Je, ni sahihi Mbalawa kubaki?

pasii

Member
Nov 13, 2015
20
3
Je, ni sahihi Mbalawa kubaki?
Nimekuwa nikitafakari na kufuatilia jinsi serikali ya Jemedari wetu Dr. John Pombe Joseph Magufuli inavyofanya kazi, kwa weredi na ufanisi mkubwa sana. Mtanzania yeyote ambaye ni mzalendo hawezi kupuuza wala kuacha kufurahia na kuunga mkono juhudi hizi.

Lakini Mimi nimejikita zaidi kwenye hili suala la hivi karibuni linaloihusu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, chini ya Professor Mbalawa, hasa kwenye kitengo cha KOJ, ambayo vigogo wake huko wametumbuliwa majipu.
Leo nachelea kusema nina wasiwasi na utendaji wa baadhi ya mawaziri wa Magufuli, kwani haiwezekani kabisa waziri Mkuu anakuja kutumbua jipu ambalo lipo kwenye kitengo cha waziri huku waziri husika akiwa alikaa kimya na hakuona uozo kama huu. Mimi ninafananisha hili jambo na mtu mzima aliyeoa ambaye ameshindwa kuona jipu lililo kwenye makalio ya mke wake, mpaka Baba mtu anakuja kuliona na kulikamua.
Hivi Mhe. Mbalawa alikuwa wapi kuona ujinga juu uliokuwa unafanyika wa kuchepusha mafuta? Je, ilikuwa ni lazima Waziri Mkuu aje ashughulikie hilo suala? Au ndio mfumo mpya wa utendaji kazi wa serikali hii? Ambayo waziri hatakuwa na mamlaka ya kufanya chochote kwenye wizara mpaka aje Mhe. Majaliwa au Rais Mwenyewe? Je tunatakiwa kuamini kuwa Mbalawa ni dhaifu? Na kama ni hivyo je, anauhalali wa kuendelea kuwepo kwenye wizara nyeti kama hiyo?
Ikiwa huu ni mfumo tutakoendelea nao ambao kila kitu itakuwa ni lazima afanye waziri Mkuu au Rais, sidhani kama kwa mtindo huo tutafika. Kwa namna hii kama ndio itakuwa ni jadi Taifa halitafikia malengo yake.
 
Nchi ya takwimu hii. Hakuna la ziada ni fukuza huyu simamisha yule kwa uchunguzi. Badala ya kufanya maendeleo tumeachwa huko kushabikia. Kama wao wanaamini wafanyakazi wote wa umma ni wezi na hawana maadili awafukuze Nazi aajiri wapya!. Siku 101 ni kutumbua majipu tu. Hii si sawa. Afanye maamuzi magumu yatakayolisukuma taifa mbele. Na kiini cha haya yote ni kuchokwa kwa chama tawala kwani wananchi hawaamini kama kinaweza kuwaletea maendeleo zaidi ya vitisho. Nimejaribu kuwaza kwa sauti kubwa kuona ilipo shida.
 
Back
Top Bottom