Je, unahisi tatizo la Simba ni Nini?

Je, unahisi tatizo la Simba ni Nini?

Ngungu anaonewa .....sio yeye anatoa budget ya timu
sasa kwa nini anakimbia kikao, badala ya kuwaelimisha washabiki ambao yeye ndiye mwenyekiti wao ili wajue ukweli?
 
Kwanza tuulizane hivi Selemani Matola ni kocha msaidizi wa kudumu pale Simba? Hivi hawezi kuwa kocha mkuu wa simba au timu yoyote ile ya ligi kuu, au daraja la kwanza?

Maana inashangaza kumuona kwenye nafasi ile ile hata baada ya kupita zaidi ya makocha 8-10 kwenye hiyo timu kwa nyakati tofauti!!

Hivi hili jambo limekaaje kwa nyinyu mashabiki wa hiyo timu!! Au mtaniambia ninamuonea wivu, badala ya kujibu hoja zangu?
 
Mapito tu hali hii anapitia Manchester United moja ya klabu kubwa pale Uingereza.

Lakini hata Real Madrid moja ya klabu kubwa Duniani mwaka Jana ilipitia magumu kidogo,hata sasa haijaa kaa sawa.

Pia Nyakati hizi Yanga iliwahi pitia,na baadhi yaashabiki wenye mioyo miepesi walihama timu so Simba ni timu kubwa na itafanya vizuri.

Asitafutwe mchawi badala yake iandaliwe mipango mikakati kuisuka upya naamini kila kitakaa sawa
Haya ya Simba sio mapito ni Maputo
 
Ahmed Ali ni miongoni mwa tatizo kwenye mambo serious analeta utoto
 
Yeye si ni msemaji tu mkuu, anachombeza tu😁
Idara ya habari ni moja ya department mhimu kwenye taasisi ikianza kutoa taarifa za uongo lazima taasisi ipate changamoto
 
Kwanza tuulizane hivi Selemani Matola ni kocha msaidizi wa kudumu pale Simba? Hivi hawezi kuwa kocha mkuu wa simba au timu yoyote ile ya ligi kuu, au daraja la kwanza?

Maana inashangaza kumuona kwenye nafasi ile ile hata baada ya kupita zaidi ya makocha 8-10 kwenye hiyo timu kwa nyakati tofauti!!

Hivi hili jambo limekaaje kwa nyinyu mashabiki wa hiyo timu!! Au mtaniambia ninamuonea wivu, badala ya kujibu hoja zangu?
Au ni mganga wa timu
 
Uongozi wa simba umekubali kuwa driven na presha na papara ya mashabiki ili kushindana na Yanga..

Kwa maana nyingine Tatizo la Simba ni kuimarika kwa Yanga......
Simba wana-force kujiringanisha na Yanga ili kuwaridhisha mashabiki wake kwa njia za mkato..

Viongozi wamejikuta wanafanya maamuzi bila utulivu, fukuza huyu lete yule, ondoa hawa, ingiza wapya.....nk
Wamejikuta wanaanza upya kila msimu....ili ku-cope na mizaha, vicheko, tambo za watani wao dhidi ya mashabiki wao....
Kiuhalisia, Simba inafanya vizuri...
Simba hii imetoka kucheza fainali kombe la shirikisho.... ....Simba ilikuwa haijafikia hatua hii tangu miaka 23 iliyopita? Leo utasema Simba ni mbovu?
Hayo yalikuwa ni mafanikio, lakini inawezekana wasiyanekane simply kwasab Wamefungwa na yanga kila mara nyingine...
Viongozi wa Simba wanatakiwa watengeneze timu kwa utulivu, bila kubabaishwa na kelele za mashabiki wachache wanaolalama mitandaoni..
Hawa ni wachache sana achaneni nao...hawafiki hata mia.
 
Back
Top Bottom