Je ni sahihi siku ya wanawake duniani kutumika kuwananga wanaume?

sonaderm

JF-Expert Member
Nov 9, 2015
618
1,816
Leo ni siku ya wanawake duniani..Hongereni akina mama na wananawake kwa siku hii muhimu!

Kero yangu ni moja tu, kauli mbiu ya siku hii ambayo nimeisikia ni wanawake kuwa nguzo ya uchumi..Cha ajabu kila redio ninayofungua ni story za akina mama kuwasema wanaume kuhusiana na manyanyaso ya kila aina waliyopitia, kifupi ni kuwa wanazungumzia negative mindset kuhusu wanaume na kusahau kauli mbiu ya jambo lenyewe..

Je, ni sahihi kwa siku hii kutumika kuongelea personal issues za akina mama kuhusu wanaume?Kila baya la mwanaume linasemwa leo wakati naamini wapo wanaume wanaonyanyaswa pia ila hakuna wa kulizungumza hadharani kutokana na tamaduni yetu..

Kauli mbiu imepigwa kapuni na sasa imekuwa siku ya wanawake kutoa ya moyoni kuhusu wanaume..kila baya la mwanaume litasemwa leo..Ni sawa?
 
Back
Top Bottom