JE MUDA NI NINI?

JE MUDA NI NINI?

King Octavian

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2011
Posts
403
Reaction score
353
Ni swali ambalo ukiulizwa unaweza kuliona kama jibu lake ni jepesi sana hasa kwa sababu ni jambo ambalo umezoea kulisikia au wengine wanadai wamezoea kuliona, La! Hasha, hili si swali rahisi kujibika, muda ni jambo ambalo linaeleweka vizuri vichwani na kwenye fikra za watu wengi kimazoea tu hasa kwa sababu wanautumia katika namna zote za maisha yao. Lakini umeshawahi kujiuliza maswali haya?

1. Je muda ni nini?

2. Je muda unaishi?

3. Je muda ni wazo tu linaloishi kichwani au ni kitu cha kweli kinachoishi peke yake nje ya mawazo yetu ambacho inatubidi tukitumie kwa uangalifu sana?

4. Je muda unaweza kujitegemea? Au muda wenyewe unaweza kuwepo bila matendo ya ulimwengu na watu kuwepo?

5. Je muda unatembea au umesimama? Kama unatembea kwa sababu gani muda unaenda mbele peke yake na haurudi nyuma?

6. Je muda utakuja kufika kikomo?

7. Unaelewa nini kuhusu NAFASI/MAHALA (space), au Nafasi ni nini?

8. Saa ni nini? Je kuna uhusiano wowote kati ya saa na Muda?

Makala hii itajikita katika kuchambua mitazamo mbalimbali ya watu mbalimbali waliojaribu kujibu swali hilo.

ANGALIZO:
Umakini na utulivu mkubwa unahitajika unaposoma makala hii ili uweze kuelewa nini kinazungumziwa, tofauti na hivyo kueleweka kwake kunaweza kusiwe rahisi kwako msomaji.

MUDA NI NINI?
Muda (Time) ni dhana ambayo imejadiliwa sana na watu katika kuutafuta ukweli wake, Muda wengine wanaita Wakati, wengine wanaita Majira, wengine wanaita masaa au zama. Walijitokeza wasomi, wanafalsafa na wanasayansi wakubwa na maaarufu ambao nao kwa nafasi zao walijaribu kutoka majibu ya swali hili “MUDA NI NINI?” “WHAT IS TIME?”

Katika mijadala yao yalijitokeza makundi matatu yaliyokua na mitazamo inayopingana kuhusu muda. Kundi la KWANZA likiongozwa na mwanasayansi maarufu SIR ISAAC NEWTON, walidai kuwa muda ni kitu kinachojitegemea na ni sehemu ya umbo la ulimwengu ambalo ndani yake ndimo matukio mbalimbali hutokea, kwa maana nyingine ni kwamba Newton alisema Matukio yanatokea katika msatari wa muda ambao tayari upo. Nadharia zenye mtazamo wa kundi hili tunawaita NEWTONIAN TIME.

Kundi la PILI, kundi hili linaongozwa vile vile na mwanasayansi maarufu ALBERT EINSTEIN. katika kitabu chake maarufu kilichopata kuuzika sana kinachoitwa THE SECRET(2014), Einstein alisema, “Time is just an Illusion” (katika tafsiri isiyo rasmi, alimaanisha kwamba “Muda ni mawazo tu au mauzauza au fikra tulizozijenga akilini mwetu ambazo hazina ukweli wowote”).


Wananadharia wa kundi hili wanasema kuwa, muda hauna uhusiano wowote na matukio, wala hauna uhusinao wowote na huo mstari ambao matukio yanaufuata ili yatokee, bali muda ni dhana tu ya kisomi iliyobuniwa inayotumika kuelezea mpishano wa matukio. Yaani muda ni dhana tu akilini mwetu, kusipokuwepo kitendo muda hauwezi kuwepo.

Waliongeza kwa kusema kwamba, Muda hupimwa kwenye nafasi(space) ambamo ndimo matukio hutokea. Matukio au vitendo hivyo ni kama vile, Usiku au Mchana, asubuhi, jioni, kuzaliwa – ukuaji – kuzeeka – mapaka kifo.

Hivyo wanasisitiza kwamba Muda hauishi sehemu yoyote na hauwezi kujitegemea.

Kundi la TATU, hawa ni wananadharia waliokuja na wazo linalopingana na makundi yote hayo matatu yaliyotangulia, wao walisema “Muda si kitu cha kweli/Halisi kinachoweza kujitegemea kama madai ya Newtonian Time yalivyosema wala muda si Mawazo au jambo lililobuniwa akilini mwa mwatu kama mawazo ya Einstein na wenzake yaliyodai”. Bali wao walisema “Muda ni UBUNIFU na KUMBUKUMBU tu za mwanadamu zinazomsaidia kuyafanya mambo yawe ukweli”.

Mmoja wa wananadharia wa mlengo huu MARTIN HEIDEGGER anaamini kwamba Hatuishi ndani ya muda, sisi wenyewe ndio Muda. Hivyo, uhusiano tulionao juu ya wakati uliopita(Past Experience) ni ufahamu wa wakati uliopo(present awareness) katika mambo yaliyopita, Ufahamu huo unaturuhusu kuufanya wakati uliopita uweze kuishi ndani ya wakati uliopo. Uhusinao tulionao kwa wakati ujao (future) ni makisio ya uwezekano fulani, kazi au maungano ya vitu, ni jambo linalotafsiri hali ya mtu kujali kitu au uhusika wake wa moja kwa moja na kitu hicho, kitendo kinachomfanya awe mbele ya mahala alipo sasa (being ahead of oneself) pale anapowaza mambo ambayo hayajatokea (pending occurance). Hivyo basi wanaona kua ile hali ya mtu kujali uwezekano wa mambo Fulani kuweza kutokea vile vile kunaruhusu wakati ujao kuweza kuishi ndani ya wakati uliopo.

Waliendelea kuelezea mtazamo wao kwa hoja mbalimbali.

Sasa watu wanaweza kufikiri kwamba muda ni kitu kinachoishi kwa kusema , “Naikumbuka jana, na jana ilikua kabla ya leo, na hivi sasa nipo leo, unaona sasa, jana si ndio huo muda uliopita?

Walimjibu kwa hoja hii, “kuna wakati uliopo peke yeke (there is only now), mambo yote tunayashuhudia sasa, na sio wakati uliopita,na wala hakuna lolote katika wakati ujao, kuna wakati uliopo tu. Kama ukilielewa hili, jana ni kumbukumbu ya uzoefu wetu tuliofanya ambao hauna uhusiano na muda.

WANAZUONI WA KUNDI LA NEWTONIAN WANAITETEA VIPI HOJA YAO JUU YA UWEPO WA MUDA KAMA KITU KINACHOJITEGEMEA?

Wanazuoni hawa walikuja na hoja inayopinga namna walivyokosolewa, wao walisema kwamba muda ni kitu kinachojitegemea na ni sehemu ya umbo la ulimwengu ambalo ndani yake ndimo matukio mbalimbali hutokea, walisema kwamba Matukio yanatokea katika msatari wa muda ambao tayari upo. Hivyo muda upo tu hata kama matukio hayatokei, kwa sababu muda ni sehemu mojawapo katika umbo la ulimwengu. Waliuliza swali

“Kama Mti ukianguka msituni na ikiwa hakuna mtu yeyote eneo hilo , je mti huo utatoa sauti? Ikiwa hakuna mtu yeyote wa kusikia au kuuona ukianguka?”

Jibu lake ni NDIYO mti huo utatoa sauti. Vivyo hivyo muda upo na unaenda bila kujali kuna matukio au mtu wa kuuona, kuutumia au kuuhisi muda huo.

JE MUDA UNATEMBEA AU UMESIMAMA? KAMA UNATEMBEA KWA SABABU GANI MUDA UNAENDA MBELE PEKE YAKE NA HAURUDI NYUMA?

Embu fikiria kidogo endapo muda ungekua na uwezo wa kurudi nyuma. Ukuaji wa mtu ungekuwa unaanzia uzeeni kwenda utotoni, au baada ya kipindi kirefu mambo yote unayoyajua yanapotea kichwani, mambo yote uliyojifunza yanapotea (unlearning everything you know).

Mijadala mbalimbali imezungumzia dhana ya muda kwenda mbele tu pasipo kurudi nyuma, Dhana hii inafahamika kama ARROW OF TIME.

ARROW OF TIME.
Dhana hii ilianzishwa na mwanasayansi aliyefamika kwa jina la SIR ARTHUR EDDINGTON na ikajipatia umaarufu katika kitabu chake cha THE NATURE OF THE PHYSICAL WORLD (1928). Ni wazo linaloelezea kua muda una uelekeo wa aina moja tu ambao ni uelekeo unaosonga mbele, tofauti na ule uelekeo wa nafasi (dimension of space) ambao wenyewe hauna uelekeo mmoja.

Sasa basi kutokaja na hoja hii ya uelekeo wa muda yalizuka maswali juu ya uhalisia wa muda, moja ya hoja hizo ni hii ifuatayo,

“kuna watu wanadai kua muda unapimwa katika space. Space ni mahali popote ambapo kitendo au matukio yanaweza tokea au kitu Fulani kuwepo. Sasa basi kwenye space ndipo panapimwa kitu kiitwacho Muda"

Ukichunguza tabia ya space au nafasi au mahala ni kwamba ina uelekeo wa aina nyingi ule unaoweza kwenda mbele na unaoweza kurudi nyuma vilevile, mfano mzuri wanao Abiria wanaosafiri katika vyombo vya usafirishaji. Lakini muda ni tofauti, ina uelekeo unaokwenda mbele tu, ikiwa muda(time) unapimwa katika nafasi au sehemu (space) yanapofanyika matukio kwa nini muda haurudi nyuma au hauna uelekeo wa nyuma(never in reverse)? Ni swali gumu ambalo wanafizikia (physician) wamekosa majibu yake mpka sasa”.


JE SAA NI NINI?
Je kuna uhusiano wowote kati ya Saa na Muda?

Wengine waliuliza, sasa kama muda haupo na hauishi kwa nini kuna saa ambazo ni vifaa vinavyotumika kupima muda?

Walijibiwa kwamba, kupima muda hakuufanyi muda kua kitu kinachoishi na kujitegemea. Saa ni kifaa chenye mlio wa sauti ya mziki, tunazitumia sauti hizi za muziki katika kuyapa matukio wakati. Milio hii ya muziki sio Muda bali ni utofautishaji au ufananishaji tu wa matukio yanayotokea. Saa ni vifaa tu vilivyoundwa na watu, tunaviita CLOCKS.

Vifaa hivi huwezi kuviita muda, tunaviita tu vipima muda, sawa sawa na mtu anaweza kupima muda katika siku yenye jua kwa kutumia Barafu ilyoganda. Tunaweza kupanga na rafiki yangu Fulani tukutane sehemu kunywa kahawa baada ya vipande viwili vya barafu kuyeyuka, hapo pia tumepima muda. Hivyo mawazo ya watu yanayoamini kwamba uwepo wa saa ni ushahidi tosha wa kuwa muda unaishi ni fikra potofu. Kwani kinachoifanya saa izunguke sio muda bali ni batteries (betri) au vyazo vingine vya nishati kama vile umeme na jua.

Wewe pia unaweza kujiuliza swali hapa, kwamba kwa nini naiamini saa yangu ya ukutani (clock) au saa yangu ya mkononi (watch) au saa yangu iliyo kwenye simu yangu ikiwa si Muda unaoiendesha saa hii?

Mambo mengi yamezungumzwa ikiwa ni pamoja na kua Muda hauhusiki na kipindi chochote cha maisha ya mwanadamu, wala hauhusiki na uzee wa mtu ambacho ni kitendo cha kibaiolojia cha kuchoka kwa seli za mwili, vivyo hivyo chagua neon lolote katika lugha mbalimbali za binadamu na ulichunguze kama chanzo chake ni muda, utakuta kwamba muda hauna uhusiano na neno hilo.

Lakini pamoja na hayo mimi na wewe bado tuna walakini na mashaka juu ya dhana hili, wasi wasi unaotupelekea bado kuuliza Maswali. JE MUDA NI NINI? au JE MUDA UNAISHI?.

KENZY
d90fa4d7d74483b59e232a8657f6dcb9.jpg
 
Ni mpangilio au utaratibu unaoonyesha saa, dkk na sekunde
 
Mkuu ungejitahidi kufupisha maana dhaaaa kwa kifupi mda ni majira yaliyo ndani ya wakati
 
Mi naona bila matukio hakuna muda.

Lakini bila muda tunaweza kupata matukio.

Mfano.

Tukitaka kuelezea jambo lolote ili tujue limetokea muda gani lazima tuambatanishe na TUKIO.

Mfano

Nimekula ugali mchana.

Hapo mchana ndio muda.

Je mchana ni nini ? Mchana ni wakati ambao jua linawaka,na jua kuwaka ni kitendo.

Hivyo utaona muda ni matukio na sio kitu kingine chochote,hauwezi kuuelezea muda bila kuuambatanisha na tukio.

Mfano wa 2.

Sasa ni usiku ?

Usiku ni wakati gani ?

Ni wakati ambao jua limezama(jua kuzama ni kitendo) hivyo usiku ni kitendo cha kuwa jua limezama so muda wa usiku tunaupata kwa kitendo cha jua kuzama.

Hapo utaona pia kwamba muda tunauambatanisha na yukio ama kitendo fulani.

Sasa jaribu kuuelezea muda bila kuambatanisha na kitendo chochote je utaweza ? Fikira ...😄😄😄

Hahah ni ngumu sana kama haiwezekani.

Hivyo utaona kabisa kwamba Muda ni matukio yanayotokea kwenye ulimwengu,muda sio kitu kingine bali ni matukio.

Kwa mantiki hiyo muda na matukio au matendo ni kitu kimoja,hivyo tunaweza kusema kitu muda ni sawa na kitu tukio.

Kwa maana hiyo watu weeengi wanaodhani kwamba Muda ni kitu tofauti na tukio basi wajue kwamba dhana yao hiyo kuhusu muda ni illusion yaani hakuna kitu hiko,muda na matukio ni kitu kimoja.

Nadhani ndio maana einstein alisema time is an illusion kwa sababu time ama muda lazima uambatane na tukio.

Ukija kudhani kwamba muda ni kitu fulani ambacho kinatofautiana na matukio basi hspo tunasema dhana yako hiyo ni illusion kwa sababu inawaza kitu ambacho hakipo.

Lakini ukisema kwamba muda ni matukio hapo dhana yako hiyo itakubalika haiwezi kuwa illusion kwa sababu unawaza kitu smbacho kipo.
 
Back
Top Bottom