Ayenda M
Member
- Jan 4, 2018
- 97
- 132
Soka la Kiafrika ni la aina yake kabisa. Soka la Kiafrika lina utamaduni wake na mambo yake tofauti na soka la mataifa ya Ulaya. Ukifuatilia sana masuala ya ndani kwenye soka la Kiafrika unaweza jikuta unauchukia mchezo wenyewe.
Kuna vitu vinatokea kwenye soka letu badala ya kukuhuzunisha inabidi ufurahie. Juzi kati kuna baraka ilitokea kwenye Ligi yetu baada ya Kampuni ya GSM kuingia mkataba wa kuidhamini Ligi. Ni jambo la baraka ila ni baraka ambayo inaacha maswali mengi?
1. Je, ni sahihi kwa boss anayetaka kuwa na umiliki wa timu kudhamini Ligi ambayo anamiliki timu? Tumwangalie Eng. Hersi, Haji Manara na Senzo Masingiza ambao ni mabosi pale yanga na Frontmen kwenye timu na kampuni ya GSM ambao ndio walikuwepo kwenye utiaji wa SAINI pale TFF. Kwanini wao? Kwa picha ndogo tunayoipata ni kuwa GSM na YANGA ni kitu kimoja na ndio maana viongozi wake wa juu wanafanya kazi pande zote mbili. Kuna dhana inafichwa na tunazidi kufichwa mashabiki.
Mashabiki walio wengi wanatumia mwamvuli wa AZAM TV kutaka kupitisha mawazo yao lakini wanasahau kuwa Popat pale Azam FC hajawahi kukaa mezani na Mzee Tido Mhando kusaini mkataba wa haki ya Udhamini wa matangazo kupitia Television.
Na watetezi wanasahau kuwa Mzee Bakheresa hajawahi kuingia kamati ya Usajili ya Azam FC au kuonekana akijadili masuala ya timu live tena akiwa na benchi la Ufundi. Kama anafaya kuna ethics anafuata tofauti na Mzee Ghalib. Maboss wa GSM ndo wanasajili, wanalipa mishahara na kutoa bonus kadhaa, tukumbuke kauli ya Khalid Aucho.
2. Dhana ya Umiliki na Udhamini! Hapa ni mtego mkubwa. Ukweli ni upi? Hivi Yanga anadhaminiwa au anamilikiwa na GSM? Kabla hatujajibu swali hili tukumbuke kuwa Club ya Yanga na GSM wapo kwenye transformation kama ilivyo kwa Simba ambayo tiyari ishaanza kumilikiwa kwa 49% ya hisa zake na MO.
Nini nakiona? Endapo mchakato utakamilika inamaana GSM atakuwa anamiliki hisa asilimia kadhaa pale Yanga na probably 49% ya hisa zote na hivyo kuwa mmiliki. Je, wale tunaotetea udhamini wa GSM kwenye ligi kuwa hauna athari kwenye mpira wetu itakuwaje kesho mchakato ukikamilika rasmi? Ina maana kampuni inayomiliki timu, inadhamini ligi kuu ambayo timu hiyo inacheza.
3. Kwanini nguvu kubwa inatumika kuhalalisha udhamini huu? Udhamini wa Azam Tv ulipita bila kelele kubwa za wadau. Udhamini wa NBC ukapita bila kelele. Swali kwanini wadau wanautilia shaka udhamini huu? Hadi FCC kuingilia kati.
Hapa ndipo wenye jukumu la kuongoza soka letu wanapaswa kupatazama. Macho ya wadau wengi yanaona mbali na ndo maana wanahoji. Msemaji wa Timu, Mjumbe wa kamati ya usajili na mshauri (mtendaji mkuu) wa timu wanawakilisha kampuni kwenye utiaji saini wa issue nyeti then watu wanyamaze wasihoji? Hapana. Sio sahihi.
Nitakuwa mtu wa mwisho kuamini kuwa GSM na Yanga si kitu kimoja na udhamini huu sio kimkakati. Na soka hili lina aina yake kabisa.
Pesa kwenye soka letu inahitajika tena sana lakini tuangalie namna nzuri ya kupata udhamini wenye sura nzuri. Itakuwa sahihi zaidi kama GSM ataweka pesa yake CHAMPIONSHIP au LEAGUE ONE maana huko ndo hatutahoji sana.
Ni wakati sasa kuacha mpira uchezwe bila kelele zisizo za lazima. FAIR COMPETITION. Atakayesukuma kete yake vibaya kwenye hili asilaumu mbeleni. Heko kwa wale wanaohoji.