Je, Ni kweli ukitakata kumpata mke anayekufaa ni lazima uwe na uzoefu na wanawake?

Markomx

JF-Expert Member
Apr 23, 2016
701
701
Wakuu salam kwa wote,

Mara nyingi huwa tunapenda kukaa na waliotutangulia kuzaliwa kupata uzoefu wa mambo ya ndoa na ushauri wa mambo mengine.

Kifupi, nina rafiki ni mkubwa kiumri kidogo na ana mke na watoto, pia sio mtu wa michepuko. Ni brother wa mfano, ana maadili YALIYOTUKUKA, anamjali mke wake na anaipenda familia yake. Kuna siku wakati tunapiga stori za kumpata mwanake bora alinifurahisha na kunishangaza kidogo, alisema "KIJANA, UKITAKA KUMPATA MWANAMKE ANAEKUFAA NI LAZIMA KWANZA UWE UNA WAPENZI SIO CHINI YA 8".

Reason yake kubwa anadai huwezi kufanya COMPARISON ukiwa na mpenzi au mchumba mmoja,huwezi kumjua yupi ni mzuri kama hayupo wa kulinganishana nae, yupi anakupenda kama hakuna wa kulinganishana nao,yupi anapenda pesa kama hauna asiyependa pesa, yupi mvivu kama hauna mchapakazi, yupi kitandani yupo vizuri kama hauna wa kulinganishana nao.

Baada ya hapo ndio unafanya choice ya yupi ni yupi, ila ni baada ya kufanya vetting ya maana na inachukua sio chini ya miezi 6 na kuendelea.

Nimeamua kuja kushea huu ushauri maana ndoa nyingi zimebaki kuwa majuto ni mjukuu, michepuko imekua kama ndo sehemu ya maisha, huenda walikosa hili somo la wahenga.

NB: Hii ni applicable kwa both sex.

Huu ushauri unauonaje mwanaJF? Inaweza kuwa ni njia nzuri kweli kama vetting system ya kupata mke/mme bora?

Nawasilisha..
 
Majanga wallah.
Sasa wanane wanatosha kweli! Wakati wanaadamu wana tabia Zaidi ya Hamsa?
 
Na je wakati unalala nao ili uwachuje na kupata mke ukipata UKIMWI? Umejiuliza hilo?

Sio kweli, tumia akili zako sio kila ushauri ni mzuri.
 
Na je wakati unalala nao ili uwachuje na kupata mke ukipata UKIMWI? Umejiuliza hilo?

Sio kweli, tumia akili zako sio kila ushauri ni mzuri.

mkuu,iyo ni side effect moja wapo,ila jamaa hakugusia ilo moja tu,unaweza aply mbinu nyingne bila kufanya sex
 
niliitumia njia hii kumpata mama wawili wangu...

sasa hv nmetulia tunalekebishana mapungufu yetu taratibu kuelekea ndoani.
 
Katika hili hakuna uzoefu, ni kumuomba Mungu tu akupe anaekufaa, ila ukumbuke hakuna binadamu aliyekamilika, kitu cha muhimu ni kumpata mtu muelewa na msikivu.

ila kunawakati tunajitakia wenyewe,tunajikuta tunashawishika kuoa au kuolewa,ukiisha ingia unaanza kubaini mbona kunamapungufu makubwa nyumba inakua chungu michepuko ndo inakua kimbilio,unajikuta,unaanza kufanya comparison uko ndani ya ndoa
 
Si kweli, mapenzi ya dhati ni yale yasiomithilika. Kitendo cha kutaka kumfananisha mpenzi wako na mtu mwingine tayari kushakuwa na walakini hapo. Mpenzi uliekuwa nae anapaswa awe ni kila kitu kwako, umchukulie ni timilifu japo ana mapungufu. Hakuna aliekamilika lakini katika moyo wako na nafsi yako inapaswa awe ni kila kitu. Utakapokuwa na wapenzi nane kwa kigezo cha kuwa na point of comparison jielewe kuwa tayari ushakuwa na nafasi nane za uwezekano wa kumsaliti mpenzi/mke/mume wako wa mbeleni.
Kwa dunia ya leo mapenzi yashapoteza maana halisi sababu tumeweka tamaa za maslahi ya kiuchumi na kimwili mbele ila ukifuatilia mapenzi kama mapenzi huitaji mfano wa aina yeyote pale ukimpata umpendae. Elewa mapenzi si utimilifu wa kila nyanja bali ni hali ya kukubali mapungufu ya mwenzi wako bila kumhukumu.
Ndoa nyingi leo zinavunjika sababu haturidhiki na tulichonacho. Ukipata anejua kupika utasema hajui mapenzi, akijua mapenzi utatafuta dosari nyingine kwa kigezo cha mwenza aliepita. Maana halisi ya upenzi wa dhati ni kumfanya mwenza wako awe ni sehemu ya maisha yako kwa minajili ya kwamba kila mmoja wenu afidie mapungufu ya mwenzi wake. Kama hajui kupika basi thamini kile anachokijua.
Na hapa ndipo tunapotofautiana na mababu zetu. Waliweza kudumu kwa muda mrefu katika ndoa zao sababu mara nyingi kila mmoja alikuwa ndio wa kwanza kwa mwenzie na ndoa haikuwa mtaji ama fashion bali ni kitu takatifu.
 
hiyo idea Nilishauriwag na mim niwe ivo!!!!!!! wote 8 hao kila mtu alianza na kutaka tu do hata miez 6 haijafika ya kujuana ndo kwanza mwez 1 nilisikia kichefuchefu Nikawa block wote!!! Tangia hapo jinsia hyo nikiiona nakwazka ila MUNGU asaidie. so hiyo kitu 1 watu 8+ nothing!!!! kuna UKIMWI alafu wanakatabia haka ata km hawajuan,,, wakija kwa mpigO siku ukiselect only 1 wengne ukawaaga hata utakae kuwa nae utmchoka coz ulikuw ukipat stress za mchoyo unaend kwa asie mchoyo,,, halikadhalika na kw mwizi >sio mwizi, malaya>sio malaya,,,yaan wew kwako kuumiza ubongo hutaki bas ata kwenye ndoa utakuw hivohvo.
 
Wakuu salam kwa wote,

Mara nyingi huwa tunapenda kukaa na waliotutangulia kuzaliwa kupata uzoefu wa mambo ya ndoa na ushauri wa mambo mengine.

Kifupi, nina rafiki ni mkubwa kiumri kidogo na ana mke na watoto, pia sio mtu wa michepuko. Ni brother wa mfano, ana maadili YALIYOTUKUKA, anamjali mke wake na anaipenda familia yake. Kuna siku wakati tunapiga stori za kumpata mwanake bora alinifurahisha na kunishangaza kidogo, alisema "KIJANA, UKITAKA KUMPATA MWANAMKE ANAEKUFAA NI LAZIMA KWANZA UWE UNA WAPENZI SIO CHINI YA 8".

Reason yake kubwa anadai huwezi kufanya COMPARISON ukiwa na mpenzi au mchumba mmoja,huwezi kumjua yupi ni mzuri kama hayupo wa kulinganishana nae, yupi anakupenda kama hakuna wa kulinganishana nao,yupi anapenda pesa kama hauna asiyependa pesa, yupi mvivu kama hauna mchapakazi, yupi kitandani yupo vizuri kama hauna wa kulinganishana nao.

Baada ya hapo ndio unafanya choice ya yupi ni yupi, ila ni baada ya kufanya vetting ya maana na inachukua sio chini ya miezi 6 na kuendelea.

Nimeamua kuja kushea huu ushauri maana ndoa nyingi zimebaki kuwa majuto ni mjukuu, michepuko imekua kama ndo sehemu ya maisha, huenda walikosa hili somo la wahenga.

NB: Hii ni applicable kwa both sex.

Huu ushauri unauonaje mwanaJF? Inaweza kuwa ni njia nzuri kweli kama vetting system ya kupata mke/mme bora?

Nawasilisha..
Akili za kuambiwa changanya na zako.
 
Mmmmh hizo mambo za kupata mke anaekufaa ni kama bahati tu..kuomba mungu asaidie,unaweza pata mwenzi wako katulia saana ila sasa kumbe hauna hisia nae za mapenzi kihivo ila kuna yule kiluka njia unahisia nae saana ila daaah pasua kichwa vbaya mnoo..
 
hongera mkuu,kwa kuaply hii principle,vinginevyo ungekua unahaha huishiwi kwa michepuko
usimpe hongera jiulize je huyo alienae ni wangapi walim test wakaona chenga, au yy huyo jamaa ni wanawake wangapi alishindwana nao kutokana na tabia zake? sasa tuachane na hayo, kwa mfano umefanya machaguo yako alaf ukapata mwanamke mzuri uliemtaka baada ya miezi 6 ukagundua kuwa hana kizazi au kaparamiwa na bodaboda akapata kilema si itabidi umwache kwa kuwa atakuwa amepoteza sifa? mambo mengine huwa yanakuja yenyewe tu, kwani ni wangap vicheche na wameshindwa kupata machaguo yao mpaka wanazeeke?
 
Njia sahihi ni moja tu,kuwa mcha MUNGU sana ili dua za ww kupata make bora MUNGUazipokee na kukupa mke wa kufanana na wewe,
Sekunde moja ya shambuluzi la shetani inatosha kabisa kumgeuza mke ulodhani umemchunguza na anakufaa,wanawake hubadirika sana tena zaidi ya sana,kuwa bora Leo haikugarantee kuwa itakuwa hivo daima,
Ni MUNGU tu
 
hiyo idea Nilishauriwag na mim niwe ivo!!!!!!! wote 8 hao kila mtu alianza na kutaka tu do hata miez 6 haijafika ya kujuana ndo kwanza mwez 1 nilisikia kichefuchefu Nikawa block wote!!! Tangia hapo jinsia hyo nikiiona nakwazka ila MUNGU asaidie. so hiyo kitu 1 watu 8+ nothing!!!! kuna UKIMWI alafu wanakatabia haka ata km hawajuan,,, wakija kwa mpigO siku ukiselect only 1 wengne ukawaaga hata utakae kuwa nae utmchoka coz ulikuw ukipat stress za mchoyo unaend kwa asie mchoyo,,, halikadhalika na kw mwizi >sio mwizi, malaya>sio malaya,,,yaan wew kwako kuumiza ubongo hutaki bas ata kwenye ndoa utakuw hivohvo.

solution ni ipi mkuu,unafanyaje vetting kumpata yule wa ndotoni?
 
Back
Top Bottom