Je, una mke/mume? Changamoto gani uliwahi kukutana nayo katika ndoa yako?

wa4

Senior Member
Jul 2, 2016
158
65
Hapana shaka wakuu swali hili litajibiwa na wanandoa haswa.

Lengo la swali hili ni kupeana uzoefu wa changamoto zinazotukabiri katika ndoa zetu. Swali la msingi ni changamoto gani uliwahi kukutana nayo katika ndoa yako ambayo ilikuumiza sana na ulifanyaje?
 
Hapana shaka wakuu swali hili litajibiwa na wanandoa haswa me, lengo la swali hili ni kupeana uzoefu wa changamoto zinazotukabiri ktk ndoa zetu. Swali la msingi ni ( changamoto gani uliwahi kukutana nayo ktk ndoa yako ambayo ilikuumiza sana na ulifanyaje
Welcome to JF
 
Hapana shaka wakuu swali hili litajibiwa na wanandoa haswa me, lengo la swali hili ni kupeana uzoefu wa changamoto zinazotukabiri ktk ndoa zetu. Swali la msingi ni ( changamoto gani uliwahi kukutana nayo ktk ndoa yako ambayo ilikuumiza sana na ulifanyaje
Daah!! Nashindwa hata nianzie wapi maana ni mlolongo wa matukio mengi hadi kupelekea kufikishwa polisi
 
Kipato kinapo shuka mwanamke anaanza kisirani anaweza akamwambia mtt mwambie baba akupe hela ukanunue chips wakati anajua huna hela kabisa inawezekana hata ya nauli alikupa yy asubuhi hii yote ni chenga moto ya kukudhalilisha kwa watoto ila mm nimeikomesha
Mkuu tupe uzoefu ulifanyaje
 
Hii yangu nahisi wengi huwa inawakuta ,Ila ngoja nichangie na wadau tupate faida kwa wote.

Kuna lipindi mdogo wangu wa kike alikuwa anaumwa halafu kwa bahati mbaya aliachwa na mume wake.Akaniomba aje kwangu ajiuguze ukiangalia mimi ndio kaka yao mkubwa . Nikamwambia wife kuwa wifi atakuja hapa kujiuguza kwa muda so jiandae kumpokea .

Alinivunja moyo sio siri alidai kuwa yule alishaolewa na anasheria zake za familia yake so akija hapa tutaanza kukinzana kwani hatoweza kuishi kwa kunifuata mimi. Nikicheki sehemu ya kulala ipo kwa sababu wadogo zake huwa wanakuja na wanakaa zaidi ya mwezi lakini sijawahi kujisikia vibaya. Ila kwa hili roho iliniuma sana kwa sababu dogo nilishamwambia aje halafu mke wangu hataki.

Mwisho akaniambia nichague moja kama atakuja mdogo wangu yeye arudi kwao .Nikazidi kuvurugwa ikanibidi nimshirikishe mama yake mama yake nikaona anaegemea upande wa binti yake.

Nikaenda kwa mdogo wangu nikamwambi kule kwangu hakuna mtu wa kukuangalia kwa ukaribu zaidi so nitakutafutia house girl akutunze hapa nyumbani(Alikuwa amerudi kwenye nyumba ya marehemu baba).

Ila nikakaa na mke wangu nikamwambia kuanzia leo wewe na mimi tutaishi wawili tu hapa sihitaji kuona ndugu yako wala ndugu yangu ili kusiwe na upendeleo na ikitokea akaja ndugu yako nitamdhalilisha mbele yako.

Na yeye akaenda kushitaki kwa mama yake. Nikaitwa na nikatoa maelezo nikamwambia mama sisi wote tunafamilia nyuma yetu ndugu yangu ameshindwa kuja kuugulia nyumbani kwa sababu nyepesi sana leo hii mimi nitajisikiaje akija ndugu yake yeye wakati mimi ndiye mtoa huduma, wakaniomba radhi . Na mdogo wangu alikuja pale kwangu akaugua mpaka akapona na maisha yanaendelea vizuri.

Maisha ya ndoa yana changamoto nyingi sana..
 
Hii yangu nahisi wengi huwa inawakuta ,Ila ngoja nichangie na wadau tupate faida kwa wote,
Kuna lipindi mdogo wangu wa kike alikuwa anaumwa halafu kwa bahati mbaya aliachwa na mume wake.Akaniomba aje kwangu ajiuguze ukiangalia mimi ndio kaka yao mkubwa . Nikamwambia wife kuwa wifi atakuja hapa kujiuguza kwa muda so jiandae kumpokea .Alinivunja moyo sio siri alidai kuwa yule alishaolewa na anasheria zake za familia yake so akija hapa tutaanza kukinzana kwani hatoweza kuishi kwa kunifuata mimi. Nikicheki sehemu ya kulala ipo kwa sababu wadogo zake huwa wanakuja na wanakaa zaidi ya mwezi lakini sijawahi kujisikia vibaya .Ila kwa hili roho iliniuma sana kwa sababu dogo nilishamwambia aje halafu mke wangu hataki.Mwisho akaniambia nichague moja kama atakuja mdogo wangu yeye arudi kwao .Nikazidi kuvurugwa ikanibidi nimshirikishe mama yake mama yake nikaona anaegemea upande wa binti yake.
Nikaenda kwa mdogo wangu nikamwambi kule kwangu hakuna mtu wa kukuangalia kwa ukaribu zaidi so nitakutafutia house girl akutunze hapa nyumbani(Alikuwa amerudi kwenye nyumba ya marehemu baba)
Ila nikakaa na mke wangu nikamwambia kuanzia leo wewe na mimi tutaishi wawili tu hapa sihitaji kuona ndugu yako wala ndugu yangu ili kusiwe na upendeleo na ikitokea akaja ndugu yako nitamdhalilisha mbele yako.
Na yeye akaenda kushitaki kwa mama yake ,Nikaitwa na nikatoa maelezo nikamwambia mama sisi wote tunafamilia nyuma yetu ndugu yangu ameshindwa kuja kuugulia nyumbani kwa sababu nyepesi sana leo hii mimi nitajisikiaje akija ndugu yake yeye wakati mimi ndiye mtoa huduma wakaniomba radhi .
Na mdogo wangu alikuja pale kwangu akaugua mpaka akapona na maisha yanaendelea vizuri.
Maisha ya ndoa yana changamoto nyingi sana

Pole sana..mh!
 
Back
Top Bottom