Je, TCRA watazimaje simu bandia ifikapo June?

ymollel

JF-Expert Member
Aug 23, 2012
3,096
2,279
Kuna maswali mengi sana mitaani watu wakisema mwezi wa sita simu feki zitazimwa.

Kitaalamu na kiuhalisia TCRA hawataizima simu iliyo feki, na si kwamba simu iliyokuwa imewashwa itazimika na kuwa OFF. bali simu isiyotambulika itashindwa kujisajili na kupata mtandao kwa kutumia simcard husika.

Je tutegemee simu bandia zitaonyesha dalili gani.

- Network registration failed.
-cannot register to the network.
-Failed to register.
-registering to the network.......

Etc etc.

Hivyo kama una simu feki sijui

OKIA
NOKLA
SAMSVUNG
BLACKDERRY
SQNY
OKING

simu yako haitazimwa utaweza kusikilizia muziki, na kupiga picha kama ina kamera ya maana.
 
umesahau na simu ya TECNO!
INFACT MIMI SIAMINI KAMA HZI SIMU ZITAFUNGWA, HII VITA YA KIBIASHARA!!
 
Swali ni Je, kama wanazifunga kwa kutambua IMEI bandia, Simu bandia yenye IMEI halisi (original) ya simu zingine itafungwaje?
 
Wakizima tutatafuta njia m badala ya ku bypass hiyo restriction. The time will tell. Tz simu feki ndo nyingi kuliko original hasa hizi smartphones.
 
Ningeishaur kitu kimoja serikali, Kwnz naunga mkono hatua hiyo kutokana na sababu na ukweli ulvyo, lkn tukirud kwa watz wny kipato cha chini walio wengi hii itakua changamoto kupata simu nyngn orijino kwa matumizi muhimu ya mawasiliano ya simu ya mkononi kutokana na Bei ya juu watakazouza, hapa nna uhakika Wauzaji wa simu orijino watapandisha Bei, hvyo naishaur serikal iingilie kati suala hili la bei isipandishwe na iwe bei ya chini ili watanzania waAcces simu orijino, *wafute machozi
 
Huku kwetu kuna simu inagoma kustart baada ya kutuma IMEI ya simu kwa namba ya TCRA ile ya 15090

Yan simu ukiiwasha inaandika ''phone startup failed please contact the retailer''
 
Simu zitafungwaje wakati bado zinaingia nchini kama utitili na ushuru zinalipiwa?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom