Je, ni kweli Mke/Mume anaweza kuwa na gundu au mkosi kwenye familia?

Watu mmen'gan'gana na nyota nyota....hakuna Cha nyota sugueni goti na mtapata majibu..shetani yupo kazini shauri yenu
 
Habari wana jamvi, tumshukuru Mungu kwa uzima aliotujalia na kwa walio wagonjwa poleni sana.

Nimeona ni vema kuuliza hili jambo kwenu wana jamvi kwani humu kuna watu wengi na wenye uelewa wa mambo mengi katika maisha.

Iko hivi, kuna mwana familia mwenzetu amekuwa akipitia changamoto huu mwaka wa pili sasa. Anadai ameanza kupata changamoto hizo nzito zisizo na majibu baada tu ya kuoa tu mwishoni mwa mwaka juzi.

Before alikuwa na maisha yake freshi tu na kazi nzuri. Baada ya kuoa tu akiwa na miezi michache akasimamishwa kazi. Ndugu yangu huyu ni fighter sana akanza kusaka michongo kwingine huku na sisi jamaa zake tukimsaidia kupata connection amegusa mambo mengi sana huku akifanikiwa kufanya Interview 7 mbili kwenye mashirika ya nje lakini mpaka hivi navyoandika hapa hola hajawahi hata kuitwa kazini.

Alikuwa na biashara ya stationary nzuri kabla ya kuoa nayo imekufa amefunga. Yaani yamemtokea mambo mengi tu mara kuumwa magonjwa yasiyoeleweka, pikipiki yake kuibiwa na sasa chuki imekuwa kubwa kwa mke wake akidai ana mkosi kwani kila inshu anayojaribu haifanikiwi na maisha yamekuwa magumu sana kwake.

Jamaa anataka kuvunja ndoa akomae mwenyewe, sasa je hii ni kweli jamani mke au mume anaweza kuwa chanzo cha mkosi kwenye maisha na kusababisha maisha au mambo kukwama? Mkewe ni mcha mungu sana na alimtoa kwenye ulokole akaja RC. Jambo hili familia inampinga sana ila hatuelewi.

Ushauri wenu ni muhimu sana. Nimeweka udhi huu najua na yeye yuko humu na ataona ushauri mtaotoa.
Hakuna gundu kwenye maisha
Ukifanya mema utavuna mema, na ukitenda mabaya utavuna mabaya

Kila baya linalokujia ni mavuno ya mabaya unayoyafanya wewe mwenyewe

Ukipata balaa kwenye kazi zako, au biashara yako, au Safari zako, au mahusiano yako, jiulize ukamilifu wako kwenye njia ya MUNGU wako ikoje!

Acheni utapeli, ukatili, uongo, uasherati, unyanyasaji, majivuno, chuki zisizo na sababu na mengineyo mtaona mafanikio ya maisha

Tuache kubebesha wanawake lawama za ajabu ajabu
Aliye mkamilifu wa Tabia aweza kumuoa mwanamke mchawi na maisha yake yakaendelea kunyoka

MUNGU Kwanza!
 
Back
Top Bottom