Je ni kweli utajiri wa mererani umekwisha?

AljuniorTz

JF-Expert Member
Jan 6, 2009
544
17
Kwa mujibu wa habari zilozopo ni kwamba utajiri wa wana-Apolo umeshuka kwa kasi baada ya migodi wanaoimiliki kukabiliwa na ukata mkali na kukosa fedha za kuendeshea mitaji yao.

Hali hiyo imesababishwa na mambo kadhaa, lakini baadhi yake na muhimu zaidi ni: -
Kushuka kwa thamani ya mauzo ya Tanzanite ktk soko la dunia.
Mgogoro wa kifedha ulioukumba ulimwengu kwa hivi sasa na jengine ni,
Kuongezeka mara dufu gharama za uendeshaji wa machimbo kwa wachimbaji wadogowadogo (Apolo)

Lakini pia serikali nayo inastahili lawama zake kwa namna moja ama nyengine, kwani nayo kwa kutokuweka sera madhubuti na zenye manufaa kwa wananchi wake ambao ni wajasiriamali ktk sekta ya madini zimesababisha kuwepo kwa hali hiyo hivi sasa.

Hebu peruzi kwa undani zaidi stori hiyo hapo chini, then ufikirie wajasiriamali wetu ktk sekta ya madini watafanya nini kwa hivi sasa?



Utajiri wa Mererani kwisha

Mwandishi Wetu, Simanjiro
Februari 18, 2009

Wachimbaji wazawa ukata mtupu

'Nyoka' wageukia uporaji

ASILIMIA 90 ya migodi ya madini ya Tanzanite inayomilikiwa na wachimbaji wazawa katika machimbo ya Mererani wilayani Simanjiro Mkoa wa Manyara, imesitisha uchimbaji wa madini hayo kutokana na sababu kadhaa ikiwamo ukosefu wa mtaji, imefahamika.

Eneo hilo la machimbo ya Tanzanite ya Mererani Wilaya ya Simanjiro limegawanywa katika vitalu vinne ambavyo ni A kinachomilikiwa na Kampuni ya Kilimanjaro, B kinachomilikiwa na wachimbaji wadogo, C kinachomilikiwa na kampuni ya wawekezaji kutoka Afrika ya Kusini ya TanzaniteOne na D kinachomilikiwa na wachimbaji wadogo.

Ofisa Mfawidhi wa Kanda ya Kaskazini wa Idara ya Madini, John Shija, alithibitisha wiki hii ya kuwa idadi kubwa ya migodi imesitisha kazi kutokana na sababu kadhaa ikiwamo ya kukosekana kwa fedha za kuendeshea kazi hiyo miongoni mwa wachimbaji.

Tanzanite

Tanzanite

“Ni kweli kuna migodi mingi haifanyi kazi kwa muda mrefu na hii inatokana na kushuka kwa bei ya Tanzanite katika soko la ndani kwa karibu asilimia 60, hivyo wachimbaji wanashindwa kuhimili gharama za kuchimba, ” alieleza.

Kwa mujibu wa tawimu za Idara ya Madini Mererani katika eneo la kitalu B kuna jumla ya migodi 323 lakini inayofanya kazi ni migodi 20 tu wakati kitalu D kina jumla ya migodi 382 na inayofanya kazi si migodi zaidi ya 30.

Wakizungumza wiki iliyopita kwa nyakati tofauti na Raia Mwema hapa, baadhi ya wamiliki wa migodi hiyo walidai kuwa kushindwa kwao kuendesha shughuli za uchimbaji kumesababishwa na sababu nyingi ikiwa ni pamoja na ukosefu wa fedha na kuongezeka kwa gharama za uchimbaji wa madini hayo.

“Wachimbaji wazawa wameathiriwa sana na matokeo ya sera mbovu za Wizara ya Madini na Nishati kwa upande mmoja, lakini pia wao wenyewe kutokana na upeo na uelewa mdogo wa kuendesha shughuli za uchimbaji, wamejikuta wakishindwa kuendelea na kazi hii, ” alieleza mmoja wamiliki wa migodi hiyo aliyeomba jina lake lihifadhiwe.
Alieleza zaidi kuwa kwa upande wa wachimbaji kukwama kwao kumetokana na kuongezeka kwa gharama za uchimbaji na pia kuwa na zana hafifu za kufanyia kazi huku migodi mingi ikiwa na kina kirefu cha mita kati ya 500 hadi 800.

Kwa sasa gharama ya chini kabisa inayoanishwa na wachimbaji katika kuhudumia mgodi ni kuanzia shilingi 250,000 kwa siku hadi 500,000, ambazo ni nyingi sana kwa mchimbaji wa kawaida.

Gharama hizo zinahusisha ununuzi wa zana za kulipulia miamba kama coltex (35,000/=), fataki (27,000/=) Mafuta (90,000/=), chakula cha kulisha wachimbaji wanaozama mgodini kufanya kazi na wale wanaotoa mchanga na kila mgodi unakuwa na wastani wa wafanyakazi kuanzia 50 na kuendelea na gharama nyingine za kuendesha mashine.

“Ukijumlisha gharama hizo zote utaona kuwa kuhudumia mgodi kwa wastani, mmiliki lazima atumie zaidi ya shilingi 250,000, fedha ambazo ni nyingi sana kwa mazingira ya sasa kwani kwa mwezi unatakiwa uwe na wastani wa shilingi milioni 4 hadi 10 ili ufanye kazi vizuri,”alisema mmiliki huyo.

Aidha, mmliki huyo alieleza kuwa pia kutokana na upeo mdogo na na tamaa ya kupata utajiri wa haraka wachimbaji wengi walishindwa kuwekeza katika migodi yao kwa kuweka miundo mbinu chini ya ardhi na kununua mashine za kisasa wakati walipokuwa wanapata fedha kutokana na mauzo ya tanzanite.

Hali hiyo leo ndiyo inayowagharimu kwani kutokana na uchimbaji usiozingatia kanuni, migodi mingi imekuwa na vina virefu vya kuanzia mita 600 huku upatikanaji wa madini ukiwa ni wa kiwango cha chini kuliko ilivyowahi kutokea katika historia ya uchimbaji wa madini hayo.

“Katika miaka ile ya mwanzo wakati madini hayo yakiwa na thamani kubwa wamiliki wengi kwa ubinafsi na upeo mdogo, walishindwa kuwekeza katika miundo mbinu ya migodi yao na kununua mashine za kufanyia kazi hali ambayo madhara yake yanaonekana leo,”anaeleza.

Anataja sababu nyingine kuwa ni sheria za uchimbaji za Wizara ya Nishati na Mdini kama ile inayowataka wachimbaji wadogo kuchimba katika maeneo yao madogo yenye ukubwa wa mita 50 kwa 50 ambayo matokeo yake ni wachimbaji wadogo kuingiliana chini ardhi na pia kuwa na migogoro isiyoisha baina yao.

Mchimbaji huyo anasema kuwa kutokana na kushamiri kwa vitendo vya rushwa na ufisadi miongoni mwa maofisa wa Wizara ya Nishati na Madini, zimewekwa baadhi ya sheria za kulinda maslahi ya wawekezaji na zimewakandamiza wachimbaji wadogo ambao wamejikuta mara kwa mara katika migogoro na mwekezaji badala ya kutumia muda wao kufanya shughuli za uzalishaji.

“Mwekezaji amepewa eneo lenye urefu wa kilomita 8 ambalo ndilo lina hazina kubwa ya tanzanite, matokeo amekuwa akiwanyanyasa wachimbaji wadogo anaopakana nao kwa kuwafanyia vitimbi mbalimbali, ”anaeleza mchimbaji huyo.

Kwa upande wake, mchimbaji mwingine, Awadh Omar, ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mererani (CCM) anasema kuathirika kwa shughuli za uchimbaji na wachimbaji wadogo kunatokana na kupanda maradufu kwa gharama za uchimbaji huku bei ya madini hayo ikiyumba katika soko la dunia.

“Kwa sasa bei ya Tanzanite katika soko imepungua kwa asilimia 40 kutokana na kuporomoka kwa uchumi wa dunia….na kuvaa vito si kipaumbele katika maisha ya watu wengi, bali hutumia fedha zao za ziada na kwa kuwa hawana ziada tena basi bei ya vito vingi ikiwamo tanzanite imeshuka,” anaeleza diwani huyo.

wachimbaji wadogo

Wachimbaji wadogo wa Tanzanite

Anaongeza: “Watu wengi nchini Marekani ambako ndiko asilimia 80 ya tanzanite inayozalishwa Mererani huuzwa, wamepoteza kazi zao, hivyo hawana uwezo tena wa kununua vito na matokeo yake hata bei katika soko la ndani imevurugika".

Awadh anaongeza kuwa tatizo jingine ni la kisera na limetokana na Wizara ya Madini na Nishati kugawa eneo la kitalu C kwa wawekezaji wa kigeni wanaotumia zana za kisasa katika uchimbaji hali ambayo imesababisha wawekezaji hao kuvuna tanzanite nyingi kuliko mahitaji ya soko.

Diwani huyo anasema kwa sasa ni vigumu wachimbaji wadogo kuweza kujikwamua kama Serikali haitaingilia kati kwa kurekebisha kasoro zilizopo lakini pia wachimbaji wenyewe hawana budi kuunganisha maeneo yao na kuunda kampuni kubwa ili kuweza kushindana na wawekezaji badala ya kuendelea kuchimba mtu mmoja mmoja.

“Serikali sasa iwaelimishe wachimbaji wadogo ili wakae pamoja na wataalamu na wanasheria waunde makampuni ambayo yatachimba kwa kutumia zana za kisasa na uzalishaji utaongezeka. Hata hii kampuni ya Afrika ya Kusini si ya mtu mmoja bali ni kundi la watu wengi ambao wameamua kukaa pamoja na kuweka utaratibu wa uendeshaji na unaona mambo yanakwenda vizuri, ” alishauri diwani huyo.

Diwani huyo anaeleza kuwa matokeo ya kushuka huko kwa uchimbaji na mauzo ya tanzanite kumesababisha watu kuhama mji wa Marerani huku biashara nyingine zikidorora na visa vya wizi mdogomdogo vikiwa vimeshamiri kutokana na vijana wengi kukosa kazi za kufanya.
"Vijana wengi wamejiingiza katika vitendo vya uporaji kutokana na kukabiliwa na njaa na matukio ya aina hiyo yamekuwa mazoea katika eneo hili sasa," anasema diwani huyo.

Madini ya tanzanite ambayo hupatikana katika eneo la Mererani pekee duniani, yamekuwa yakinufaisha zaidi mataifa mengine hasa nchi za Kenya, Afrika Kusini na India ambazo ndizo zinazoenekana kama wauzaji wakubwa wa madini hayo katika soko la dunia.
Hali hiyo inaelezwa kuwa inatokana na Serikali ya Tanzania pamoja na wadau wengine kushindwa kuweka sera na mipango madhubuti ya kuchimba na kuuza madini hayo katika soko la dunia.


TAFAKARI
 
Katika kitabu "The Ascent of Money: A Financial History of The World" profesa wa Harvard Niall fergusson ameelezea jinsi gani ufalme wa Hispania, licha ya kuwa na mlima wa madini ya fedha huko Peru (the legendary Eldorado), haukufanikiwa kuwa mahiri katika uchumi kuliko Wataliano na Wadachi ambao walikuwa hawana mlima wa fedha, lakini walikuwa na mfumo mzuri wa biashara na masoko ya mitaji.

Mzee Mwinyi alitumia msemo mmoja wa Kiswahili, "Mali bila daftari, hupotea bila habari"

Sasa sisi inaonekana tunabweteka sana na hizi maliasili bila ya kutaka kufanya kazi ya akili (masoko ya mitaji, kusafisha na kutengeneza vito n.k)

Hata hao waarabu waliobweteka na mafuta siku hizi wanaamka.
 
Sio tu wizi utaongezeka sanasana Arusha bali kama ni kweli upatikanaji wa Tanzanite unahusishwa na imani za kishirikina basi tatizo la kuuwawa maalbino ndio kwaanza limeanza. Watu waliozoea kunywa from am to am kwa sababu ya hela za the so called mawe watalazimika kufanya juu chini machimbio yateme waendelee kutanua.
 
Mmh! hapo kazi ipo, wana apollo itakuwaje?isije kuwa janja ya mwekezaji ili aendelee kutolipa mrahaba na ushuru,
please weka proof ndg!then tutajua what next.
 
Mmh! hapo kazi ipo, wana apollo itakuwaje?isije kuwa janja ya mwekezaji ili aendelee kutolipa mrahaba na ushuru,
please weka proof ndg!then tutajua what next.

Mwekezaje hana uhusiano na wachimbaji wadogowadogo (wana-apollo), hawa ni wachimbaji wanaojitegemea ktk vitalu vyao.

Wawekezaji nao wanavitalu vyao, ambao wao hawajakumbwa na msukosuko mkubwa labda wao tatizo litakuwa lipo ktk uuzaji ktk soko la dunia km nilivyoeleza hapo juu, manunuzi ya Tanzanite yameshuka.

Thanx
 
Back
Top Bottom