Je, naweza kufanya biashara gani kwa mtaji wa milioni tatu?

Feb 5, 2017
37
72
Ninatamani sana kufanya biashara ila biashara gani naweza kuifanya kutokana na mtaji wangu ndiyo sijui. Kutokana na kutokua na uzoefu wa biashara, mtaji wangu ni 3m, nachofikilia kufanya hapa kuna mambo mawili japo sijajua lipi ni lipi.

Kitu cha kwanza ni kuanza biashara ya vipodozi, lakini sijui ninawezaje kuanza biashara hiyo. Je, kwa mtaji huo inawezekana kweli? Kama kuna mwenye kujua zaidi kuhusiana na mishe hii tafadhari anipatie mwongozo.

Kitu kingine ninachokiwaza ni kwenda Dodoma na kuingia minadani kununua mbuzi na kuwapeleka Dar kiwandani. Hii mishe pia sina uzoefu nayo japo nasikia inalipa, mwenye kuijua pia tafadhari naomba mwongozo.

Ila kama kuna mwenye idea nyingine tafadhari usisite kushare na mimi, nipo Mwanza, ila sehemu yoyote yenye fursa naweza kuishi.
 
Kwani hiyo pesa umeipata kwa njia ipi? Unaonaje ungeongeza nguvu zaidi kwenye njia iliyokupa hiyo pesa .
Au ni pesa ya kupewa ?
 
Nunua pikipiki 2.5 uwe boda mkuu.
Bora anunue used 3 za mil 1 each.

Ila me naungana na sayoo hapo juu.

Kama iyo Mil 3 kuna mishe ulifanya ukipata endeleza uko uko ila kama ni ulikua umeajiriwa ukadunduliza sasa ajira imeisha au ulipewa ndio subiri wataalamu waje.

Ingawa haujasema upo wapi ila inaonekana upo Dar.

We una uzoefu na biashara gani au shughuli gani?
 
Kwani hiyo pesa umeipata kwa njia ipi? Unaonaje ungeongeza nguvu zaidi kwenye njia iliyokupa hiyo pesa .
Au ni pesa ya kupewa ?

Kazi yangu ninayoifanya na ambayo imenipa hiyo hela ni kazi ya Boda, mi ni dereva boda, ila nahitaji kuiacha kutokana na changamoto zake, ni kazi ambayo nimeifanya kwa mda mrefu na sasa hivi najisikia kifua kinauma hivyo sasa hivi wazo limeniijia ni kuiacha kazi hii na kuangalia upande mwingine
 
Bora anunue used 3 za mil 1 each.

Ila me naungana na sayoo hapo juu.

Kama iyo Mil 3 kuna mishe ulifanya ukipata endeleza uko uko ila kama ni ulikua umeajiriwa ukadunduliza sasa ajira imeisha au ulipewa ndio subiri wataalamu waje.

Ingawa haujasema upo wapi ila inaonekana upo Dar.

We una uzoefu na biashara gani au shughuli gani?

Pes nimepatia kwenye boda ila nahitaji kuiacha kutokana na changamoto zake hasa za kiusalama, na kwasasa kifua kinauma, na huo ndo uzoefu mkubwa niliokua nao, hivyo nahitaji kupata mawazo mapya
 
Kazi yangu ninayoifanya na ambayo imenipa hiyo hela ni kazi ya Boda, mi ni dereva boda, ila nahitaji kuiacha kutokana na changamoto zake, ni kazi ambayo nimeifanya kwa mda mrefu na sasa hivi najisikia kifua kinauma hivyo sasa hivi wazo limeniijia ni kuiacha kazi hii na kuangalia upande mwingine
Safi kaka fungua duka la vifaa vya pikipiki ila hakikisha kijiweni hapo unakuwa na fundi hapo hapo
 
Bora anunue used 3 za mil 1 each.

Ila me naungana na sayoo hapo juu.

Kama iyo Mil 3 kuna mishe ulifanya ukipata endeleza uko uko ila kama ni ulikua umeajiriwa ukadunduliza sasa ajira imeisha au ulipewa ndio subiri wataalamu waje.

Ingawa haujasema upo wapi ila inaonekana upo Dar.

We una uzoefu na biashara gani au shughuli gani?
Unazijua changamoto za pikipiki used unataka sifa za kuonekana una pikipiki nyingi ambazo kumbe ni mikweche 😆😆usije shangaa kwa wiki unaletewa hesabu mara moja huku service zinahitajika
 
Ninatamani sana kufanya biashara ila biashara gani naweza kuifanya kutokana na mtaji wangu ndiyo sijui. Kutokana na kutokua na uzoefu wa biashara, mtaji wangu ni 3m, nachofikilia kufanya hapa kuna mambo mawili japo sijajua lipi ni lipi.

Kitu cha kwanza ni kuanza biashara ya vipodozi, lakini sijui ninawezaje kuanza biashara hiyo. Je, kwa mtaji huo inawezekana kweli? Kama kuna mwenye kujua zaidi kuhusiana na mishe hii tafadhari anipatie mwongozo.

kitu kingine ninachokiwaza ni kwenda Dodoma na kuingia minadani kununua mbuzi na kuwapeleka Dar kiwandani. Hii mishe pia sina uzoefu nayo japo nasikia inalipa, mwenye kuijua pia tafadhari naomba mwongozo.

Ila kama kuna mwenye idea nyingine tafadhari usisite kushare na mimi, nipo Mwanza, ila sehemu yoyote yenye fursa naweza kuishi.
Tupe mrejesho, ulifanikiwa kuanza biashara gani?
 
ushauri wangu ni kwamba unaweza kufanya biashara yoyote halali ukiwa na huo mtaji wako,kila biashara inalipa na kila biashara inafaida ukiifanya vile inavyotakika,Mimi nakushauri ufanye utafiti mdogo Kwa biashara kadhaa ambazo:
1,Zitaendana na mtaji wako
2,zina risk ndogo
3,zinaendana eneo ulipo.
4,kuna soko la biashara husika.
Baada ya kujua biashara ambayo itaendana na sifa hapo juu,sasa fanya yafuatayo;
1,Tumia Mda kujifunza zaidi kuhusu biashara hiyo na upate ujuzi WA kutosha.
2.Watambue watu wanaofanya biashara kama yako na jinsi utakavyoshindana nao Kwa kuwanyang'anya wateja,sio Kwa uchawi!!!! shindana nao Kwa kuwa mbunifu zaidi ili kuwafanya wateja waje kwako.
3.Andaa mpango wa biashara ambao ni practicable.
4.Tambua kuna mawili kuwin au kufail
5.anzisha biashara yako, Kwa kuzingatia mpango WA BIASHARA ambao umeshauandaa.
sasa ukishaanzisha biashara,kuwa mbunifu,kuwa mvumilivu, tengeneza wateja wa kudumu na kuza biashara yako Kwa kuongeza mtaji au ubora wa huduma/bidhaa
Baada ya kukushauri hayo,ngoja nikupe mfano WA biashara unazoweza kuzifanya japo sio vizuri kwa kuwa sijui mahali ulipo,ujuzi wako na Hali ya eneo lako,ni vizuri ukazingatia haya, anyways hizi NI baadhi ya biashara ambazo huwa zipo profitable maeneo mengi,;
UFUGAJI WA KUKU, KUUZA CHAKULA, Kuuza nguo, kilimo cha mazao, uuzaji wa mazao,Kuuza vinywaji, NK
Kwa ushauri Zaidi unaweza kuwasiliana na Mimi Kwa mawasiliano haya;
Raphael kalolo (mwanafunzi wa shahada ya Kwanza ya biashara Katika chuo cha biashara CBE dar es salaam )
phone/watsapp 0756401790
email: raphaelmathewkalolo@gmail.com
Instagram : raphaelkalolo23
 
Back
Top Bottom