Je, ni kweli wafuasi wa CHADEMA wanapendana?

Frey Cosseny

JF-Expert Member
Feb 4, 2015
1,984
1,405
Nimekuwa nikiona baadhi ya wanaccm Wakidai kuwa CCM hatupendani tofauti na wafuasi wa chadema ambao hata viongozi wao wakikosea wanaungana kuwatetea Makosa yao.Hii dhana inawezekana Isiwe sahihi au inatamkwa na wanaccm wasiyojua falsafa ya Chama Cha Mapinduzi na pia kutokujua tofauti ya kisiasa Kati ya chadema na Chama Cha Mapinduzi.

Moja ya sifa ya ccm ni kuwa Chama Chetu kina Hazina ya viongozi na wanachama wenye Upeo na ueledi mkubwa kuliko vyama vingi sana barani Africa.Chama Cha Mapinduzi kina Hazina ya machapisho na vitabu kedekede inayowasaidia viongozi na wanachama wake kufafanua falsafa, sera na itikadi ya Chama Chetu.

Chama Cha Mapinduzi ni Chama makini kinachoamini juu ya demokrasia ya wazi iliyobebwa katika itikadi ya Ujamaa na kujitegemea. Ccm inaamini katika Ujamaa wa kiafrika y'a kushirikiana ktk shida na raha bila kubaguana kijinsia kiumri wala kWA madaraka mtu aliyonayo, ndiyo maana ktk ccm Tunaamini kuwa cheo ni dhamana.

Sasa Nirudi kwenye suala la tofauti yetu na chadema na kwanini chadema wao hawana uwezo wa kuwakosoa viongozi wao hata pale wanapokosea.Kwanza itambulike kuwa chadema hawana falsafa ya miiko ya viongozi Ndiyo maana kwao mtu mkorofi asiye na maadili anaweza kumtukana kiongozi au hata kupigana huyo Ndiyo anaonekana shujaa na mkomavu wa kisiasa.

Lakini pia chadema wanaamini juu ya wafahidhina (conservative) katik dhana ya conservative watu ugawanywa katika makundi matatu rejea wakati wa ukoloni ambao walitugawanya ktk makundi matatu yaani.

Grade y'a kwanza Wazungu watawala Grade ya pili wahindi na Waarabu wasimamizi na grade ya tatu Waafrica watawaliwa na wapagazi. Katika vyama vya conservative Mara nyingi hawaamini Juu ya uongozi Bali wanaamini juu ya utawala ndiyo maana Juzi mkisikia Rais wa America kutoka chama Cha Republican Akidaikuwa Waafrica Bado wanatakiwa kutawaliwa na siyo kuongozwa.

kWA chama Kama chadema ambacho falsafa yao imejengwa Juuya utawala Ndiyo maana unaona wanachama wao hawana nafasi ya kukosoa viongozi wao make hawaamini juu ya demokrasia ya dhati wanachama wa chadema Wamegawanyika katika makundi makundi matatu. Kundi la kwanza ni Watawala,Hawa ndiyo watawala hawaguswi hata wawe na Maovu kiasi gani na hao watawala Ndiyo wenye kufikiri na watakachofikiri Hakuna wa kupinga.

Kundi la pili wasimamizi wa maamuzi ya watawala hawa ni Kama wabunge, madiwani, maafisa wa kanda na wenyeviti wa mikoa na kanda hawa Kazi yao kubwa ni kusimamia utekelezaji wa maamuzi ya watawala.Kundi la tatu Ni kundi la wanachama Hawa ni watawaliwa hawana maamuzi yoyote (mazwazwa) wao lazima yao ni kutumika kadri watawala wanavyotoka na Ndiyo maana kila mwanachama wa chadema anapigana awe na nafasi ktk utawala.

Watawaliwa hawa Kazi yao kubwa ni kushabikia chochote kinachosemwa na watawala chini ya wasimamizi.Chama Cha Mapinduzi kiko tofauti Sana na mfumo Huu ambayo baadhi ya wanachama wetu wanataka tuufuate wakidhani kuwa Ndiyo mfumo mzuri WA kupendana ccm inaamini Juuya mfumo wa demokrasia shirikishi inayojengwa juu ya viongozi na Waongozwa tofauti Kati ya kiongozi na mtawala ni kuwa kiongozi anatangulia na Waongozwa wanafuata nyuma Huku wakijifunza toka kwa kiongozi wao wakati mtawala yeye anawatanguliza Wataliwa mbele kuwaswaga Kama wanyama.

Kwahiyo wanaccm wenzangu mnaotaka wanaccm wote waitikie chochote kinachofanywa na viongozi wetu Ukweliiii ni Kwamba huo siyo falsafa ya Chama Cha Mapinduzi wanaccm hawataliwi bali wanaongozwa katika Mfumo halisi ya demokrasia shirikishi isiyo Bagua wanachama na viongozi na Ndiyo maana ndani ya CCM kuna miiko ya viongozi na pale wanaopoenda kinyume na miiko yetu kwakuwa ni viongozi wetu sisi wanachama tunapaswa kuwakumbusha kwa kuwakosoa.

Ushauri wangu kwa wanachama wenzangu hasa wale mnaofikiria kuwa viongozi ndani ya Chama Au viongozi wa umma mnapopata nafasi ya kufika Dodoma tembelea maktaba y'a Chama Chetu pale Makao Makuu ya Chama upitie machapisho na vitabu vya Chama.

Kidumu Chama Cha Mapinduzi.
Na Frey Cosseny
 
Nimejiuliza maswali mengi sana kuhusu hii thread yako la kwanza ni je hapa jf hakuna wana ccm wakuja kukusapoti kwa kile kizuri ulicholeta? 2 : je inakuaje thread ipo jukwaani kwa zaidi ya masaa 7 bila kupata mchangiaji hata mmoja hii tafsiri yake nin?? na mwisho kama akina pohamba ,jingalao,cocochanel ,lizaboni na wengine wana ccm wanashindwaje kuja kuupa uzi unaokinadi chama chao au ndio tayar sasa hivi ishu sio ccm tena bali ni makonda na Magufuli na ukitaka uungwaji mkono na wana ccm basi uwazungumzie hao na si chama? hii ni ishara mbaya sana kwa ccm mitandaoni hasa jf na nikweli cdm wanapendana sana mfano hai ni hili bandiko lako na sapoti ya wanachama wenzako.
 
Umeleta uzi hata wanaccm wenzako wanaona aibu kukuunga mkono. Eti ccm mnaamini katika siasa za ujamaa na kujitegemea!! Kwamba eti ccm wanaruhusu wanachama kukosoa viongozi wao wakati juzi mchana kweupe akina Bashe, msukuma nk wamewekwa ndani kwenye mkutano wa ccm kisa watapinga mambo ya mwenyekiti, mpaka mkutano ulipoisha wakaachiwa. Jomba sasa hivi watu wanawachora tu baada ya wapinzani kuwapeleka puta mmejikuta mnaaigiza uzalendo ambao hauko moyoni, ni kama mmebeba gunia la misumari ili wananchi wawakubali muue upinzani kisha mrudie kwenye deals zenu. Kwa taarifa yako mtalazimisha uzalendo wa kinafiki huku mkuzuia wengine kufanya uhuru nchi nzima lakini wapi, hamkubaliki kihivyo bali mnalazimisha ili muonekane mnakubalika.
 
Back
Top Bottom