Leo jumatatu, Septemba 11, 2023 nimemsikia Rais wa Tanzania akisema hivi;
1. Anadai wanaotaka katiba mpya hawajui ni vifungu gani vibadilishwe
2. Anadai katiba haiwezi kuleta maendeleo
3. Kwa kifupi anasema wanaoomba katiba mpya hawajui chochote kile
Je Rais kama kweli aliuliza watu wawili watatu kuhusu katiba, je watu hao wana upeo gani kuhusu katiba/Dunia, vipi kama waliogopa kumpa majibu sahihi kwa sababu machawa huogopa sana
NB
Uzi huu usiwekwe kwenye uzi mwingine, mimi nataka kupata tu maoni ya wananchi kuhusu swali langu hilo hapo juu, na sijaonesha dalili yoyote ya upande wangu wa kisiasa.