Je niko sawa katika hili?

Deva

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Posts
1,237
Reaction score
1,819
Habari za mida hii wakuu.

Mimi ni kijana wa miaka 24

Nipo chuo nasomea masomo ya afya Mwaka wa tatu ambao ni wa mwisho.

Katika mawazo yangu ninawaza kuoa mwanamke mara tu nitakapo maliza masomo yangu mwaka kesho hii kwa lengo la kupata mtoto, maana naona kuwa sitaweza kuzaa na mwanamke nje ya ndoa.

Je ni kwanini nimefikia kuamua kuoa?

Nimefikia maamuzi ya kuoa baada ya kumpoteza mwanangu wa pekee( Hii story nimeshaileta humu jinsi alivyouawa).

Sasa najiona mpweke sana kiasi kwamba sioni kama nitaweza kukaa muda mrefu bila kuwa na mtoto (naomba kudeclare interest kuwa ninapenda watoto na wala sijawahi kukataa mimba, kwangu mimi mtoto ni pendekezo namba moja kwenye maisha yangu).

Sasa ninahisi njia pekee itakayonipa faraja ya maisha ni kupata mwanamke ambaye atakuwa wangu wa maisha na kunizalia watoto.

Najua humu kuna watu wazima wenye busara za kutosha mmepitia mambo mengi yenye kuwapa ujuzi , naomba mnipe ushauri katika suala hili.

Asanteni.
 
Mimi naamini kwamba ni maamuzi yako tu wewe mwenyewe na ninavyojua mm Mapenzi hayana mshauri bali ni wewe mwenyewe kujiongeza.

Na kwa kuwa umesema upo chuo mwaka wa 3 naamini hapo chuo kuna wasichana wengi wazuli wa kila muonekano ivyo ni wewe tu kuangalia chuguo lako na kufanya maamuzi

Ni hayo tu .....
 
Uko sawa mkuu.

Nitapepesa macho.
 
Mkuu hebu tusaidiane kimawazo, ni reason zipi zaweza kuwa right.

Karibu tushee experience mkuu

I admit losing a child is hard. Lakini think things through first.

Find yourself a good woman, unaempenda and move on from there. It might take you a while kumpata, inaweza ikawa longer than the timeframe uliojiwekea lakini in the end ukawasatisfied na utakaempata na ukaishi maisha ya ndoa ya furaha.

Lakini ukisema unaoa tu kisa unapenda watoto, mbona hata kesho tu its possible. Ni kumtafuta any woman ambae anahaja ya ndoa na kuanza process za ndoa. Lakini in the end you'll never be happy kwasababu target yako ni kupata watoto tu. Trust me you'll never love that woman, kwasababu atakuwa sio focus yako. Yeye yuko pale kwaajili ya kukuzalia tu, to put it bluntly. Na hii inaweza ikaleta mtafaruku baadae.

Watoto ni byproduct ya a good loving relationship(most of the time). You gotta love the hen first kabla yakuanza kufurahia mayai yake.
 
You are very bright mkuu.

Thats why i shared my story here najua nitakutana na watu wa namna yako wenye kunipa mawazo zaidi.

Binafsi nimelenga baada ya kumaliza chuo nianze process hizo japo ninajua ninaweza nisifikie lengo hilo nililojiwekea kwa muda huo maana pia ninaangalia ni mwanamke gani wa kuzaa, nae nijihakikishie kuwa hataniletea shida na nimempenda kweli.

Ninahitaji kuweka umakini sana kwenye mwanamke nitakayekuwa nae na hii itanichukua muda kidogo zaidi ya muda niliojiwekea.
 
Nimekielewa ulichokiandika mkuu
 
Kama umempata wa kufanana na wewe oa tu mkuu, ila ukilazimisha ndoa itakusuta baadae
 
Kama umempata wa kufanana na wewe oa tu mkuu, ila ukilazimisha ndoa itakusuta baadae
Duuh itanisuta vipi mkuu

Hebu nisaidie isije kunisuta mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…