Je, mwenge ni alama ya Taifa au alama ya CCM? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, mwenge ni alama ya Taifa au alama ya CCM?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Hofstede, Jun 3, 2012.

 1. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #1
  Jun 3, 2012
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Nilipokuwa shule ya msingi na baadae sekondari kulikuwa na somo la siasa. Nakumbuka miaka yetu moja ya vitabu ambavyo vilikuwa vya rejea katika somo la siasa ni katiba ya CCM. Ni ukweli usiopingika kuwa bila ya kuijua katiba ya CCM kufaulu somo la siasa ilikuwa ni ndoto ya mchana. Maana enzi hizo tulikuwa tukifundishwa kujua na kukariri majina ya viongozi wa chama na serikali pamoja na vifungu vya katiba ya CCM na ya nchi, pia historia kidogo ndani yake. Lakini pia tulikuwa tukifundishwa kujua alama za Taifa na kati ya hizo ni pamoja na BENDERA YA TAIFA, NGAO YA TAIFA, MWENGE WA UHURU etc.

  Kinachonichanganya ni je mwenge siku hizi umekuwa alama ya CCM au bado ni alama ya Taifa?. Zamani wakati wa chama kimoja nakumbuka mbio za mwenye zilikuwa zikiratibiwa na umoja wa vijana wa CCM ambao ndiyo ulikuwa kama umoja wa vijana wa kitaifa, kwani enzi zetu haikuwa hiyari kujiunga na umoja huwa kama wewe upo sekondari au hata chuo kikuu. Kadi za UVCCM tulikuwa tunapewa tunapo-report form one na katika form ya kujiunga, ukiachana na caution money pia ilikuwepo ada ya kadi ya umoja wa vijana.

  Kutokana na jukumu la mwenge kwa UVCCM, kadi ya umoja wa vijana na sare zake zilikuwa na picha ya 'MWENGE WA UHURU' Juu yake. Lakini baada ya mwaka 1992 kuanzishwa kwa vyama vingi tumekuwa tukishuhudia role ya mavazi ya UVCCM kwenye mwenge kupungua na nafikiri lengo ni kuendelea kuufanya mwenge kuwa alama ya Taifa badala ya kuhusiana na chama fulani. Ndiyo maana leo hii viongozi wa mwenge hawavai tena nguo za CCM. Japo sioni nia wala sababu ya kuendelea kukimbiza mwenge huku tukiendelea kueneza Ukimwi katika mikesha yake lakini siamini kama mwenge huu ambao unatumia pesa za serikali na si za CCM unaweza kuwa associated na CCM.

  Muangalie Bashe na uniform yake ya UVCCM akiwa kwenye mkutano halafu tujadili je Mwenge ni Alama ya Taifa au ya CCM? kupitia umoja wake wa vijana?.

  [​IMG]

  [​IMG]

  Mavazi ya wakimbiza mwenge 2012. Hapa ni mkoani Ruvuma. Je hawa ni UVCCM walijibadilisha mavazi?. Nini hasa faida za mwenge wa uhuru kwa watanzania kama ni mali ya CCM?. Je kila chama nacho kianzishe mwenge wake kama aina ya uhamasishaji wa maendele?
   
Loading...