Je, sisi Wanaume wa Kitanzania ni wakatili au tatizo ni nini?

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
Katika maisha yangu yote siku zote nionapo mtoto ana matatizo huwa namuona tu yuko na mama yake, ni nadra sana kumuona mtoto akiteseka na baba yake pembeni, kama ni mtoto aliye na ulemavu na hajiwezi kwa lolote basi anayemuhudumia yule mtoto siku zote ni mama yake tu baba yake haonekani, na kamwe sijawahi kumuona Mwanaume wa KitanZania kapiga picha na mtoto wake anayehitaji msaada lkn ni kawaida kumuona Mwanaume wa KitanZania kapiga picha na mtoto wake aliye na afya na anafanya vizuri maishani!

Sasa ni kwa nini? tatizo ni nini? Je, sisi ni wakatili na wabinafsi au kuna sababu yoyote ile ya msingi inayotufanya tuwe hivi?

Labda kuna sababu kwa nini Diamond Platinumz anampa bata Mama yake na hana mpango na wala hataki hata kumsikia baba yake!
 
Back
Top Bottom