Je umewahi kupigiwa simu kwa namba hii +255901761234?

ipwisi

Member
Jul 11, 2015
38
15
Kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikipigiwa simu kwa namba hii + 255901761234 lakini nikiipokea sielewi kinachoongelewa na kibaya zaidi nimeshindwa kujua hii namba ni mtandao gani hapa nchini Tanzania. Naomba mchango wenu wapendwa jumatatu njema.
 
hao ni SBT Japan wauzaji wa magari hata leo asubuhi wamenipigia wanauliza unampango wa kununua gari au la wanatumia IP Phone nafikiri
 
kuna kadada kanaongea siwapend kwel hao na namba zao
 
Mm napigiwaga nayo ukipokea unasikia mihito za nyimbo na mengine usubufu tu
 
Hiyo namba inatumiwa almost na customer cares almost wa mitandao yote it depend na wwe unatumia mtandao gani...mara nying wanapiga ili kukutaarifu ofa na taarifa mbali mbali...
 
Hiyo ni number yangu huwa nawapigia watu kuwapa mkwanja.

Sasa kama huelewi lugha ipi inayoongelewa ndo kukosa kwako pesa.
 
Hiyo number ni ya mtandao husika unaoutumia hivyo usiache kupokea inaweza kuwa inahusu promotion, kuhakiki usajili wako, kuwakilisha madai yaliyoripotiwa na mteja juu yako kama vile kutumiwa pesa kimakosa, pia inaweza kuwa ya bahati so usipopokea na bahati yako bhasi.
 
Utakuta kuna mtu aliahidi atakupigia mida flani kwa issue ya maana,

Simu inaita na wewe unakuwa na hamaki kubwa kupokea kumbe ni hiyo namba.....inakera mno.
 
hao ni SBT Japan wauzaji wa magari hata leo asubuhi wamenipigia wanauliza unampango wa kununua gari au la wanatumia IP Phone nafikiri
Asante sana kwa mchango wako ila wanawezaje kupiga simu kwa kodi ya Tanzania +255 kwa kutumia mtandao ambao haupo hapa nchini? Au nimepitwa na huo mtandao mpya, msaada Tafadhali!
 
Hiyo number ni ya mtandao husika unaoutumia hivyo usiache kupokea inaweza kuwa inahusu promotion, kuhakiki usajili wako, kuwakilisha madai yaliyoripotiwa na mteja juu yako kama vile kutumiwa pesa kimakosa, pia inaweza kuwa ya bahati so usipopokea na bahati yako bhasi.
Asante kwa mchango wako, is this true? Au ndo kuongezeana siku za kuishi?
 
Kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikipigiwa simu kwa namba hii + 255901761234 lakini nikiipokea sielewi kinachoongelewa na kibaya zaidi nimeshindwa kujua hii namba ni mtandao gani hapa nchini Tanzania. Naomba mchango wenu wapendwa jumatatu njema.
Mkuu hiyo ni vodacom huduma kwa mteja hua same time wanakupigia wanakuuliza maswali kuhusu kukuingiza kwenye droo ya ushandi labda wa gari au chochote ambacho kimedhaminiwa kwao hua mara kwa mara wananipigiaga sana nawakatia cm!!ila nilichogundua kama kwenye salio lako la kifedha (m.pesa) kama una hela nyingi hawa jamaa hua wanasumbua sana kama wakiona salio lako ni kubwa!!
 
Back
Top Bottom