Je TANESCO wanajitambu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je TANESCO wanajitambu?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Maswa, Feb 1, 2012.

 1. M

  Maswa Member

  #1
  Feb 1, 2012
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu wana JF, napenda kushiriki nanyi ili kujua namna ambavyo TANESCO wanavyofanya kazi.
  Kwa mtizamo wangu, naona kama vile hili shirika halina uzalendo na wala moyo wa kuwezesha maendeleo ya nchi. Maana yangu ni kwamba, TANESCO ilitakiwa kuja kuweka umeme kwenye mtaa wetu toka mwaka 2008 lakini mpaka leo hii hakuna kilichofanyika zaidi ya usumbufu wa ufuatiliaji.
  Pamoja na ongezeko la 40% ya gharama za umeme lakmini hawatendei haki watanzania hasa wa vijijini ambao wanaona kwamba hawana hela za kuwapa takrima!
  Rai yangu ni kuhakikisha wanatekeleza ahadi wanazowapa wananchi hasa wakati wanapokuwa wakitaka kutimiza azima yao.
  Mfano; Walituomba kwa njia ya barua kwamba turuhusu kwa haraka umeme upite kwenye maeneo yetu kwa ahadi ya kutuletea transformer bure ikiwa ni sehemu ya fidia badala ya kutulipa na sisi tulikubali kwa haraka kupitisha umeme na nguzo kwenye viwanja na maeneo ya wananchi, sasa mpaka leo ahadi imeshindikana kutekeleza ktk miaka minne(4).

  Wadau naomba ushauri sisi walengwa tufanyeje? tuwashitaki TANESCO? maana barua ya toka 2008 waliyotuandikia tunayo na kumbukumbu ambazo tumekuwa tukiwakumbusha! Kibaya zaidi kuna muwekezaji ambaye alipelekewa umeme wakati huo tulipoahidiwa na ndiyo maana walihitaji turuhusu haraka ili mwekezaji apelekewe umeme, na mwekezaji alilipa hela nyingi ikiwa ni pamoja na kusaidia wanakijiji/mtaa na alilipa hela nyingi sana sana zaidi ya Milioni 200 kupelekewa yeye na wanakitongozi.

  Wananchi wanahasira kiasi kwamba wanataka kung'oa nguzo za umeme!

  Tunaomba ushauri!
   
Loading...