Je, ni kweli mapenzi yanaweza kudhitibishwa?

McCain

JF-Expert Member
Dec 2, 2016
1,169
517
Rombo. Mkuu wa Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro, Agnes Hokororo amemweka rumande mwalimu wa Shule ya Sekodari Matolo baada ya kukutwa akifanya mapenzi na mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule hiyo.

Hokororo amesema tukio hilo limetokea (leo Jumatatu saa 12 asubuhi) baada ya mwalimu huyo kuwekewa mitego na wazazi wa mwanafunzi huyo ambapo mwanafunzi huyo alitoroka nyumbani usiku na kwenda kulala nyumbani kwa malimu huyo.

Amesema baada ya wazazi na baadhi ya majirani walizingira nyumba ya mwalimu huyo na kunipigia simu ili akashuhudie wakifanya kitendo hicho.

“Kwa kweli ni jambo la kusikitisha nilifika katika nyumba ya mwalimu asubuhi majira ya saa 12:00 na kukuta akiwa na mwanafunzi huyo huku mwanafunzi akikiri kuwa amekuwa akitoroka mara kwa mara na kuja kulala kwa malimu wake,”amesema Hokororo.

Picture+197.jpg
 
Back
Top Bottom