Je, tuliwatuma Bungeni kujadili hoja au kujadili tabia za watu? Hoja za Jerry Silaa na Askofu Gwajima zinahitaji majibu

seedfarm

JF-Expert Member
Feb 9, 2020
260
2,654
Bunge zima wamejaa wana CCM, Wanajadili tabia za watu badala ya kujadili hoja aliyoongea mtu, Je? hii ndio kazi tuliwatuma Bungeni?

Hoja ya Jerry Silaa anasema wabunge hatulipi kodi, tuanze kulipa kodi ili tuwe mfano kwa watanzania wanaoumia na kulipa kodi.

Majibu ya wabunge wa CCM: wanasema Jerry Slaa ni kijana mdogo, Jerry Slaa ni mgeni Bungeni, Jerry Slaa aombe radhi, Jerry Silaa ananyanyua mabega, Sheria inasema wabunge wasamehewe allowance na posho wasilipe kodi lakini Jerry Silaa hajui tumtoe kamati ya PAC, CCM tuna utaratibu wetu wa kuongea mambo, Jerry Slaa alikuja kwenye kamati na vitabu vingi kuonyesha dharau kwa Spika.

Hivi wabunge wa CCM mna matatizo gani badala ya kujibu swali mnajadili tabia za mtu, Je, kodi mnalipa au hamlipi kodi?

Hoja ya Askofu Gwajima, Kwanini Waziri wa afya na naibu wake ni vigeugeu walisema chanjo hazifai, Chanjo hizo zinagusa utu wa Mtu yaani DNA mbele ya Rais Magufuli na watanzania, Leo Waziri na naibu huyo huyo wanasema chanjo zile zile zinafaa mbele ya Rais Samia, Chanjo ina madhara gani ya muda mrefu au mfupi?

Majibu ya wabunge wa CCM: Gwajima aligoma kukaa kwenye kiti wakati wa kuhojiwa ashughulikiwe, Gwajima anahatarisha amani ya Taifa vyombo vya ulinzi ashughulikiwe, Hata sisi tuna dini zetu Gwajima hajasoma vizuri biblia, Mimi nimetembea Israel yote najua umbali Yesu aliotembea, Msipomkamata Gwajima tutaanza na Waziri wa Mambo ya ndani, Gwajima angekuwa Rais Magufuli asingeyasema Haya, Mimi simuogopi Gwajima nimejitoa sadaka akanisema kanisani kwake.

Ahaaaa, Hivi kwanini msijibu hoja mnaanza kujadili mtu, Tuliwatuma Bungeni kujadili watu? Jibuni hoja za Askofu Gwajima.

Je, Waziri na naibu wake ni vigeugeu kuhusu chanjo au sio vigeugeu?

Je, chanjo zinafaa au hazifai na zina Madhara gani ya muda mfupi au mrefu?
 
Sikio la kufa ..... Yote haya ni matokeo ya Uchafuzi Mkuu.
 
Bunge Lile Tumepigwa Mchana Kweupe Ndugu
Gwajima Ni Mjeuri Haa
 
Tangu lini sisi wana ccm tukajibu hoja bwana, Mimi ni mwana ccm wakati wa kampeni za uchaguzi, Tundu lissu alipokuwa anashusha nondo na hoja nzito nzito nilishauri wana ccm wasimjibu Tundu lissu watazidi kuharibu

Nilileta uzi hapa JF na ilisaidia sana,

Hoja hujibiwa kwa hoja sio kwa kuzipiga lungu(Jakaya Kikwete nuku)

Kikwete baada ya kusema hayo akachukiwa na wana ccm akiwepo kijana Ally Hapi na Musiba cypirian

Hoja za lissu zilikuwa watu wanabambikiwa kodi, Hakuna Maendeleo bila watu kuwa huru

Majibu yalikuwa lissu ni kibaraka, Lisu anatumiwa na mabeberu

Badala ya kujibu swali wana ccm tulikuwa tunajadili personality za lissu

Mtu ambaye hana hoja za kujibu au kazidiwa na hoja hukimbilia kujadili tabia za mtu
 
Back
Top Bottom