Je ni sahihi kumfunga aliyempa ujauzito mwanao?

reyzzap

JF-Expert Member
Oct 3, 2014
6,796
21,702
Mwanao ni mwanafunzi let say secondary ulipanga asome afike mbali sana kielimu, kwa bahati mbaya kapewa mimba haijalishi alipanga au ni bahati mbaya na mtu aliempa hio mimba walikubaliana ku sex (HAKUBAKWA) na wote wamekiri wapo willing kuish pamoja, kijana anakubali kumlea mtoto na mama.

Sasa sheria inasema anatakiwa afungwe miaka 30 no matter how, ila let say kwa mfano wewe una uamuzi wa afungwe au aachwe. Kipi utachagua?
 
Kama hii Sheria ingekuwa inafatwa dah wengi wangefungwa.

Nadhani wakati umebadilika na maisha yamebadilika kuna wakati ukifata Sheria unaweza ukawa unaharibu mambo kuliko kujenga.

Cha msingi Ni kuangalia alternative tuu baada ya kujifungua atasoma vp sambamba na kupata ushirikiano from upande mwingine wa me.
 
Mambo mengi ya kifamilia hua yanamalizwa kwa hekima, busara na mazungumzo.
Kumbuka huyo kijana tayari amesha kua mzazi mwenza wa Binti yako, sasa hapo ukitumia zajba unaweza Fanya maamuzi ambayo yatajenga chuki ya milele kati yako na binti yako, pia mtoto wao ambae ni mjukuu wako.
Sio kila jambo linamalizwa eti kwakua sheria inasema hivyo
 
Sikiliza nikuambie. Ukimfunga kijana unapata faida gani?? Mjukuu anazaliwa, akae miaka 30, atakuwa amemaliza chuo kikuu na kazi kishafanya miaka isopungua 5. Halafu ghafla, anajiwa na kizee kilicho choka kutoka kifungoni na kinamuomba msaada wa kibarua chochote ili kiweze kidhi haja ya mlo wa siku. Aambiwe huyu ndo babako alifungwa kwa sababu alikuzaa wewe.
Sidhani kama mjukuu atakusamehe. Pia kwetu wanasemaga; Mpera huzaa mpera na wengine wanasema; Mwana wa ifolong'o ni ifolong'o. Je naye akija fanya hivyo, akafungwa akutane na babake jela wadhani ni nini kitatokea.
Hakumbaka, waliridhiana, waache waendelee kuridhiana walee tunda la maridhiano yao.
 
Kama walikubaliana si uwaache, muhimu kuhimiza ajifungue na kuendelea na masomo. Mtoto huyu baba yake kifungwa utasaidia kumlea na kumpeleka jela kumsalimu kila siku!?
 
Hapo piga tu hesabu za kawaida. Ukimfunga utapata faida gani? Kama wameelewana then ni bora ukawaacha wajenge familia maana huwezi kumlazimisha ng'ombe kunywa maji.
 
kati yenu mlojibu kuna mwenye mwana wa kike. Acheni kabisa kujibu kilevi ( samahanini kwa matusi wadau). Mtoto anasoma kazi yake ni kusoma full stop, akipata mimba haijalishi ya mwanafunzi mwenzie au mtu mzima, haijalishi walifanya kwa utashi wai au la. Mimi kama mzazi, huyo mwanume nitampeleka polisi baada ya kumuhanisi kwanza, nakipigo cha haja atasomea mashtaka akiwa amelazwa ICU. Na kwa gharama yoyote hitahakikisha anakula miaka 45, na kesi ya kutembea na mwanafunzi haina msamaha wa raisi. Na nitahakikisha maisha yake huko jela yatakuwa jehanamu ndogo na wala hatamaliza hata miaka mitano hai.
 
Si kila anayekosa anapaswa kwenda kisongo, jukumu la mzazi ni kumlea mtoto na kuhakikisha anakua kiroho, kielimu na kimwili. Kosa kama hilo litokeapo, tusikimbilie kutoa hukumu za fatiki bali tuangalie ni namna gani tutasuluhisha tatizo kwa manufaa ya wote. Kuna wazazi wengi hawatimizi majukumu yao ama kwa kutokujua ama umasikini.
 
Pumbavu kabisa, kati yenu mlojibu kuna mwenye mwana wa kike. Acheni kabisa kujibu kilevi ( samahanini kwa matusi wadau). Mtoto anasoma kazi yake ni kusoma full stop, akipata mimba haijalishi ya mwanafunzi mwenzie au mtu mzima, haijalishi walifanya kwa utashi wai au la. Mimi kama mzazi, huyo mwanume nitampeleka polisi baada ya kumuhanisi kwanza, nakipigo cha haja atasomea mashtaka akiwa amelazwa ICU. Na kwa gharama yoyote hitahakikisha anakula miaka 45, na kesi ya kutembea na mwanafunzi haina msamaha wa raisi. Na nitahakikisha maisha yake huko jela yatakuwa jehanamu ndogo na wala hatamaliza hata miaka mitano hai.
Ufanye hivo ukiwa huna mtoto wa kiume wala mdogo wa kiume wala hutegemei kupata mjukuu wa kiume.
Kama ni adhabu wote wapewe..tena usikute mtoto wa kike ndo alijitongozesha.
 
Sikiliza nikuambie. Ukimfunga kijana unapata faida gani?? Mjukuu anazaliwa, akae miaka 30, atakuwa amemaliza chuo kikuu na kazi kishafanya miaka isopungua 5. Halafu ghafla, anajiwa na kizee kilicho choka kutoka kifungoni na kinamuomba msaada wa kibarua chochote ili kiweze kidhi haja ya mlo wa siku. Aambiwe huyu ndo babako alifungwa kwa sababu alikuzaa wewe.
Sidhani kama mjukuu atakusamehe. Pia kwetu wanasemaga; Mpera huzaa mpera na wengine wanasema; Mwana wa ifolong'o ni ifolong'o. Je naye akija fanya hivyo, akafungwa akutane na babake jela wadhani ni nini kitatokea.
Hakumbaka, waliridhiana, waache waendelee kuridhiana walee tunda la maridhiano yao.
Umeongea mkuu, iko hv kuna dg hapa jiran amerud pasaka kwa siku km nne hv, yupo form six, wazazi walishtuka km anatoka na mshkaj flan, wakaamua alivyorud wamchek ujauzito kiutan utan wakamkuta na ujauzito wa miez minne,

Asa inshu ipo hiv mzee anakazania jamaa anyee ndoo.
Mama na dg wanaomba yaishe kwenye familia,

Ila shule haijulikan inshu yyt, Kesho anatakiwa aondoke arud shule muafaka haujaafikiwa.
Ni majiran zetu wa karb Mshua wake akaja kuomba ushaur kwa mzee, digi nae sijui n pombe imefika kweny utosi Anasema huyo n wa kufunga tuu. sasa nashindwa kuelewa halmashaur za vichwa vyao.
 
Pumbavu kabisa, kati yenu mlojibu kuna mwenye mwana wa kike. Acheni kabisa kujibu kilevi ( samahanini kwa matusi wadau). Mtoto anasoma kazi yake ni kusoma full stop, akipata mimba haijalishi ya mwanafunzi mwenzie au mtu mzima, haijalishi walifanya kwa utashi wai au la. Mimi kama mzazi, huyo mwanume nitampeleka polisi baada ya kumuhanisi kwanza, nakipigo cha haja atasomea mashtaka akiwa amelazwa ICU. Na kwa gharama yoyote hitahakikisha anakula miaka 45, na kesi ya kutembea na mwanafunzi haina msamaha wa raisi. Na nitahakikisha maisha yake huko jela yatakuwa jehanamu ndogo na wala hatamaliza hata miaka mitano hai.
, wewe nahic ungempeleka selo usiku huo huoo, ila kumbuka ukilisanua tuu na shule wakajua bas ten masomo hana , na 4m6 wanamaliza mwez wa tano katkat kbsa
 
sioni umuhimu wa kumfunga, zaidi una jenga chuki kati ya familia yako na anayotoka baba wa mjukuu wako

mbaya zaidi kwa miaka 30 hiyo wewe ndo utamuhudumia mjukuu huku mama yake (mwanao) akihangaika

akili za kufunga, kutoa mimba za watoto wao wanazo wazee wanaojifanya watu wa hekima na busara na tendo ilo anaona kama limewachafua

vizee vinavyo jitia busara, hekima na heshima kwenye jamii vina mambo ya kikuda kweli
 
Ufanye hivo ukiwa huna mtoto wa kiume wala mdogo wa kiume wala hutegemei kupata mjukuu wa kiume.
Kama ni adhabu wote wapewe..tena usikute mtoto wa kike ndo alijitongozesha.
I dont care, zawadi ni miaka 45 yenye mateso na shida. akiweza maliza miaka mitano yeye mwanaume wa shoka.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom