Je umewahi kusikia adhabu kama hii kwa shule za msingi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je umewahi kusikia adhabu kama hii kwa shule za msingi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kimbori, Apr 13, 2012.

 1. Kimbori

  Kimbori JF-Expert Member

  #1
  Apr 13, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 2,738
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Waalimu wa shule ya msingi Mbezi Ndumbwi iliyopo Mbezi Beach jijini Dar es salaam, wanawaadhibu wanafunzi wasiofanya majaribio ya kulipia wakati wa asubuhi (speed test) kwa kuwakalisha chini (sakafuni) siku nzima.
  Wakati wa kuingia darasani asubuhi, wanafunzi wa darasa la 4, 6 & 7 waliofanya mtihani wa asubuhi, huitwa majina na kuruhusiwa kuingiza madawati watakayokalia. Wanafunzi wasiofanya mtihani hupewa adhabu ya kukaa chini siku nzima huku madawati yakibaki nje bila kutumiwa.
   
 2. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #2
  Apr 13, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  nchi hii kila mtu anajiamulia lake, sasa hapo kosa la watoto au wazazi? na ile ruzuku ya wanafunzi ina kazi gani? au wizara haiipi shule ruzuku? au kamradi kwa walimu?
   
 3. Kimbori

  Kimbori JF-Expert Member

  #3
  Apr 13, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 2,738
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Huu ni mradi wa waalimu! Wazazi wamelipia madawati. Wanafunzi wengine wanalazimika kukaa chini kwa kukosa madawati, huku madawati hayatumiwi. Mwalimu Mkuu akiulizwa anakuwa mkali kama mbogo, anawadharau wazazi, shule inapaoromoka, .....
   
Loading...