Iselamagazi
JF-Expert Member
- Sep 26, 2011
- 6,083
- 6,234
Kwa miaka mingi kumekuwa na
dhana ya Wahehe kula mbwa,wapo waliogoma kula nyama ktk naeneo ya mkoa
wa Iringa kwa hofu ya kula nyama ya mbwa,Wapo waliooa au kuolewa na
wahehe,na walipofika ukweni wakagoma katakata kula nyama,hata walipoona
mbuzi akichinjwa live,ni bahati nzuri au mbaya hata wahehe wenyewe
huona fahari kuitwa wala mbwa,sbb kwao ni utani,na wao hawajachukua
juhudi zozote za kuuweka wazi ulaji wao wa mbwa.
Wahehe si mila yao kula mbwa,haijawahi kutokea...japo watani wa
wahehe uwahusisha wahehe na ulaji wa mbwa,Mtani wa mhehe ni Mngoni na
Mmanda si Mnyakyusa wala Mbena kama wengine wanavyodhani.Hutaniana ktk
misiba na harusi,utani wao huenda mbali kama kumwagiana maji,kuwaanika
wafiwa juani mpaka kiasi fulani cha pesa kitolewe ambacho huchangia
shughuli za msiba,hupakana unga au majivu kama sehemu ya utani.Wapo
ambao hunyang'anywa viatu au kanga ili watoe pesa,lengo la utani ni
kuwafariji wafiwa,kuchangamsha eneo la msiba lisigubikwe na wimbi la
majonzi na wakati mwingine kuburudisha.
Wahehe chakula chao kikubwa ni ugali wa kiwerege,nyama na
matofu(viazi mviringo),hakuna wazee wapenda nyama kama wazee wa zamani
wa kihehe,wakati wa kula ilikuwa ni kosa sana kwa mtoto kuanza kuchukua
nyama kabla ya mzee,na wakati mwingine mzee ndio alikuwa na jukumu la
kukuchagulia nyama ya kula,kwa kuitoa ktk mchuzi na kuinyonya ndio
akupe.Kinywaji chao kikuu ni pombe ya ulanzi na komoni...haikuwahi
kutokea mhehe kufuga mbwa kama kitoweo.
Mbwa hufugwa kama mlinzi na msaidizi machungoni,wahehe wana miiko ktk
vyakula(lusilo) kulingana na ukoo,wapo wasiokula
kanga(ndege),bandama,nyopolwa(ndama),moyo wa ng`ombe,firigisi n.k n.k!!
Ktk maisha yao ya kijamii wahehe huwatenga watoto wa kike na wa
kiume,baba hukaa mbali na watoto wa kike,haikutokea watoto kujua au
kuchangia choo na baba,wala watoto walikuwa hawajui kama baba huenda
chooni,baba akijisikia haja,hubeba kajembe kake na kupiga mruzi kuita
mbwa wake na kutokomea porini...hali hii iliwafanya watoto waamini
wakubwa hasa baba haendagi chooni wala kujisikia kupumua,ndio maana
wahehe wana msemo wanasema mvina siafula= mkubwa hajambi(asha kumu si
matusi
Kwa asili wahehe hawataili,si mila yao kwenda jando,baadae baada ya
muingiliano na wamisionari ndio wakaanza kutahiri,huoa mitala,ni fahari
kuwa na wake zaidi ya mmoja.Ni wakulima wazuri ktk kipindi chote cha
mwaka...nyakati za kiangazi hulima ktk finyungu mazao ya
mbogamboga.Wameathiriwa na dini ya kikristo ktk dhehebu la Katoliki,na
hasa baada ya ujio wa wamisionari wa Benedictin ktk maeneo ya
Tosamaganga,na baadae ujio wa wamusionari wa Consolata.Uislamu kwa asili
upo ktk eneo Kalenga na Pawaga, na maeneo ya Pawaga lilifikiwa na
Waarabu kutokana na uwindaji wa Pembe za Ndovu kandokando ya iliyokuja
baadae kuwa mbuga ya Ruaha...si ajabu wahehe waislamu wengi hutoka
maeneo haya.
Eneo la Uhehe ndio liliokuwa tishio kivita,liliwatisha wavamizi wa
kigeni na wenyeji..'uzuri wa jeshi la kihehe analijua kiongozi wa
wasangu na wabena,kutoka nje adhabu aliyoipata Jemedari wa kijerumani
Zelewisky kwa kuuwawa na askari wa kihehe imebaki mpaka kesho ktk vitabu
vya historia vya Wajerumani.
Wanawake wa kihehe ni wachapakazi,wachamungu na waadilifu
sana,wameumbwa na utii na hofu kwa wanaume,sio wahuni lkn wana huruma
kila waombwapo...wao huamini ktk hofu ya Mungu,ndio mana ukiwaomba
watakujibu vee niangusage elaa ulyee,isambi sa kwako....yaani we
niangushage ule,zambi za kwako.Ni wachapakazi ndio maana wadada wengi wa
ndani hutoka Iringa.Tatizo lao ni hasira,wana hasira sana...ukimuuzi
hataki tabu,anakuachia dunia kwa kujinyonga ili wewe uishi kwa amani.
Wana uwezo wa kuongoza lkn si hawana spirit ya ubepari,i.e
aggressive in investment,lkn wakipata mtu wa kuwaongoza ni wasimamiaji
na watekelezaji wazuri sana ktk uwekezaji.
Tatizo lao ni pombe,kukuta muhehe hanywi ni nadra sana,kukuta hana
hasira ni nadra,lkn wanajua kupenda na kumjali mwanamke,ni wasiri
sana,yamkini hufaa ktk kazi za kishushushu.Hawapendi kunyanyasika au
kuona mtu ananyanyaswa,mfano wa Mwamwindi kwa Mkuu wa mkoa Dr.Wilbert
Kleruu inaeleza jinsi wasivyopenda kuonewa,makofi aliyokula mkuu wa mkoa
Said S. Shamshama akiwa jukwaani toka kwa mzee wa kihehe miaka ya
1960's baada ya kuwadhihaki ni alama halisi ya hawa watu kuikataa
dharau,si ajabu ktk muitikio wa mfumo wa vyama vingi wahehe walikuwa ni
moja ya mkoa uliopokea mabadiliko kwa kumpa ushindi mbunge wa Upinzani.
Wahehe wana kiburi,wao huita kidada,hawapendi kujipendekeza hata
kama hawana kitu...wao hutumia msemo wa ndimgaya sidaa,hata kama hana
mia mfukoni ni mara chache kijishusha.
Asante mkuu barafu!
Last edited by a moderator: