Je, ni kweli tunahitaji 'graduates' wengi?

Tanzanite klm

JF-Expert Member
May 7, 2013
453
376
Habari za wasaa huu!

Tanzania sasa imefikia kundi la mataifa yaliyo uchumi wa kati lakini sasa tunahitaji juhudi na mikakati mingi zaidi iliyo kabambe kuwea kufikia uchumi wa juu tuwe kundi moja na Singapore au Uingereza.

Tumekua na kasumba kuwa lazima tuwe na watu wenye degree wengi sana mitaani, lakini tatizo ni kuwa tuna graduates wengi wasio ajirika na productivity yao ipo chini.

Ben Shapiro amewahi zungumzia katika kitabu chake kimoja namna elimu ya chuo kikuu imegeuka na kuwa biashara na nlengo lake hasa sio kumtengeneza mtu bali ni kutengeneza kitu.

Katika dunia tunayoishi sasa iliyojaa mparanganyiko wa kila namna tunahitaji elimu inayomtoa mtu mwenye fikra yakinifu na anayeweza kwenda na usasa.

JE, TUNAHITAJI UTITIRI WA VYUO VINAVYOTOA DEGREE?
Tunahitaji vyuo vya ufundi vya kutosha, jamii ya DIT, vyuo vya VETA vya kutosha, baada ya hapo tutahitaji wataalamu wa masuala ya biashara. Wataalamu wenye uzoefu mkubwa katika masuala ya biashara za kimataifa ili kusaidia hawa wanaomaliza VETA kuanzisha miradi yao mikubwa.

WE NEED MORE:
POLYTECHNICS UNIERSITY
VOCATIONAL EDUCATION COLLEGES

Pia serikali serikali kama inatoa fedha nyingi kama mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu ni kitu kizuri ila pia serikali iangalie utaratibu wa kutoa ruzuku au mikopo kwa wanafunzi wanaomaliza vyuo vikuu waweze kufungua miradi mikubwa lakini wawe chini ya uangalizi maalumu.

SIDO ipewe nguvu kubwa, SIDO inaweza kutupeleka mbali sana ikipewa nguvu.

Mafundi wana mchango mkubwa sana katika ujenzi wa hii nchi yetu na dunia kwa ujumla.

Mafundi walio soma Veta na ma engeneer wa vyuo vya kati.
 
Hoja yako ni cross cutting na haina jibu mojà ila ntachangia kwa angle ambayo kama tunakubaliana ifanyiwe kazi itakuwa na manufaa kwa wahitimu wa vyuo kwa level yoyote ambayo mtu anapata professional training.

Gradutes (wahitimu wa vyuo) iwe kwa level ya cheti, stashahada, shahada ambayo ndio msingi wa hoja yako watakuwa wahana maana yoyote kama hakuna mazingira ya kuwa-absorb baada ya masomo.

Mathalani, wakati wa mwl. Nyerere alikuwa na very graduates wa kiwango cha shahada. Watu waliohitimi kidato cha nne waliafanya kazi nyingi katika sekta umma hasa na binafsi kwa kuwa nafasi za kazi zilikuwepo na waajiri walitoa nafasi ya waajiriwa (graduates) kuwa na onjob training.

Tusitafute quick fix kwa kudhani VETA au Technicians wa vyuo kama Mbeya Tech, Arusha Tech na Dar Tech kama zitarejeshwa kama kuongeza ufanisi wa hawa vijana kufanya miujiza.

Ni lazima Taifa lije na ubunifu wa kufanya liwalo na liwe ili kuzalisha kazi.

Zamani bank tellers hata darasa la 7 walifanya. Leo kazi ya teller wa bank mpaka MBA Holders, ukiangalia wanajaza vyeti kulinda ajira na sio kuongeza ufanisi kwa kazi za U teller.

Hata kazi za ambazo hazihitaji lots of practical hands on training kama Ualimu na Udaktari nao wanapiga msuli.

Ushuri wangu, ili mbegu iote na kuzaa matunda ni lazima kuwa na supportive system; temperate, oxygen na moisture.

Mbegu ikiota lazima ilindwe, imwagiliwe na kuwekewa mbolea ili kupata maximum production kutoka kwenye mbegu.

Nadhani wizara ya Ajira ina Waziri ambaye ka-focus kwenue kazi za kibunge na hana DNA na innovation kuzalisha ajira.

Ana mifuko ya pension chini yake, boss wake (immediate boss ni Waziri Mkuu) ila anashinda kuja na interconnection ya resource available ili hawa graduates wapate platform kutumia akili zao kuzalisha.

Nguvu kazi ni rasilimali. Nguvu kazi ambao ni vijana ni nguvu kazi ambayo, kama itaelekezwa vyama kwa kujenga mazingira watachangia sana kukuza uchumi wa Tanzania.

Kuna wakati Rais JPM aliwahi kusema I wish I could be IGP maana aliona Jeshi la Polisi chini ya Ernest Mangu lilikuwa linalegea.

Nadhani kama wizara ya kazi na ajira kwa kushirikiana na wizara ya viwanda & biashara, kilimo, uvuvi, mifugo na madini kuna lots of organized jobs could be created ili vijana washinde in the course tax base inakuwa na tunapunguza imports na kuongeza exports.

Wakati mmoja Rais Mkapa alisema Watanzania ni wavivu wa kufikiri; wàtu wakachukia sana. Nataka nikiri uvivu wa kufikiri unaendelea kuongezeka in the course.

Kuna watu kujifichia tunatengeneza mifumo, yet hatuoni mifumo ikiwa na msaada kama watu hawafikiri "nje ya box".

JPM kama angeweza, kama jinsi alivyo na official TISS kama DSO, RSO na DG wa TISS, hawa wanafahamika, ila ana vijana ambao hawafahamiki who is who.

Aje na parrel system ya kufanya kazi hasa za kujenga uchumi, ili kama hawa known portfolio ministers wanashindwa kukimbizana na kazi yake, hawa vijana wa kitaa wampe how it takes to get there ili kuzalisha organized system za kujenga uchumi jumuishi na endelevu. Ofcourse ikifikia hatua ya mwisho ya ku-execute, hawa portfolio ministers watafanya kama wajibu wao.

Maana ugumu ni project/investment design hapo bila shaka wenye DNA ya kufikiri bila shaka tunao wachache.

Ukitaka kujua, sikiza radio, soma magazeti, tembelea social media na network few people speaks, writes and shares outbox innovations. Wengi bla bla na kusifiana na kukandiana pas kuonesha solution.

Lots can be accomplished in our motherland Tanzania kama mazingira yatajengwa ili yatokee.

Mungu Ibariki Tanzania
 
Hivi kwa akili ya kawaida unafikiri uhitaji wa wataalam umetosha?

Kwa muono wangu bado uhitaji ni mkubwa tu, si walimu si wagavi au mainjinia.

Kinachosumbua ni kwamba nchi bado masikini na uchumi ni mdogo sana, serikali bado inahitaji wataalam ila uwezo wa kuajiri na kulipa haupo!
 
Hivi kwa akili ya kawaida unafikiri uhitaji wa wataalam umetosha?
Kwa muono wangu bado uhitaji ni mkubwa tu, si walimu si wagavi au mainjinia..
Kinachosumbua ni kwamba nchi bado masikini na uchumi ni mdogo sana, serikali bado inahitaji wataalam ila uwezo wa kuajiri na kulipa haupo!
Na haya mamiradi yetu makubwa tuliyo anzishiwa na mzee wetu kwenye hii awamu yake ya tano, nadhani yanachangia pakubwa kukomba kile kibubu chetu cha hazina, na hivyo kukikuta kushindwa kuajiri wahitimu kwa kiwango kinacho takiwa!

All in all, naunga mkono ubadilishaji wa mitaala yetu. Hii mambo ya kulazimisha watanzania wote wasome mpaka kidato cha nne na kuendelea, halafu mwisho wa siku wanaishia kuwa bodaboda, nadhani ingetazamwa upya.

Kama kuna uwezekano, tungeiboresha ile sera ya Mwalimu Nyerere ya Elimu ya Kujitegemea. Hii ingechangia sana kupunguza hili tatizo kubwa la ajira, lakini pia elimu isiyo ma uhusiano kabisa na mazingira yetu.
 
Elimu ya chuo kikuu ni ya muhimu sana ili tuweze kuwa competitive katika dunia hii. Ila content matters a lot.
Israel au Netherlands, wakulima/wafugaji/wavuvi ni graduates.

Na viwanda vya maziwa, viwanda vya nyama, textile, viwanda vya madawa ya mifugo, viwanda vya mbolea ni kampuni kubwa ambazo shareholders wakubwa ni wakulima.

Tanzania imekosa msemaji wa kuisemea kilimo kama Elimu ya kujitegemea. Mkulu amekaa muda mrefu ujenzi na DNA ya kujenga imemwingia vema.

Ilitakiwa tuwe na kama sio sectoral ministers basi outsiders kwenye uwekezaji uliopo mpya ambao unatufanya tujenge uchumi jumuishi na wa kujitegemea.

Tanzania 70%wanategemea kilimo, uvuvi na mifugo.
Tanzania ni nchi ya 2 kuwa na ng'ombe wengi Africa.
Tukiwa na DNA ya kufikiri na kumtaka Mkulu ajali kilimo sio kwa kutoa hela pekee, hapana. Hata kutoa gov guarantee kwa mimi ninaetaka kuanzisha kiwanda cha mbolea au madawa ya mifugo. Soko liko wapi, Tanzania na South Sudan kama ni madawa ya mifugo.

Uzalishaji wa viwanda kama hivyo vitapunguza cost ya kuagiza madawa nje na kuongeza mzunguko maana soko la wafugaji lipo.

Kama ni mbolea au viwatilifu, kwa kuwa nina soko la ndani, kwanini TIC na Wizara ya uwekezaji isinipe access ya certificates tu na ardhi then kwa kufanya hivyo inakuwa sehemu hata ya management ili kufuatilia step kwa step kama ninatekeleza.

It begins with leadership. Kama kuna attitude ya kufanya liwezekanalo mambo yatokee tutapaa kwa haraka sana.

Ila kama tuna watu wana checklist ya fanya hivi, njoo na hiki, leta hiki, mbona hajafanya hiki; kwa namna hiyo tunajichelewsha sisi wenyewe.

Lazima tuwe na PPP yenye winning team na sio upande mmoja hasa ambao una dhamana ya rasilimali nyingi (serikali) kuwa passive.

Mandela hakuwa na passport ili afanye shughuli za kuhamasisha ukombozi wa bara la Africa. Mandela hakuwa raia wa Tanzania. Mwl. Nyerere kwa kujua passport ni ufunguo kwa Mandela kusafiri pasi vikwazo alimpa passport.

Kuna Watanzania wanahitaji gov backing tu. Kuna partners wa uwekezaji wanataka kufanya kazi na Watanzania; ila wanachotaka ni assurance kama serikali iko nyuma yao. Sio kwa matamko ya jukwaani, ila kwa maandishi na certification kwenye potential investments.

Haya yakifanyika, graduates wataona raha kutumia akili na nishati zao kuwa sehemu ya kujenga uchumi wetu. Hakuna la kujivunia ati graduate wa Masters degree anaendesha bajaji; bajaji made in India.
No, we can do something better to change the present situation only if we listen to one another.
 
Habari za wasaa huu!

Tanzania sasa imefikia kundi la mataifa yaliyo uchumi wa kati lakini sasa tunahitaji juhudi na mikakati mingi zaidi iliyo kabambe kuwea kufikia uchumi wa juu tuwe kundi moja na Singapore au Uingereza.

Tumekua na kasumba kuwa lazima tuwe na watu wenye degree wengi sana mitaani, lakini tatizo ni kuwa tuna graduates wengi wasio ajirika na productivity yao ipo chini.

Ben Shapiro amewahi zungumzia katika kitabu chake kimoja namna elimu ya chuo kikuu imegeuka na kuwa biashara na nlengo lake hasa sio kumtengeneza mtu bali ni kutengeneza kitu.

Katika dunia tunayoishi sasa iliyojaa mparanganyiko wa kila namna tunahitaji elimu inayomtoa mtu mwenye fikra yakinifu na anayeweza kwenda na usasa.

JE, TUNAHITAJI UTITIRI WA VYUO VINAVYOTOA DEGREE?
Tunahitaji vyuo vya ufundi vya kutosha, jamii ya DIT, vyuo vya VETA vya kutosha, baada ya hapo tutahitaji wataalamu wa masuala ya biashara. Wataalamu wenye uzoefu mkubwa katika masuala ya biashara za kimataifa ili kusaidia hawa wanaomaliza VETA kuanzisha miradi yao mikubwa.

WE NEED MORE:
POLYTECHNICS UNIERSITY
VOCATIONAL EDUCATION COLLEGES

Pia serikali serikali kama inatoa fedha nyingi kama mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu ni kitu kizuri ila pia serikali iangalie utaratibu wa kutoa ruzuku au mikopo kwa wanafunzi wanaomaliza vyuo vikuu waweze kufungua miradi mikubwa lakini wawe chini ya uangalizi maalumu.

SIDO ipewe nguvu kubwa, SIDO inaweza kutupeleka mbali sana ikipewa nguvu.

Mafundi wana mchango mkubwa sana katika ujenzi wa hii nchi yetu na dunia kwa ujumla.

Mafundi walio soma Veta na ma engeneer wa vyuo vya kati.
elimu ni biashara hivyoo kaa kimya
 
Naona Dr.Kimei alisoma huu uzi na kuona mashiko yake na kuamua kulizungumzia bungeni.
Dr.Kimei ni vissionary leader
 
Tun

Tunahitaji watu wenye akili sio watu wenye vyeti.
 
Back
Top Bottom