monjozee
Senior Member
- Sep 19, 2016
- 115
- 297
RIPOTI YA FARU JOHN IMEKAMILIKA,JE SERIKALI IMEMSAHAU BENARD SAANANE?
(Mwenye kusoma andiko hili na aelewe)
Na; Mohonia JP
Baada ya kelele za serikali za muda mrefu juu ya upotevu wa faru John anayedaiwa kununuliwa kwa gharama, na sakata lilipelekea Watanzania kupigwa "STOP" kulijadili (kwa bahati nzuri tulitii) na kuamua kukaa kimya bila kulijadili.
Ofisi ya Waziri Mkuu iliamua iundwe Tume maalum ya kuchunguza kifo cha mnyama huyo, Tume ambayo ilikuwa chini ya Mkemia mkuu wa Serikali Prof. SAMWEL MANYELE.
Leo Tume hiyo imekabidhi ripoti hiyo inayodaiwa kukamilika,ambapo majibu ya ripoti hiyo ni kuwa "IMETHIBITIKA KUWA FARU JOHN ALIKUFA KUTOKANA NA KUKOSWA MATUNZO".
Okay, fine,turudi kwenye mada ya msingi.
Kwa kulijadili hili la faru John na kwa kululihusianisha upotevu wa Mtanzania mwenzetu.
Nitauliza Maswali kwa Watanzania wenzangu wa nchi hii kupitia MAANDISHI.
Moja; Faru John alivyobainika kupotea tume iliundwa,lakini Mtanzania mwenzetu ndg. BENARD SAANANE, mpaka sasa ninavyoandika hakuna tume iliyoundwa kumtafuta binadamu huyu, wala hakuna jitihada za makusudi za wazi za kututia moyo sisi Watanzania wa kawaida kuona kweli serikali inalifanyia kazi suala hili.
Polisi walishafikishiwa suala hili wakaahidi kulifanyia kazi, lakini kwangu binafsi, sina hakika kama linaendelea kufuatiliwa kwa kuwa;
(a) Polisi wamekaa na suala hili kwa muda mrefu bila kutoa taarifa za awali kwa umma juu ya Mtanzania huyu.
(b) Sijawahi kusikia jeshi la polisi likimuita mtu yeyote ama kikundi/viongozi wa chama alichokuwa anakifanyia kazi huyu ndg.ili kuwahoji.
(c). Sijawahi kusikia kuwa kuna mtu yeyote mpaka sasa anayetuhumiwa "walau" kwa hatua ya kwanza ili kusaidia upepelezi,kama tulivyozoea kusikia katika vyesi vingine.
Nauliza Watanzania wenye nchi hii,hivi tulikalia kimya suala hili mpaka lini?
Tukumbuke,leo kwako, kesho kwangu. Serikali imekuwa busy kutafuta "uthibitisho" wa kifo cha mnyama, badala ya kumtafuta binadamu.
Tunakaa kuangalia kukabidhiwa ripoti ya mnyama "LIVE" kwenye Televion zetu huku tukipiga makofi, na kushangilia.Tumesahau, kuna Mtanzania mwenzetu, tumesahau kuna mwanadamu mwenzetu ambae haonekani.Tumesahau kuna binadamu wenzetu miili yao iliokotwa mto Ruvu na kuzikwa ghafla, huku tukiaminishwa kuwa walikuwa "wahamiaji haramu".
GOD PROTECT US.
Nani aililie nchi hii. Nani ajitokeze kuunga mkono kumtafuta Mtanzania huyu mwenye familia na mtoto mmoja, ambaye kesho atakuwa mkubwa aulize "Baba yangu yuko wapi?".............Nani atakaempa jibu mtoto huyu.
Hakika naamini katika majibu yatakayotolewa neno "Tanzania" halitakosa.
Kwa imani yangu, Mtoto huyu ataichukia ardhi ya Tanzania mara mbili zaidi ya laana tuliyopewa na Mungu.
Nani asimame apige kelele katika nchi hii?
Who will volunteer?.... Maswali ni mengi yanayokoswa majibu sahihi ya kujibiwa.
Watanzania tuziache tofauti za vyama, dini na makabila yetu, tuvae jezi moja yenye jina "TANZANIA, UTU NI MUHIMU ZAIDI",hakika tutampata kijana huyu.
Chama changu cha CHADEMA, kuanzia mimi ninaendika mpaka yule mwenyekiti wangu mkuu wa Taifa, tunamtaka BENARD SAANANE.
His our brother, his our fellow Tanzanian, we MUST search for him.
Mh.Freeman Mbowe, tunakutambua kwa ukamanda wako na ujasiri katika kuendesha Operations mbalimbali.
Katika hili, ninakuomba ulitake Jeshi la Polisi litoe ripoti yake, anagalau ya awali.
Na kama haiwezekani, ninakuomba serikali iseme kama jitihada zake zimefeli, Watanzania wenye moyo wa "UTU", "UZALENDO" na "MAPENZI MEMA" kwa binadamu wenzao tutamtafuta BEN, hata kwa kumuliza na kurunzi usiku.
HIS OUR FELLOW TANZANIAN
HIS OUR BROTHER
I'M CRYING FOR BEN SAANANE.
KALAMU YANGU NAWEKA CHINI,MWENYE KUSOMA ANDIKO HILI NA AELEWE.