ki2c
JF-Expert Member
- Jan 17, 2016
- 7,496
- 13,973
Juzi nilimwazima mwenzangu pikipiki aende akapate chakula mgahawani,ile pikipiki ilikua haijalipiwa bima.Alipofika yule jamaa yangu akapaki nje kidogo ya mgahawa,karibu na kituo cha bodaboda,akaenda kupata chakula,alivyorudi akakuta pikipiki haipo,kuulizia watu waliokuwepo maeneo yale,wakasema pikipiki yako imebebwa na polisi wale wanaoitwa 'TIGO',akauliza wameibebaje wakati funguo ninazo,akaambiwa wamekata nyaya wakaziunganisha wakaondoka nayo.
Mimi nikapewa taarifa nikaenda polisi kuifuata hiyo pikipiki,nilipofika kuhoji kwanini pikipiki yangu ibebwe bila ya idhini ya niliyempatia pikipiki ambaye angetoa funguo ioondoke kwa utaratibu,nikajibiwa kua huo ndiyo utaratibu wao wakuchukua vyombo vya moto ambavyo vinakua na makosa halafu wenyewe wanakua hawapo eneo la tukio.
Mimi kuokoa muda,nikalipa faini Tsh.30,000/= nikaichukua pikipiki,ila moyoni nikabaki nina wasiwasi juu ya njia waliyotumia kuikamata pikipiki yangu.
Naomba kuuliza kuhusu hicho kitendo cha hao polisi kukamata pikipiki yangu,walifuata taratibu zinazokubalika kisheria au walikiuka.
Nawasilisha.