Je ni sahihi kumlaumu atakaye kujiajiri kisa kachelewa kufanya hivyo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je ni sahihi kumlaumu atakaye kujiajiri kisa kachelewa kufanya hivyo?

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by Stigliz, Oct 28, 2011.

 1. S

  Stigliz Member

  #1
  Oct 28, 2011
  Joined: Aug 9, 2011
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Elimu ya tanzania kimsingi haituandai kuwa waajiri bali waajiriwa.Ukweli unajidhihirisha ktk mitaala mpaka ya chuo.Mimi mtoto wa mkulima wa kijijini tena kabila la Lowasa nilipitia mlimani<udsm> na kumaliza salama.Awali ckuwa na wazo la kujiajiri,nimelipata sasa.Taabu iliyo mbeleni ni watu kuanza maneno ya kukatishana tamaa mwanzo wa safari!Nimechoka kuomba msaada na kuzunguka na bahasha za kaki kila ofisi huku masekretari wakitoa majibu machafu pasi kujua sie pia watafutaji. NAOMBA MAWAZO YAKINIFU YENYE MASHIKO yatakayo nifikisha ktk maisha bora na c bora maisha. NAWASILISHA!
   
 2. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #2
  Oct 28, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,601
  Likes Received: 18,611
  Trophy Points: 280
  Stigliz, wewe unamatatizo, mwanzo nilidhani ni ugeni wako humu?. Sikukatishi tamaa bali nakusisitiza lazima ujipange, kama hata hujijui unataka nini na wala hujijui unaweza nini, then usaidiweje!. Hatua ya kwanza jitambue unataka nini, pili jipime unaweza nini ukishajua, jipange kuanza utekelezaji!.

  Kuna wengi wana matatizo kama yako bila wao kujijua they are problem themselves. Kwa fani ya bussiness mbona kazi bwelele?, kusoma UDSM sio tija, nimesimamia usaili wa kazi fulani, waliomba mpaka watu wenye masters na hizo barua zao za kuomba kazi zilikuwa utumbo mtupu!.

  Hebu angalia uliomaliza nao wako wapi na wewe uko wapi?, kwani hao huko walipo wananini ambacho wewe hauna?. Wake up boy!
   
 3. prakatatumba

  prakatatumba JF-Expert Member

  #3
  Oct 28, 2011
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 1,337
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Umesomea nini?
   
 4. S

  Stigliz Member

  #4
  Oct 28, 2011
  Joined: Aug 9, 2011
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nataraji kuanza biashara ya vyakula eneo la chuo,hapa dsm,nimeanza kujifunza uchomaji nyama za foil,uandaaji wa salad na lugha za biashara.Baadae nikikuwa kimtaji nielekeze nguvu kwenye biashara ya nafaka.
   
 5. S

  Stigliz Member

  #5
  Oct 28, 2011
  Joined: Aug 9, 2011
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Uchumi!UDSM!
   
Loading...