Vitalis Msungwite
JF-Expert Member
- May 11, 2014
- 3,318
- 7,983
JE, SERIKALI HAIYAJUI MAKAMPUNI YA KITAPELI TANZANIA?
*Soma hadi mwisho Usijetapeliwa*
Kufa Kivyako na Koma Kutulaghai Wenzio ukitushawishi kujiunga na hizi E- Commerce; QNET, H2I, GLOBAL ALLIENCE, FOREVER LIVING; D9 nk
E-commerce ( électronic commerce) maana yake ni ile hali ya kuuza na kununua bidhaa kupitia mtandao wa internet. Kwa maana kwamba biashara yote hukamilika kwa njia ya mtandao. Kwa maana nyingine e commerce huitwa internet commerce.
Hapa nchini, kuna wimbi kubwa la aina ya biashara mtandao nazo ni kama zilivyo tajwa hapo juu yaani: QNET, H2I, GLOBAL ALLIENCE, FOREVER LIVING na D9. Watumishi wengi hasa wa idara ya Elimu (walimu) wametia fora kupapatikia kujiunga na wengi wao wanalia na kusaga meno maana wamezika huko milioni zao kadhaa wakitarajia kuwa ma MILLIONNAIRE, ajabu hawajakata taama; *Wajinga ni watu wa ajabu kweli* [emoji1787][emoji1787].
Walimu wa jinsia ya kike waliopo kazini na wastaafu wanaonekana kurubuniwa ama kulaghaiwa kirahisi maana inaonekana wao ndio walio wengi kuonekana kuchangamkia fursa rahisirahisi kumbe wamepotea,[emoji848]. *Nakwambia hakuna kupata pesa kirahisi hapa duniani
Wapo pia wanaume ambao nao wamejiingiza kwenye hizo biashara mtandao na kila siku wanatembea wakiwa wanajiona matajiri wa kesho (next millionnaires)[emoji1787][emoji1787]. *Ila milionea wa Leo hayupo, hatumuoni Why?*
Watu hawa ndio masaa yote asubuhi, mchana na usiku kucha kusumbua kwa mialiko yao ya semina (1rst presentation, 2nd presentation na 3 Rd presentation) huku wakitaka nasi tujiunge. *Nakusihi usitumie hata dakika moja kuwasikiliza, wana lugha ya ushawishi balaa na wamejipanga kwa hizo presentations, yaani wako vizuri kwa mipango isiyoiva* Jua kuwa wao mafanikio yao ni idadi ya binary bond aliyonayo. (BINARY TRY, Branches)
Baada ya kutoa huo utangulizi, sasa ona jinsi gani alipojiunga na hiyo biashara mtandaoni wanavyopata tabu na kuteseka kupata members.
Kila mtu ambae alidanganywa na akadanganyika kweli kweli na akaenda Bank akakopa mkopo au anauza shamba lake ama mifugo ili apate milioni kadhaa za kujiunga na biashara mtandao aliyoaminishwa kufanikiwa, sasa ivi anateseka sana kupata members maana ugumu wa hizi biashara zinaenda kwa njia ya matawi au washiriki (generation) wako ambao si chini ya 16.
Kwa bahati mbaya katika jamii ya kitanzania si rahisi umpate mtu haraka haraka umshirikishe na kumwelewesha kwa ushawishi manufaa ya e commerce furani na akuelewe chap chap na akubali kurisk milioni zake nne na nusu ( tshs. 4500000) au tano (5000000) kwa ajili ya biashara mtandao. Si rahisi sana nasema tena si rahisi sana kiivo kupata watu 16 wajiunge kwa hayo mamilioni. USIDANGANYWE
Pia, kwenye familia zetu ama majirani zetu, marafiki zetu si wote wanauwezo wa kupata hizo hela. Wengi wetu masikini ya Mungu hata Laki kuishika tu kwa pamoja ni ndoto sasa leo hii wewe unaanza kumwalika na kuaanza kumshirikisha biashara mtandao ya milioni zaidi ya 4.5[emoji848]
Baadhi ya biashara mtandao kama Global Allience wao wanajihusisha pia na uuzaji wa bidhaa ambazo niseme ukweli *si rafiki* na kipato cha jamii ya kitanzania hivo kuwa changamoto katika kupata wateja.
Qnet na D9, wao hawahusishi uuzaji wa bidhaa mitaani ila wanajihusisha na ununuaji wa bidha kwenye maduka yao kimtandao (shops) ambapo member anapaswa kununua bidhaa huko hasa hasa kuna Saa, camera, simu iPhone na japokuwa nao pia wanachangamoto ya bei ghali ya bidhaa hizo.
Kwa sasa, biashara mtandao inayovuma kwa watumishi, sisi walimu tukiwa tumetia fora kuitikia ni QNET. Hii QNET imeliza wengi na inaendelea kuliza wengi kama zilivyofanya D9, FOREVER LIVING, H2I na GLOBAL ALLIENCE.
Wengi wanaojiingiza huko wanapata ushawishi wa platform yake kubwa na kuonekana kuanzishwa na matajiri wa huko nchini malaysia. Hali kadhalika, kutokana na ufadhiri (sponsorship) wao kwenye baadhi ya makampuni na vilabu vya michezo ikiwemo Manchester City, kumiliki mahoteli na vyuo vikubwa duniani, watoa semina (presentation) hutumia kama major point kuwashawishi na kuwavuta watu kujiunga.
Leo hii watu wanajiunga na QNET bila kujiuliza watapata wapi binary members hadi 16 ( generations) wa kuwatengenezea matawi. Kumbuka kwamba the more your binary trees (branches) grows the more you get commissions. Tena watu wa QNET wao wanakwambia kila siku ya J2 na J4 ni siku ya Mavuno[emoji1787][emoji1787][emoji1787]. Hii iko applyied kwa biashara mtandao karibu zooooote.
Ndio, wewe umeweza kujiunga kwa maana una hizo milioni, je utawapata wengine watakaokuja kukujazia BINARY TREE yako ili itengeneze pesa kila J4?
Kwa hakika wengi hufeli hapo hapo. Utakuta mtu kajiunga na sasa ana miezi sita au mwaka na zaidi na hajapata hata mtu mmoja alieko nyuma yake[emoji12] yaani hana hata bond moja nyuma yake, hao 16 atawafikisha lini kama siyo ujinga?. Cha ajabu kila siku hutiana moyo kwa kuitana NEXT MILLIONNAIRES na salaam yao kila wakati ni *Good morning millionaire!*
Miaka ya 2015 hadi 2016, nilishuhudia walimu wanastaff wenzangu jinsi walivyoahidiwa kiuchumi na mawazo hadi familia zao kuyumba kutokana na wao kujiingiza kwenye D9 na H2I. Du! Aisee sitokuwa sahau. Sasa nazidi kushangaa sana navoona watumishi wanavopapatikia na kurubuniwa kipumbavu pumbavu kujiunga na QNET. Aisee!!
Wengi walijiunga na hizo business hali yao mbaya kabisa kwani kujiunga na Biashara mtandaoni ni hasara tasilimu na kukaribisha kwenye maisha yako:
- Umasikini
- Magonjwa yasiyoambukiza ( presha na kisukari)
- Msononeko na hali ya mfadhaiko
- Magonjwa ya Akili.
Swali linakuja ivi: Je, ya nini kumshawishi na kumvutia rafiki yako, ndugu yako mfanyakazi mwenzako sehemu kusiko kwenye ambako wewe mwenyewe unajuta kujiunga? Jamni, tupendane.
Na si vizuri mabaya yanayokukuta umwombee Nduguyo, rafiki yako au mfanyakazi mwenzio yamkute. Daima tuombeane mema ya mafanikio. Pale wewe ilipotelea na ukakosea, mjuze na mwenzio asijiingize huko.
Tusije tukawa kama mgonjwa wa Ukimwi anayeamua kuambukiza wengine kwa makusudi kwa dhana ya kuwa waangamie wengi.