Tripper
JF-Expert Member
- Nov 15, 2020
- 803
- 1,638
Mwaka jana, Korea Kaskazini ilishutumiwa kwa kufanya mashambulizi ya kimtandao dhidi ya majukwaa ya biashara ya sarafu za kidijitali (cryptocurrency) na kuiba mabilioni ya dola. Mwaka huu, imeshutumiwa tena kwa kufanya wizi mwingine mkubwa wa fedha za kidijitali, ambao unaripotiwa kuhusisha Binance na kiasi cha dola bilioni 6. HACKERS watatu ambao wamehusika kwenye matukio hayo wameshajulikana sura zao na tayari ishathibitishwa serikali ya Kim ipo nyuma yao. Halafu mbaya zaidi Kim kaambiwa kuhusu hilo tukio akajibu kwa kurusha makombola ya masafa marefu tu. Hii inaonesha jamaa alivyo hapendi amani.
Hata hivyo, hatujaona kiwango kilekile cha vitisho vya hadharani, kauli kali za uchokozi au mazungumzo kuhusu kutuma vikosi vya kijeshi nchini Korea Kaskazini ili kumkamata Kim Jong Un kupitia FBI.
Kwa nini Marekani na FBI hazionyeshi msimamo mkali kama huo dhidi ya Korea Kaskazini? Kwa nini kila kunapotokea matatizo barani Afrika au katika nchi nyingine, Marekani huwa ya kwanza kuonyesha nguvu zake za kijeshi na kisiasa, lakini inapofika kwa Korea Kaskazini, ghafla mtazamo wake hubadilika?
Je, ni kwa sababu Korea Kaskazini ina nguvu zaidi na ina silaha za nyuklia, au ni kwa sababu madhara ya kukabiliana moja kwa moja na Kim Jong Un ni makubwa zaidi?
Swali linabaki pale pale: Kwa nini msimamo huo huo mkali hautumiki kwa nchi zote?
VIVA LISU.