaa kwanini hi Katiba haifai
Ndiyo maana mimi sioni kama kuna upinzani wa maana hapa Tanzania. Watu waliingia kwenye uchaguzi mwaka 1995 bila kutumia akili zao. Sasa si wakati wa kumlaumu rais maana rais anachokifanya siyo kosa maana katiba inamruhusu. Ndiyo maana siwaelewi watu kama kina Sumaye kutuhubiria demokrasi wakati wameikanyaga miaka yote kwa katiba yao ya CCM. Hawa UKAWA walio wengi ni makapi ya makada ya CCM na watakuja wengi sana upinzani. Lengo lao ni moja maana visasi ndiyo dini ya CCM na wakiingia hata kina Sumaye hawataibadilisha maana katiba ni kulipizana visasi.

Hapa JF tunapiga kelele kama kweli tunaifahamu hii katiba na tunadanganywa na wanasiasa wa upinzani ambao wengi wao sina hakika kama wanaijua hii katiba pia. Na wanaoijua kama kina Lissu nao ni wapiga deal tu. Hatari sana
 
akifanya hivyo IBARA YA 46 Inapaswa kutumika
 
mkuu...acha kulalamika..toa suluhisho
 
mkuu...acha kulalamika..toa suluhisho
Mimi sijalalamika mkuu bali naeleza ukweli. Watu tunapoteza muda kushabikia upuuzi wa wanasiasa. Jiulize mwenyewe ukiangalia makombora tuliyokuwa tunampiga Lowasa kwa miaka zaidi ya sita. Tumia akili hapa bila kuwa nabii kujua nini Magufulia angefanya, kati ya hawa wawili Magufuli na Lowasa ungemchagua nani??? Tatizo naulaumu upinzani kwakuwa hawapo serious wanacheza na maisha ya watanzania kwa kuwapa kiburi CCM. Walijiandaa vyema miaka zaidi ya saba, wamekuja kupotoka miezi 4 kabla ya uchaguzi kutuletea wale wenye madoa kutoka huko CCM, halafu wanasingiza wameibiwa kura nani kaiba kura?? Wanadhani watanzania ni wajinga wangemchagua mtu walimuita fisadi?? Si waliwapa CCM nyundo kuwamaliza??? Kwa kusema hivyo siyo kama napenda haya ynayotokea hapa Tanzania. Uliona wapi rais wa nchi anapewa mamlaka kikatiba kumweka ndani mtu kwa masaa 48?? ama mkuu wa mkoa?? Hawa kina Lissu wapo wapi na wao ni wanasheria kwanini hawakuliona hili? wapo busy kukimbilia Ikulu bila kurekebisha njia ya kwenda Ikulu kirahisi.
 
Hujaelewa lolote kwenye hiyo ibara. Tafadhali,ukiwa ni mbumbumbu wa sheria,usiwe unazungumzia sheria. Ni heri ukauliza. Bure kabisa!
wewe ni mwansheria baada ya kutusaidia kutuelewesha sisi ma lay unakuja na matusi ya nguoni. Ninyi ndiyo mliotufikisha hapa tulipo. Wanasheria wa Tanzania mimi nawalinganisheni na waandishi wa habari wa Tanzania hamna lolote. Walimu wenu si hao kina Prof Kabudi na Mwakyembe wamewafundisha kuwa wanafiki tu. Waganga njaa tu na kesi zenu za kuwahonga majaji. Judicial System yote ina virusi.
 
Well, the Article 37 (1) as quoted does not mean he can't comply with those provisions contained on the Constitution. In terms of dealing with 'Criminal Laws'. In this case, it is clearly until now Mr. President unjustified keep protecting RC Daudi Bashite by misusing his power to defend Makonda's crimes. The same crimes which Makonda had committed other people have been punished for it. If Mr. President keeps advocating these rules and called for punishment on others, why Daudi Bashite should be untouchable?? He keep ignore us while we are the one's put him in the office. This issue is of the public interest!
 
Hujaelewa lolote kwenye hiyo ibara. Tafadhali,ukiwa ni mbumbumbu wa sheria,usiwe unazungumzia sheria. Ni heri ukauliza. Bure kabisa!

Naomba utupe ufafanuzi katika hili la 'umbumbumbu' maana hhumu kila mtu na taaluma yake.

hapo pamekaaje kutoka kwa mtoa mada, fafanua?

usitoe povu unipe maelezo yamekaaje mheshimiwa
 
Ndugu yangu
Hicho kipengere kwa kiswahili tungeweza kusema kuwa, zaidi ya kulazimika kufuata matakwa ya katiba na sheria za nchi, Rais hatalazimiki kuchukua ushauri wa mtu yeyote.

Cha kwanza kwenye kipengere hicho inaonekana wazi kuwa Rais analazimika kufuata katiba na sheria za nchi.

Sasa tujiulize, katiba na sheria anazolazimika kuzifuata, zinasemaje juu ya kuwatumikia watu wote bila ya upendeleo au ubaguzi? Rais kwa kuwatumbua watu wengine kwa sababu tu wamelewa kazini na kuamua kumlinda kiongozi ambaye mevamia taasisi kwa vitisho kwa malengo yake binafsi, lakini kwa kutumia cheo chake, siyo ubaguzi katika kuwatumikia wananchi wote kwa haki na kwa usawa, kama alivyoapa?

Sheria pia inasemaje, Rais akiamua kuwalinda wahalifu? Wanasheria wanaweza kutusaidia zaidi.
wanasheria gani unataka waje kutusaidia? Tanzania tuna makarani wa sheria tu wanatia hata aibu fani za watu. Angalia idadi ya wanaotaka kuwa mawakili njaa kali wanataka cha juu. Kina Ulimwengu miaka yote wapo kimya na katiba chafu hii tuliyonayo mwenzao alipofanyiwa ubaya na katiba ya ukandamizaji wanajifanya kujazana kisutu kama kuna msiba. Wanatia aibu sana. Angalia Kagame na wenzake walipopata mshikemshike na wanasheria wa Ufaransa, hapa kwetu hakuna hata mmoja anayehoji mapungufu ya katiba, halafu wanakuja hapa JF kutunanga ati hatujui sheria.
 
Well, the Article 37 (1) as quoted does not mean he can't comply with those provisions contained on the Constitution. In terms of dealing with 'Criminal Laws'. In this case, it is clearly until now Mr. President unjustified keep protecting RC Daudi Bashite by misusing his power to defend Makonda's crimes. The same crimes which Makonda had committed other people have been punished for it. If Mr. President keeps advocating these rules and called for punishment on others, why Daudi Bashite should be untouchable?? He keep ignore us while we are the one's put him in the office. This issue is of the public interest!
It looks like you are contradicting yourself Sir!!!!
 
Katiba tuliyonayo ambayo inaatwa katiba ya mwaka 1977 ni katiba ambayo sio HALALI [LEGITEMATE] kwasababu wakati huo inapitishwa population ya nchi yetu ilikuwa ndogo ukifananisha na leo na ndio maana wananchi wa leo wanataka KATIBA ambayo itakidhi maendeleo yao!! Hii katiba ya mwaka1977 ni halail kisheria lakini sio legitemate kuwa inakubalika na wengi!!!
 
Back
Top Bottom