Je, ulijisikiaje siku ya kwanza ulipoijaribu bangi? Mwenzenu ilikuwa hivi...

Niliwahi kuletewa mochwari na wavuta bangi mlevi aliyezima kwa viroba wakisema eti ni maiti wameiokota
Nisingekuwa mweledi ningemtia kwenye jokofu lakini nikasema ngoja nimfundishe kuacha pombe, nikamuweka chini sakafuni penye baridi sana na maiti ambazo bado nilikuwa sijaziingiza kwenye jokofu
baada ya kama nusu saa akazinduka...
Kuangalia kazungukwa na mizoga kuangalia mbele nipo mimi na koti jeupe akajijua tayari....nikimuona ananyanyua mdomo apige kelele huku macho yamemtoka pima lakini alishindwa....alikuja kuzindukia wodini
hahahahah nadhan ameshaacha
 
Aseee mi nakumbuka siku hiyo ilikuwa nzito mno
Maana nilipata mawenge ya maana
Shughuli ilianzia maskani na washkaji basi nilipiga pafu kiasi
Baada ya muda kidogo nikawa naskia mwili km unavibreti
Nikasema ohoooo isiwe shida fasta nikachomoka mpaka home tena huku nakimbia...Nilivyofika hom nikaingia room basi nikawa kama nimepigwa na butwaa huku naangalia viatu
Mwisho ikaja hali ya kucheka bila sababu afu baada ya sekunde kadhaa najiuliza nacheka nn...Mungu si mzee mkumba mara mshua akaniita tena yupo na wageni kama wanne hivi sebuleni ile kufika tu kumuona mmoja kati ya wale wageni niliangua cheko la haja
Wakiniuliza nacheka nn ndio wanakuwa wamenizidishia kicheko
Mwisho mzee akanambia we chizi nn
Nikasepa tena ghetto nakumbuka nililala kwa tabu mno ndoto za ajabu tu
Hahahahahahah mkuu umenichekesha kishenz
 
dah huu uzi mtamu kinoma, mi huwa navuta feg bt hazinitesi wala nin, lakn nafaham kabsa feg ni mbaya bt how to stop it ndo shida wakuu.. ganja cjawah jaribu mana kuna mwanetu kitaa kawa zuzu kwa hayo maswala.
 
So good, so freshh.. Kawaida tu, zaidi napata apetite ya kupiga menu na kunywa vimiminika kwa sana.. Bangi zangu za buku jero.. Kadhaa za juice
 
Nakumbuka napiga hiki kitu kwa mara ya kwanza nipo la 7 na jamaa zangu wawili ambae mmoja tayari ka R.I.P,tulificha jumba mbovu tumepiga wee hadi kuvua mashati tumetoka njaa inauma tukashauriana tunafanyaje na majumbani msosi bado hawajapika mana siku hiyo ilikua weekend na ni asubuhi,mwenzetu mmoja akasema naenda kuiba maandazi ya mama mana alikuwa akiwauzia watu asubuhi jamaa akasema nisubirini kidogo baada kama dk 10 jamaa kaja na ndoo ya maandazi sijui hata alitoka nayo vipi bila kuonekana ikabidi twende nayo kwenye lile jumba mbovu tulikula yote huku tukishushia na maji hadi kupitiwa na usingizi kumbe mama mtu kacharuka anatafuta maandazi yake na bahati mbaya ama nzuri kuna mtu alituona tukiingia na ndoo kwenye lile jumba, wakaja wakakuta tunachapa usingizi na pembeni mbegu za bangi kibao na harufu ya bangi bado ipo wakatuzibua mavibao hata maumivu hatuhisi tunaishia kucheka tu mama mtu akasema mi sikubali hawa watoto wanaenda polisi wamenitia hasara tukaveshwa mashati na kufunganisha kwenye kingo za mashati kama wezi hadi kituoni mama akajieleza kosa letu wakamwambia hawa njooni muwachukue saa 12 jioni dawa yao ndogo hawatarudia tena,asee tulikula fimbo za waya matakoni inapitishwa mara 2 afu unasikia afande anasema hicho ndo cha kwanza yalipigwa mayowe ya Hatari mana tulipigwa 10 sawa na viboko 20 kila mtu mana inapitishwa mara 2 kisha tukamwagiwa maji ya baridi na kupelekwa hicho chumba cha mahabusu tukawakuta makaka wawili ambao waliletwa kwa kosa la wizi wakawa wanatuuliza mmefanyaje si kimya mana muda huo unaugulia maumivu kukaa chini hatuwezi tako limevimba hadi unasikia Ganzi na wale makaka kuona hatujibu wakawa wanatupiga makonzi eti tunawadharau hatutaki kuwajibu,tulilia hadi macho yakawa makavu tunatamani saa 12 ifike tutoke mana mule ndani kulikua si kuzuri muda ukafika yule mama akaja kutuchukua kumbe kashasema hadi kwa madingi kizaazaa kikahamia nyumbani....sitasahau japo mmea mara mojamoja si mbaya
 
...Day 1 kitu kilikaa poa nikaishia mazarau na kula saana ugali wa bi mkubwa, Day 2 nikaona ngoja nipande juu ya bati ili harufu isienee baada ya kula stick 3 nikaanza kunyata kwenye bati letu nikizani sionekani kumbe nyumba za jirani wananiona...dah ndumu noma saaana...J

uzi juzi nikashtua tena basi mbwa wetu wakawa wanalia saana mi ninakawa naona kama malaika wanashuka kwa kasi toka mbinguni wanatawanyika wengine wanakuja kwangu kila wakiwa wananikaribia mbwa wanalia saana...Basi staki tena hii kitu inaweza kukuabisha!!
 
Mara ya kwanza nakula kaya, nilikula na jamaa nikafanya kama ndio uwa mpango wangu, nimekula kitu kimoja tu.. Njaa ya hatari mpaka tumbo lina kwangua, nikaondoka mpaka home, kufika home nakuta msosi mezani baba bi mkubwa na madogo na wageni.. Nikapakua msosi mbwa haruki, bila kusalimia wa kuwaangalia watu nilio wakuta, nikainamia chakula nikapiga msosi faster faster, gafla nikajishtukia mbona kimya sana, nikainua macho kuwatazama, nawatazama nakuta wote wamestop kula wananiangalia.. Nikarudisha macho kwenye sahani, nakuta inazunguka mezani kwa speed.. Nikaona aahaa kumbe sahani inazunguka ehee,! Nikaweka kijiko chini nikaanza kw mikono, navizia sahani kwa timing mpaka na nesa nesa, kisha napereka mkono faster nachukua tombe mdomoni, kama mara nne hivi.. Ghafla nilipokea kofi la shavuni paaaah.. Nikazila chakula nikaondoka home.. Shule basi nikaanza kukomaa mtaani.maana ndio ukawa mwisho wa shule, mzee kanikata sio mtoto wake..

Nashukuru leo nipo na familia maisha mazuri nashukuru Mungu nipo vizuri na ni baba mzuri. Ila siwezi kuacha kitu naama sina kilevi kingine zaidi ya iko, nisipo pata wife ananiambia kapate Mr wangu, japo mwanzo alipata shida.. Ila sijawah kumpa shida nikismoke
 
Back
Top Bottom