Je! Tunajifunza nini baada ya uchaguzi wa 2015?

TAWA

JF-Expert Member
Jun 23, 2013
3,673
1,571
Wanabodi salam
Jana 23/06/2016 tulikuwa tunatamatisha zoezi la uchaguzi mkuu wa 2015 kwa tume ta taifa ya uchaguzi NEC kumkabidhi rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ripoti ya mwenendo mzima wa uchaguzi jinsi ulivyokuwa.
Nataka kufahamu tu, baada ya uchaguzi ule sasa ni takriban miezi nane, je tumejifunza nini ndani ya miezi nane?
 
nikichojifunza mimi tuache kufanya maamuzi kwa kupendelea rangi fulani. inacost sana
 
tumejifunza kuwa na tume ya uchaguzi iliyo timamu kama ile ya Jecha ni muhimu sana vinginevyo nchi inaweza kuingia kwenye machafuko!
 
Wanabodi salam
Jana 23/06/2016 tulikuwa tunatamatisha zoezi la uchaguzi mkuu wa 2015 kwa tume ta taifa ya uchaguzi NEC kumkabidhi rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ripoti ya mwenendo mzima wa uchaguzi jinsi ulivyokuwa.
Nataka kufahamu tu, baada ya uchaguzi ule sasa ni takriban miezi nane, je tumejifunza nini ndani ya miezi nane?
tumeweza kujifunza uchaguzi wa uingereza jana wameamua kujitoa EU, demokrasia ya hali ya juu,waziri mkuu na serikali hawakutaka wajitoe. lakini hapakutumika nguvu ili wabakie..
 
Nimejifunza kuwa upinzani Tanzania hauna msimamo na hauna nia nzuri na nchi yetu.

Wapo kwa ajili ya maslahi yao binafsi.
Wame achana na sera ya kupinga ufisadi sasa hivi wanakumbatia ufisadi.
kwa hiyo fisadi ni nani ndani ya chadema?
 
Nimejifunza Tanzania inaelekea katika Vita ya Wenyewe kwa wenyewe

Kwasababu
Vyama vya siasa vinakandamizwa asaivi
Wananchi hatuna uhuru wa kutoa maoni
Katiba inavunjwa

Mwisho wasiku tutaambiwa marufuku Kulala na mkeo na hatimaye ndipo zitakapo pigwa hapo
 
Tafuta hotuba ya CHADEMA pale mwembe yanga. Ni wao wenyewe waliwataja mafisadi. Halafu ni wao hao hao wakawapa dhamana kubwa hao mafisadi.

Tafuta hiyo hatuba ndugu. Na kuna mmoja alitaja kuwa atakaye mpigia kura huyo fisadi apimwe akili.

Sasa lengo lao ni nini?
Kweli tumejifunza mengi hatuna budi sasa kuachana na ukawa.
 
tumeweza kujifunza uchaguzi wa uingereza jana wameamua kujitoa EU, demokrasia ya hali ya juu,waziri mkuu na serikali hawakutaka wajitoe. lakini hapakutumika nguvu ili wabakie..

Mi nafikiri hilo kwa afrika ni ndoto za alfajiri. Hakuna demokrsia hata robo kijiko afrika. Walio madarakani wnafikiri haki yao pekee ni kushinda kwa chochote kile hata ujinga
 
Tafuta hotuba ya CHADEMA pale mwembe yanga. Ni wao wenyewe waliwataja mafisadi. Halafu ni wao hao hao wakawapa dhamana kubwa hao mafisadi.

Tafuta hiyo hatuba ndugu. Na kuna mmoja alitaja kuwa atakaye mpigia kura huyo fisadi apimwe akili.

Sasa lengo lao ni nini?
Kweli tumejifunza mengi hatuna budi sasa kuachana na ukawa.

Sasa kama ishu ni lowasa vipi ccm kutokana na hotuba ile wamebaki mafisadi wangapi? Maana wametajwa wengi katika ile orodha
 
Kama wewe ulitaja kuwa flani ni fisadi basi ni wewe mwenye wajibu wa kujitenga na huyo fisadi. Lakini ikitokea sasa wewe umemtuhumu mtu fulani ni fisadi halafu baadae kwa tamaa zako ukaamua kumkumbatia ili upate kura. Hakika wewe utakuwa na nia mbaya na jamii inayo kuzunguka. Na utakuwa na tamaa mbaya.
 
Nimejifunza upinzani hawana msimamo manake katikati ya safari mwenyekiti wa CUF akajiuzulu kidogo katibu mkuu mpendwa wa CHADEMA naye katoka nje ya ulingo kwa sisi tuliokua serious tukabaki na mshangao!!!!
 
Hujui unaloliongea wewe!
 
Nimejifunza Tanzania inaelekea katika Vita ya Wenyewe kwa wenyewe

Kwasababu
Vyama vya siasa vinakandamizwa asaivi
Wananchi hatuna uhuru wa kutoa maoni
Katiba inavunjwa

Mwisho wasiku tutaambiwa marufuku Kulala na mkeo na hatimaye ndipo zitakapo pigwa hapo
Haya unayotoa sio maoni au umeshikiwa mtutu??

Au labda ulitaka utoe live kupitia TBC ndio uone una uhuru wa kutoa maoni?
 
Nimejifunza upinzani hawana msimamo manake katikati ya safari mwenyekiti wa CUF akajiuzulu kidogo katibu mkuu mpendwa wa CHADEMA naye katoka nje ya ulingo kwa sisi tuliokua serious tukabaki na mshangao!!!!
Sema mkabaki mnamzungushia mikono Fisadi
 
Back
Top Bottom