Je, Rais Magufuli Atagombea Urais 2020?

Je, Rais Magufuli Atagombea Urais 2020?

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
14,242
Reaction score
34,917
JE, MAGUFULI ATAGOMBEA URAIS 2020?

Mtawala anayevunja [HASHTAG]#Haki[/HASHTAG] na kuleta mdororo wa [HASHTAG]#Uchumi[/HASHTAG] hawezi kushinda Uchaguzi 2020.
-----------------------------------
Ni dhahiri kwamba Rais Magufuli hawezi kushinda Uchaguzi wa 2020 kama atagombea na kama ataendelea na sera zake za ukandamizaji wa haki na kutokuwa na umakini katika sera za kiuchumi, biashara na kodi. Atashindwa uchaguzi 2020! Atashindwa! Na ameshashindwa!

"JPM, Kama atagombea tena Urais mwaka 2020, hawezi kushinda kwenye uchaguzi ulio huru, haki na uwazi. Mhariri wa gazeti lililofungiwa hivi karibuni la Raia Mwema alipata pia kutanabaisha kwenye safu yake, kwamba uchaguzi wa mwaka 2020 utaamuliwa na ajenda mbili kuu za msingi, HAKI na UCHUMI" .

Kwa nini [HASHTAG]#Haki[/HASHTAG] na [HASHTAG]#Uchumi[/HASHTAG] ni mtihani kwa Magufuli?
-----------------------------------
Hapana shaka ya chembe kwamba utawala wa Magufuli unaongoza kwa kuvunja haki za watu kwa kiwango cha juu sana ambacho hatujawahi kukishuhudia huko nyuma katika nchi yetu.

Vilio na machozi ya wanaovunjiwa nyumba bila fidia ilhali kukiwa na zuio la mahakama, watu wanaouwawa hovyo na wengine kuokotwa kwenye fukwe za bahari utadhani ni samaki waliokufa kwa kukosa hewa, watu wanaoshambuliwa hovyo kwa kutoa mawazo yao tu dhidi ya Serikali, watu wanaoswekwa ndani kwenye magereza bila makosa, tabia ya visasi dhidi ya watu mbalimbali na wakosoaji wa sera zake, na uvunjifu wa haki nyingine za Kikatiba kama uhuru wa mawazo, kauli zinazovunja nguvu watumishi/wafanyakazi juu ya nyongeza ya ujira na stahiki zao nyingine, uhuru wa kukusanyika, uhuru wa kufanya shughuli za siasa, haki ya kupata Katiba mpya na Haki za Wazanzibari kutokana na sintofahamu ya uchaguzi wa Mwaka 2015.

Hayo pamoja na mambo mengine ni mifano michache tu inayoonesha ubinywaji wa haki kinyume kabisa na Katiba ya nchi yetu, Katiba ambayo Rais aliapa kuilinda.

Je, ni wananchi wa namna gani wanaweza kumchagua Rais wa namna hiyo endapo atagombea tena mwaka 2020? Bila shaka hakuna! Unabii utatimia!

[HASHTAG]#Uchumi[/HASHTAG] wetu una hali gani na unakwenda wapi?
-----------------------------
Licha ya takwimu kuonyesha kasi ya ukuaji wa uchumi kuwa kubwa kwa kiwango cha 7%, si jambo la kuficha kwamba wachumi wanajua kuwa shughuli za uchumi zimedora na kutia mashaka na hicho kiwango cha wastani wa 7% ni maendeleo ya sera za awamu ya nne ambayo sasa yanaanza kukatika.

Baadhi ya taarifa zinaonesha kuwa, tayari makadirio ya kasi ya ukuaji wa uchumi yameshushwa mpaka 6% mwaka 2017 na 5% mwaka 2018. Ikifika mwaka 2020 kasi ya ukuaji wa uchumi itakuwa karibu sawa na kasi ya ukuaji wa idadi ya watu (2%) na hapo ndio tutaona ongezeko la familia zinazolala bila kula, matumizi ya bidhaa kushuka na mdororo wa uchumi kushika kasi(Zitto Kabwe)

Hivi sasa hali ya maisha imekuwa ngumu kwa wananchi, mauzo ya bidhaa za viwanda nje kwaajili ya fedha za kigeni yameshuka kwa zaidi ya nusu, malipo yetu nje yamekuwa na urari hasi kwa sababu ya [HASHTAG]#Maamuzi[/HASHTAG] ya hovyo ya miradi mikubwa kama ndege na Reli (miradi muhimu iliyotekelezwa bila weledi wa maarifa ya uchumi wa dunia unavyoendeshwa).

Sekta ya Kilimo imeshuka mpaka kiwango cha kabla ya Uhuru, kwani kasi ya ukuaji wa sekta ya Kilimo mwaka 2016 ilikuwa 1.6% tu. Wakulima wa Korosho hawajapewa pembejeo, hivyo uzalishaji wa zao linalotuingia mapato ya Kigeni zaidi nchini utashuka msimu huu wa mavuno, Tumbaku (zao la pili Kwa kuingiza Fedha za kigeni) tayari wakulima wanalia, mazao ya choroko na kunde bei imeshuka kwa zaidi ya 500%, Pamba uzalishaji umeshuka Kwa 63% kati ya mwaka 2015 na 2017 (miaka miwili ya Magufuli), na mauzo Nje ya dhahabu kuanza kushuka kwa sababu mbalimbali na hivyo kupelekea shilingi kushuka thamani na hivyo mfumuko wa bei kupanda kwa kasi.

Kutokana na shughuli za Uchumi kudorora, Mapato ya Serikali kwa mwezi yameanza kushuka kufikia chini ya makusanyo aliyoacha Rais wa Awamu ya Nne.

Je, mtu anayeangusha uchumi kwa kasi ya "jet" ya namna hiyo anawezaje kuchaguliwa tena na Watanzania kuwa Rais?

Tatizo kubwa la utawala wa awamu ya tano ni kuamini kwamba maamuzi ya 'kibabe' yasiyozingatia haki, sera za kiuchumi, biashara na kodi yanaweza kulinusuru taifa hili, huko ni kukosa weledi katika mambo haya, ni kujifunga kitambaa cheusi usoni!

Mtawala yeyote anayetumia ghiriba kwa kutaja kila mara kwamba yupo kwa ajili ya wanyonge ilhali wanyonge hao ndio wanaoendelea kuathirika kwa kasi ya ajabu, ni wa kumuogopa, ni kushindwa katika uchaguzi! Ninadhani sasa wanyonge hawa wanamuelewa kweli kweli!

Nimetimiza wajibu.

[HASHTAG]#TuendeleeKumwambiaUkweli[/HASHTAG]

[HASHTAG]#PrayforTunduLissu[/HASHTAG]

2017 October 7

N:B Swali la Kizushi: "WATU WASIOJULIKANA NDIO WALE WATU WA NCHI JIRANI WALIOINGIA NA KWENDA DODOMA KWA KAZI MAALUM?"
 
MDINI MKABILA MCHUKI NA ZAIDI NI MZADIKI


Mungu shusha maono.


Swissme
 
Tatizo sio kushindwa bali kushindwa na nani?
 
Anafanya hivi kwa sababu hana haja ya kugombea tena 2020."he has nothing to loose in 2020".Hapendi kupata kura za wafanyakazi wa Tanzania
 
Natamani kila mtanzania aweze kufaham kuwa kwa sasa miongon mwa watu wanaoweza kuimudu vizur nchi hii kiuongoz ni 'Zitto Zuber Kabwe'
 
Je, ni wananchi wa namna gani wanaweza kumchagua Rais wa namna hiyo endapo atagombea tena mwaka 2020? Bila shaka hakuna! Unabii utatimia!
Nimeku quote pale ila ujue kushinda ni lazima sababu wapiga kura wengi si wafanya kazi, siyo wasomi, hawajui kama kuna upinzani, walishaaminishwa kuwa ukichagua upinzani unaleta vita kama vile vya Rwanda kama kimama kimoja cha CCM kilivyowatishia wana Bukoba Mjini baadaye upinzani ukashinda. Mikoa iliyonyuma kielimu na kimaendeleo lazima watachagua CCM na hata wasipoichagua, yatakuwa yale yale ya siku zote.
 
Wafanyabiashara na watumishi wa umma wasidanganyike,wamnyooshe kwa debe come 2020
 
Unahisi hawa watu 2000 wa humu jf ndio watasababisha asishinde simuoni mpaka sasa wa kushindana nae!
 
Natabiri Magufuli atavunja zaidi haki, kuangusha zaidi uchumi na kuiba kura kushinda uchaguzi.
 
Back
Top Bottom