Je ni kweli maji ya madafu/nazi yanasababisha busha?

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,253
Kutokana na maneno mbalimbali ya watu mitaani, wengi wanadai kwamba maji ya madafu yanasababisha kupata busha. Kwa muda mrefu tumekuwa tunatishwa sana kwamba wanaume tusinywe maji ya madafu au hata maji ya nazi yenyewe.

Pia utafiti zaidi unaonyesha kuwa watu waliozaliwa ukanda wa Pwani yaani; Tanga, Dar es salaam, Mtwara, Zanzibar na Pwani wanaonekana kushambuliwa sana na tatizo hili. Wengine wanadai ni kutokana na ukweli kwamba minazi hupatikana sana sehemu hizi na hivyo kutumika kwa wingi.

Wapo wengine wanadai maji ya madafu yanapambana na malaria.

Swali: Je kitaalamu, ni kweli maji ya madafu husababisha busha? Na uhusiano ukoje?

Nawasilisha.
 
duuh hizi imani bado zipo kumbe.. mkuu
1. tezi dume siyo busha.
tezi dume ni tezi ya kawaida ambayo kila mwanaume anayo. kazi yake ni kutengeneza ute utakaojichanganya na mbegu kutoka kwenye korodani.
tezi dume likivimba au likipata saratani hapo ndipo kuna kuwa na tatizo. na matatizo huwa kwenye njia ya mkojo. ingawa kutokana na kutumia nguvu kusukuma mkojo hupelekea pia kuvimba kwa korodani ( scrotal hernia).
kwa hiyo mtu akimtukana mwenzie kuwa 'ANA TEZI DUME" inabidi umtazame mara mbili kwa maana hajui alisemalo.
2.maji ya madafu hayasababishi wala hayajawahi kusababisha busha.
busha husabishwa na minyoo sawa na inayosababisha matende, minyoo hiyo huenezwa na mbu ambaye hupatikana hasa maeneo ya pwani. mwili unapojaribu kupambana na minyoo hiyo hupelekea kupasuka kwa mirija iliyopo mwilini (lymphatic vessels) na kuanza kuvuja. hivyo maji huendelea kujazana sehemu yenye nafasi.. ndo ikitokea sehemu hiyo ni mfuko wa korodani hapo ndo unaona busha.
 
Hapana, bali waliona mkila sana madafu nazi hazita patikana sokon ndio maana wakaona bora wawatishe kwa hlo, mbn watu wanatumia bat hawapati hlo busha
 
Kwa elimu yangu ndogo ya biology tezi dume na busha are two different things.

Matatzo ya tezi dume huweza sababishwa na bad feeding au life style huwakamata wanaume wengi aged from like 55 years and on....and at tyms kukutibu/check inabdi like wakuangalie kwa kushika maeneo flan flan huko na madaktari wakibongo tena.

(aaargh dadeki, Mungu niepushie. Hujafa hujaumbika. Mambo mengine sikia kwa wenzio tu. )
 
Mkuu maji ya madafu ukichanganya na ndimu ni inasaisia sana kuindokana na ugonjwa wa UTI kama ni mtumiaji wa hivyo kuugua ugonjwa huo inakia nadra sana namaanisha yanasafisha sana kibofu cha mkojo na maji ya miwa pia
 
Back
Top Bottom