Jerry Silaa: Serikali iweke Tozo ya Tsh. 100 kwenye mafuta yanayonunuliwa Dar ili Kupata Pesa za Kujenga Barabara za Jiji

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
42,433
49,102
Akichangia mjadala wa Bajeti ya TAMISEMI, mbunge wa Ukonga Jerry Silaa kwa niaba ya Wabunge wa Dar es Salaam amependekeza kwa Serikali iweke Tozo ya Shilingi 100 kwa mafuta yanayonunuliwa Jijini humo ili kupata Fedha za kujenga Barabara za Jiji la Dar es Salaam.

Jerry Silaa amesema amesema Jiji la Dar es Salaam linatumia zaidi ya Lita milioni 3 kwa siku ambazo zinaweza kuwezesha Jiji la Dar kupata Bil. 130 Kwa mwaka ambazo zitatumika kujenga Miundombinu ya Barabara ndani ya Jiji Hilo.

Aidha Slaa amesema Tsh 100 itakayoongezwa italeta msawazo wa bei na maeneo mengine ya Nchi ambayo yananunua mafuta Kwa bei kubwa sana, akisema formula yake ataiwasilisha Kwa Waziri wa Tamisemi na Wizara ya Fedha.

My Take: Jerry Silaa ana Hoja ya msingi na asikilizwe, nimeipenda ubunifu wake sio Kila kitu kusubiria mikopo.

Yani wapige maelea zaidi ya hizo kila.mwaka halafu eti waseme yozo iwekwe kwenye mafuta kupata ela ya kujenga miundombinu hivi hawa wabunge wamelaaniwa au...
Hilo la kupiga ni hoja pia ila umewahi sikia Tarura pesa imepigwa? Hizo pesa zinaenda Tarura sio Jiji la Dar vinginevyo endeleeni kuongelea kwenye mashimo maana Kwa Sasa Serikali Haina pesa kwenye regular budget na ule mradi wenu wa DMDP umeyeyuka
 
Sawa yawezekana ana hoja ya msingi but chanzo chake cha pesa kwaajil ya hizo barabara noooo!! Nadhan zichukuliwe kwanza pesa zote zilizoibiwa toka report ya CAG iliyopita mpaka hii ya sasa, litolewe fungu kwaajil hiyo!!!
Pesa zimeibiwa sasa zichukuliwe kutoka wapi? Jerry ana hoja kumbuka hiyo ni specific Kwa Dar tuu.

Pia Vyanzo vingine sio sustainable, kama Sumbawanga wananunua bei kubwa kuliko Dar Kwa nini Dar msinunie bei sawa na wao tena Kwa faida yenu?
 
Pesa zimeibiwa Sasa zichukuliwe kutoka wapi? Jerry ana hoja kumbuka hiyo ni specific Kwa Dar tuu.

Pia Vyanzo vingine sio sustainable,kama Sumbawanga wananunua bei kubwa kuliko Dar Kwa nini Dar msinunie bei sawa na wao tena Kwa faida yenu?
Walioiba hawafahamiki na kama wanafahamika sheria mnaziogopa kuzitumia?
 
Akichangia mjadala wa Bajeti ya Tamisemi,mbunge wa Ukonga Jerry Silaa Kwa niaba ya Wabunge wa Dar es Salaam amependekeza Kwa Serikali Iweke Tozo ya Shilingi 100 Kwa mafuta yanayonunuliwa Jijini humo Ili kupata Fedha za kujenga Barabara za Jiji la Dar es Salaam.

Jerry Silaa amesema amesema Jiji la Dar es Salaam linatumia zaidi ya Lita milioni 3 Kwa mwaka ambazo zinaweza kuwezesha Jiji la Dar kupata Bil.130 Kwa mwaka ambazo zitatumika kujenga Miundombinu ya Barabara ndani ya Jiji Hilo..

Aidha Silaa amesema Shilingi 100 itakayoongezwa italeta msawazo wa bei na maeneo mengine ya Nchi ambayo yananunua mafuta Kwa bei kubwa sana,akisema formula yake ataiwasilisha Kwa Waziri wa Tamisemi na Wizara ya Fedha.

My Take..

Jerry Silaa ana Hoja ya msingi na asikilizwe,nimeipenda ubunifu wake sio Kila kitu kusubiria mikopo.
Tozo ndio ubunifu 😄😄😄
 
Hiyo 100 iwekwe kwenye posho za wabunge.. akili matope sana
 
kwa mantiki hiyo ya kusawazisha bei hata wafanya biashara wa chakula wanaofuata vyakula mikoani, kwa mfano wa mchele nao serikali iwape ruzuku kidogo ili bei ya mchele dar ishuke iwe sawa na mbeya na mikoa mingine?
Ndio Kwa sababu si unapunguza tozo za masoko Ili bei iwe nafuu?
 
Back
Top Bottom