Je, ni sawa DSTV pekee kupewa uhalali kuonyesha CNN?

Je, ni sawa DSTV pekee kupewa uhalali kuonyesha CNN?

Mzalendo_Mkweli

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2012
Posts
2,056
Reaction score
1,303
Habari ndg wa JF,

Mimi natumia king'amuzi ambamo mojawapo ya channel iliyokuwepo ni CNN. Kuanzia mwezi huu channel ya CNN haionyeshwi tena katika hicho Kingámuzi na badala yake wameweka channel iitwayo France International.

Nilipowasiliana na wahusika waliniambia kuwa DSTV wamepewa exclusive Right ya kuonyesha CNN katika ukandaa huu ambapo mimi nimetilia shaka majibu haya. Naomba kuwauliza ndugu mnaotumia Digtech, Continental, Zuku, Startimes nk je hakuna King'amuzi chochote kinachoonyesha CNN?

Kwa wale mlio na ufahamu wa mambo haya ya mawasiliano, Je ni sahihi DSTV kuwa na Exclusive Right ya kuonyesha channel Fulani e.g. BBC, CNN, Aljazeera etc AU hawa wahusika wa hiki King'amuzi wamekwepa ghrama na kwamba hapa wanatumia uongo kuficha huo ukweli?

Nawasilisha.
 
kwa nchini kwetu nina uhakika na CNN ipo kwenye Dstv pekee sijui kwa nini ila karibu ving'amuz vingi haipo kabisa sina uhakiki TING
 
acha waje wenyewe, wengine sisi ni watizamaji tu.
 
Ukitaka kizuri lazima ukubali kutoa
 
Kwani TCRA si wapo humu?
Watupe majibu hata yaliyo shallow tutaelewa tu
 
Last edited by a moderator:
Kwani TCRA si wapo humu?
Watupe majibu hata yaliyo shallow tutaelewa tu
TCRA ni moja ya taasisi zenye kuhojiwa mambo mengi sana katika wakati huu wa matumizi makubwa ya mitandao. Umefika wakati nao wawe na dawati lao humu JF kwa ajili ya kujibu maswali yanayowatatizo wananchi kama walivyo VODA, NMB, STARTIME nk.
Kwa ulimwengu wa sasa mitandao linatoa suluhisho na majibu ya maswali madogomadogo kwa wakati kuliko Press release.

cc. Invisible . Jee hamuwezi kuarrange jambo hili na kuwapa maombi haya?
 
Last edited by a moderator:
DSTV majanga vifurushi vimepanda being ile mbaya, juzi nimelipa 80,000. Roho inauma
 
kwa nchini kwetu nina uhakika na CNN ipo kwenye Dstv pekee sijui kwa nini ila karibu ving'amuz vingi haipo kabisa sina uhakiki TING

Ni kweli CNN ilikuwepo Ting. Je hao channel 10 mbona nao wamekataa kuwepo ktk King'amuzi cha Ting?
 
Mimi naangalia cnn usiku wakati itv wamejiunganao...alafu kiswahili chako kinamapungufu kwenye title,ulitakiwa kutumia neno "kuonesha" ....naunga mkonyo hoja!
 
Mimi naangalia cnn usiku wakati itv wamejiunganao...alafu kiswahili chako kinamapungufu kwenye title,ulitakiwa kutumia neno "kuonesha" ....naunga mkonyo hoja!
Kiswahili chako pia kina utata ulitakiwa kutumia neno ''Mkono''
 
TCRA ni moja ya taasisi zenye kuhojiwa mambo mengi sana katika wakati huu wa matumizi makubwa ya mitandao. Umefika wakati nao wawe na dawati lao humu JF kwa ajili ya kujibu maswali yanayowatatizo wananchi kama walivyo VODA, NMB, STARTIME nk.
Kwa ulimwengu wa sasa mitandao linatoa suluhisho na majibu ya maswali madogomadogo kwa wakati kuliko Press release.

cc. Invisible . Jee hamuwezi kuarrange jambo hili na kuwapa maombi haya?

Wana account humu bila shaka na wanasoma post zote just to check if all goes well.
 
Back
Top Bottom